Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
LOUS RUDOVIKO RWAGASORE SHUJAA NA BABA WA TAIFA WA BURUNDI, CHEMBE CHEMBE ZA UKOMINISTI ZILIMFANYA KUWA MTU HATARI MBELE YA MABEPARI NA KUKATISHIWA MAISHA YAKE KWA KILE KILICHOITWA OPERATION OCTOBER.
Na. Comred Mbwana Allyamtu.
Saturday -7/7/2018 (siku ya Sabasaba)
Kama ilivyo kuwa kwa Sylvanus Olimpio wa taifa la Togo au Samora Machel wa Msumbiji ndivyo ilivyo tokea kwa Rwagasore wa huko Burundi taifa dogo ambalo lilianza kujidumkiza katika siasa za Moscow (USSR) mapema tu wakati wa harakati za ukombozi kwa kujinasibisha na siasa za mashariki (Warsaw pact).
Lous Rwagasore ni waziri mkuu wa kwanza wa Burundi pia ni Baba wa taifa la Burundi hutazamwa Kama muasisi wa taifa hilo ikiwa ni pamoja na kuonwa Kama shujaa wa uhuru katika taifa Ilo la Burundi linalopatikana mashariki mwa Afrika. Japokuwa afahamiki sana kama walivyo wenzake wakina Patrice Lumumba, Julius Nyerere, Nkwame Nkhuruma, Nelson Mandela na wengine wengi barani Afrika. Bado historia yake ni muhimu na yenye mvuto mkubwa sana ndani ya Burundi mpaka Kwenye pembe zote za Afrika.
Kwa heshima yake nchi kadhaa zimemuenzi kwa kuipa mitaa, shule, Vitongoji, Barabara, madaraja na mjengo ya umma jina lake, mfano wa hayo ni barabara ya Rwagasore ya jijini Mwanza, chuo cha Rwagasore kule Mueda Mozambique (Msumbiji) mtaa wa Rwagasore jijini Pretoria huko Afrika ya kusini jengo la kumbukumbu ya tamaduni Cairo nchini Misri na nchini Burundi kuna minara na sanamu yake, noti ya taifa hilo ina picha yake kama heshima kwa taifa lake huku siku ya kifo chake ni siku ya kitaifa.
Burundi pamoja na mambo mengine ni taifa iliyokumbwa na machafuko mengi ya kisiasa,kikabila na mapinduzi kadhaa yalichukua safu ya machafuko yakifuatiwa na mapigano ya miongo kadhaa.
Historia ya machafuko hayo yalianza Mwaka moja kabla ya uhuru wa taifa hilo kwani kulikuwa na uchaguzi wa kwanza uliofanyika chini ya usimamizi ya UN (United Nation) na chama cha UPRONA kilichukua ushindi chama ambacho kilichoongozwa na mwanamfalme Mtutsi Louis Rwagasore.
Yes ni Rwagasore ndio tutamuangazia leo..... Rwagasore huyu ndio aliyemwoa mwanamke wa Kihutu aliyeitwa MARIE ROSE NTAMIKEVYO wa kutoka kabila la kihutu (kabila hasimu kwa Watutsi), Rwagasore aliunda chama cha kitaifa na chama chake kiliunganisha pande zote mbili. Lakini miezi michache baadaye Rwagasore aliuawa na chama chake kilitengana kufuatana na minyukano mikali ya ukabila.
Kufatia kifo chake hatima ya Burundi ikawa njia panda ndipo mwaka 1962 Umoja wa Mataifa uliamua kuipa Ruanda-Urundi uhuru kamili, lakini kila nchi uhuru wake pekee. Baada ya uchaguzi uliofuata wa mwaka 1965 mapigano makali yalitokea tena kwa silaha, na kikundi cha Watutsi wakali wenye misimamo ya kihafidhina (waliokuwa wakiungwa mkono na mataifa ya kibepari) waliidhibiti nchi na kufanikiwa kuichukua serikali.
Katika machafuko hayo Mwaka 1966 mwami alipinduliwa na mwanasiasa Mtutsi Michel Micombero kujitangaza kuwa rais wa nchi na kuifanya nchi kuwa jamhuri. Kuanzia hapo wanasiasa na watumishi wakubwa walio Wahutu walifukuzwa, kukamatwa au kuuawa kwa miongo mingi iliyofuata.
Baada ya kutazama sura nzima ya Mwenendo wa kitaifa katika safu ya kisiasa na historia yake nchini Burundi sasa ni vyema turudi mpaka kwenye viunga vya jiji la Bujumbura ili tujikite kumuangazia muasisi wa taifa hilo mwanamapinduzi na mwanamfarme Lous Rwagasore kama ambavyo kichwa cha makala yetu kinavyojieleza.
