Ruzuku ya serikali ya bilioni mia moja kwenye mafuta ni kituko katika kupunguza bei ya mafuta

Ruzuku ya serikali ya bilioni mia moja kwenye mafuta ni kituko katika kupunguza bei ya mafuta

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Hakika serikali inacheza na akili zetu ni afadhali ingekaa kimya kuliko kutoa matumaini ya unafuu wa maisha ambao haupo.

Ni ukweli uliowazi kuwa serikali imehusika kwa kiasi kikubwa kupanda kwa gharama za maisha kwa sababu ingewezekana kabisa serikali kuchukua hatua za kuzuia kupanda kwa bei za mafuta mapema, kwani jambo hili halikuwa dharula.

Screenshot 2022-05-12 at 18.15.51.png

Naipenda swrikali yangu lakini kupunguza bei kwa kiwango cha senti ambayo hata chenji dukani haurudishiwi,unaweza kusamehe na wala senti hiyo haitumiki tena kupata chochote hapa tanzania ikiwa peke yake sio poa saana.
 
Sio kweli, ni vitu viwili tofauti. Kwanza hapa inaongelea imepunguza.. Effect ya punguzo la bilioni 100 itaanza Juni 1

Pili ruzuku haitafanya kazi mwaka mzima, itahusu kipindi kifupi cha mpito wakati Serikali ikisubiri mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza Julai mosi.

Baada ya Julai bajeti ya ruzuku itafadhiliwa na fedha za mkopo kutoka WB na IMF
 
Amesoma usuluhishi wamigogoro upatanishi mnampa kazi ya biashara ya nishati Mana yake kilakibu analoletewa ni toka kwamtu mwingi nisawa ndo wizara lakini nayeye ajiongeze
 
Bodaboda na watu wengine,kazi IPO,ndomaana mama alisema waziri atakuja kutolea ufafanuzi,neno ambalo alilitumia kimkakati.
 
Hakika serikali inacheza na akili zetu ni afadhali ingekaa kimya kuliko kutoa matumaini ya unafuu wa maisha ambao haupo.

Ni ukweli uliowazi kuwa serikali imehusika kwa kiasi kikubwa kupanda kwa gharama za maisha kwa sababu ingewezekana kabisa serikali kuchukua hatua za kuzuia kupanda kwa bei za mafuta mapema, kwani jambo hili halikuwa dharula.

View attachment 2221840
Kwanini uchaguzi unachelewa? tufanye jambo letu
 
Naipenda swrikali yangu lakini kupunguza bei kwa kiwango cha senti ambayo hata chenji dukani haurudishiwi,unaweza kusamehe na wala senti hiyo haitumiki tena kupata chochote hapa tanzania ikiwa peke yake sio poa saana.
Hivi zile jojo za watoto bei gani?😂😂😂
 
Watz ni wajinga sana aisee!

Kwahiyo mlitegemea kabisa kuna kitu kinafanyika?

Shida ni kwamba mama ana wapiga debe wengi mno
Wewe ni Mrundi?
 
Back
Top Bottom