nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
[h=2][/h]JUMATANO, JANUARI 09, 2013 06:49 NA ALPIUS MCHUCHA, RUVUMA
MKOA wa Ruvuma, umepata mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka saba, kuanzia mwaka 2005 mpaka 2012. Kwa kutumia vigezo vya msingi, pato la kila mwananchi mkoani humo, limeongezeka kwa asilimia 31.9 imeelezwa.
Akitoa taarifa ya mkoa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka saba kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, alisema ongezeko hilo limetokana na jitihada kubwa za pamoja za wananchi na Serikali katika kuleta maendeleo.
Alisema Mkoa wa Ruvuma, umekuwa wa sita kitaifa ukitanguliwa na Mkoa wa Dar es Salaam, Iringa, Arusha, Mbeya na Kilimanjaro.
Aliyataja mafanikio katika sekta ya kilimo kuwa, ni uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 652,291 (2005) hadi tani 1,322,128 (2012) na kufanya uhakika wa usalama wa chakula kuanzia ngazi ya kaya na afya za wananchi kuboreka.
Eneo la umwagiliaji, limeongezeka hekta 4,500 zilizomwagiliwa kwa miundombinu ya asili mwaka 2005, hadi hekta 17,655 mwaka 2012.
Alisema hali hiyo imeongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kupitia umwagiliaji wa kisasa kutoka tani 84,096 mwaka 2005, hadi tani 294,018.
Alisema katika sekta ya ushirika, wanachama wake wameongezeka kutoka 22,762 (2005) hadi wanachama 56,047 (2012) na mitaji yake ikiongezeka kutoka Sh 1,781,656,736 (2005) hadi Sh milioni 7,607,213 (2012) na mikopo iliyotolewa ikiongezeka kutoka Sh milioni 1,831,150,835 (2005) hadi Sh 12,244,968,443.
Alisema mavuno kutoka Ziwa Nyasa, yameongezeka kutoka tani 1108.78 zenye thamani ya Sh 704,590,213 mwaka 2005, hadi tani 6,709.12 zenye thamani ya Sh 5,439,239,792, mwaka 2012.