PRINCE LOUS LUDOVICK RWAGASORE NI NANI?
Mwanamfalme Louis RWAGASORE alizaliwa katika mji wa GITEGA kusini mashariki mwa nchi iliyokuwa ikiitwa Ruanda-Urundi mnamo tarehe 10 january 1932 katika familia ya kifalme ya kabila la kitutsi kabila ambalo ndio lilokuwa likitawala kimila wakati huo ambapo nchi hiyo ikiitwa Ruanda-Urundi. Jina lake alilopewa wakati wa kuzaliwa lilikuwa ni Rudoviko Rwagasore, baba yeke alikuwa ndio mfalme wa himaya ya Urundi aliyeitwa MWAMI MWAMBUTSA IV na mama yeke alifahamika kwa jina la Therese Kanyonga.
Rwagasore alianza kupata masomo yake mnamo mwaka 1939 katika shule la msingi iliyoitwa Bukeye, huko KANYINYA. Mpaka mwaka wa 1945 alipo hamia Ruanda (Rwanda ya sasa) katika shule iliyoitwa GROUPE SCOLAIRE D'ASTRIDA katika mji wa BUTARE ambapo huko alipata elimu yake kwa miaka 6. Alifaulu vizuri na kuweza kujiunga na chuo kikuu nchini Ubeligiji katika mji wa Anvers ambapo alisomea taaluma ya utawala wa kilimo hata hivyo alishindwa kuendelea na masomo na hakuweza kumaliza chuo na hii ilitokana na Yeye kuanza kujiusisha na siasa za Afrika zilizokuwa zimeanza kupamba moto wakati huo hivyo akaamua kujiunga na makundi ya wapigania uhuru. Mara kadhaa alikuwa akimtaja Abdul Naser Gamal kama mfano wake katika vuguvugu la ukombozi wa Afrika.
Hii ilikuwa ni baada ya kukutana na wanafunzi tofauti tofauti wa kiafrika waliotokea kila pembe ya bara hilo ambao walikuwa Masomo huko nghambo, Rwagasore alifanya uamuzi wa kurejea nyumbani Burundi mwaka 1956 na kuamua kuwa mwanasiasa asiyejali vitisho kutoka kwa wakoloni wa kiberigiji hata hivyo haiba yake na ubora wa mikakati yake ikampa mvuto na ikampatia umashuhuri nchi nzima.
Louis Rwagasore alikuwa mwana diplomasia stadi na mtu mwenye kipaji cha kuongea na kuwaleta watu pamoja. Aliwavutia warundi wengi kutokana na moyo wake wa ubunifu, kwanza aliamua kuanzisha mashirika ya wakulima yaliyolengwa kuwapatia warundi wote uwezo wa kudhdibiti uzalishaji na shughuli zao za kilimo na kuachana na mtindo wa kulima kahawa tu.
Kutokana na uhusiano aliokuwa nao pamoja na wanaharakati wengine mashuhuri wapigania uhuru wa Afrika Mwana mfalme Rwagasore aliweza kukutana mara kadhaa na mwaharakati Patrice Lumumba wa Kongo, Pia alikuwa na mawasiliano ya karibu na Gamal Abdel Nasser wa Misri hii ilimfanya kujijenga hasa kisiasa pia mara kadhaa alikutana na rafiki yake Julius Nyerere (aliye mpa mikakati ya kuazisha vuguvugu la kisiasa).
Kupitia vyama vya wakulima chama chake cha ushilika cha wakulima hakikufika mbali, lakini kiliweza kumpatia umashuhuri na kumpelekea kuunda chama chake cha siasa (kwa ushauri wa Mwl Nyerere) ikumbukwe kuwa Mwl Nyerere ndie aliyemshauli aanzishe chama cha siasa ikiwa ni pamoja na kumtaka abadili muelekeo kutoka vyama vya wakulima na kuanza kudai uhuru nchini nzima ushauri huo uliambatana pamoja na kumtaka aunde chama kitakachokuwa na sura ya kitaifa. Hata hivyo aliunda Chama cha Umoja na Maendeleo kilichoitwa UPRONA, ambacho kilikamilika mwaka 1958 kilichokuwa na wanaharakati kutoka jamii zote za makabila makubwa mawili yani Watusi na wahutu.
Rwagasore alionekana kuanza kuvutika na siasa za Moscow na hii alishawishika kutoka kwa rafiki yake Abdul Naser Gamal wa Misri. Hii ilithibitika baada ya kuonekana akitaka ushawishi wa Urusi katika mapambano yake ya kuitafutia uhuru Burundi,
Mkutano wa kwanza wa chama hicho ulifanyika March 1960 ambapo toka hapo Rwagasore alianza kuomba uhuru wa nchi ya Burundi. Sambamba na kuanza kuwataka wananchi kugoma na kuitisha mgomo kwa raia nchi nzima wa kuacha kazi za kuwatumikia, na wasilipe kodi kwa wazungu. Baada ya mgomo huo wakoloni walimkamata wakamfugulia mashtaka ya kuchochea vurugu na kuhukumiwa miaka 7 gerezani kufuatia kufungwa kwake hali hiyo ilichochea vurugu nchi nzima na kuongeza kasi ya kudai uhuru pamoja na kuongezeka kwa migomo kadhaa nchi nzima hata hivyo wakoloni waliamua kuitisha uchaguzi wa majimbo na halimashauri za miji ambao ulifanyika Tarehe 8 september 1961 uchaguzi huo ulifanyika huku Rwagasore akiwa gerezani chama chake cha UPRONA kilishinda kwa kupata kura nyingi ya 80% ya kura zote.
Wakoloni waliamua kumtoa Rwagasore gerezani Siku chache baada ya uchaguzi na Rwagasore akaunda serekali na kupewa cheo cha Waziri mkuu wa kwanza wa Burundi iliyokuwa imepewa uhuru wa bendera (Dominion Government) kwa minajili ya kuanza maandalizi ya kupanga kamati itakayo shughulikia masuaa ya kuipatia uhuru Burundi mwaka mmoja baadae. Rwagasore alipendelea sana siasa za kikomnsit hata hivyo dalili za hilo zilianza kujionesha mapema tu pale alipo anza kutoa mualiko wa serekali ya Moscow kuhudhuria Kwenye sherehe ya uhuru na kuiacha Marekani jambo hili liliwashutua sana mataifa ya kibeberu ya magharibi.
Hapa ndipo walianza kumuona Kama adui wao na kuanza kusuka mipango ya kuvuruga uhuru wa taifa hilo kwani wiki mbili tu baada ya kuunda kamati ya maandaliz ya uhuru Rwagasore aliuwawa kwa lisasi siku ya tarehe 13 Oktoba 1961 alipokuwa akila chakula cha usiku mjini Bujumbura kwenye Hoteli iliyoitwa Tanganyika.
Baada ya kuuwawa kwake Rwagasore wale walio tekeleza mauaji bila wao kujua nini kiko nyuma ya pazia walikamatwa kwa kufanya mauaji akiwemo mzungu wa kiberigiji aliyeitwa Jean Kageorgis uchunguzi ulifanyika na kubainika hujuma kadhaa hata hivyo walitajwa viongozi wengine wawili wa chama kilicho anzishwa na wakoloni ambacho kilikuwa kikipingana na UPRONA katika harakati za kudai uhuru chama hicho kiliitwa Christian Democratic Party(CDP). Watu hao waliotajwa ni pamoja na Baptiste Ntidendereza na Joseph Biroli watu hawa walipewa mkakati wa kutekeleza mauaji katika sura ya kikabila bila wao kutambua kuwa mkakati huu wa kumuua Rwagasore ni ukoministi ndio ulio mponza.
Mkakati huo ulisukwa vizuri na serekali ya Uberigiji, USA na Uingereza kwa kuyahusisha mashilika yao ya kijasusi. Mpango wa kummaliza Rwagasore ulifaatia baada ya operation Barracuda ya kumuua Patrice Lumumba wa Kongo kumalizika mwaka 1960. Jean Kageorgis aliandaliwa na majasusi wa CIA na M16 kwa kupewa mkakati wa kutekeleza mauaji. Operation hiyo ilipewa Jina Operation October.
Yeah ni operation October iliyopagwa vyema mjini Kampala nchini Uganda siku ya tarehe 1/10/1961 Kwenye makao makuu ya gavana wa Uganda (iliyo kuwa koloni la UINGEREZA wakati huo) mkakati ulisukwa na kupeana majukumu ya utekelezaji wa mauuaji hayo hata hivyo mpango Ilikwenda vyema Kwani wiki mbili tu baadae yani tarehe 13/10/1961 kigaragosi huyo aliyeitwa Jean Kageorgis alifanikiwa kuyakatisha maisha ya Rwagasore.
Hata hivyo mara baada ya mauaji hayo kutokea waliona watumie mtindo wa kuzima kutambulika kwa uhusika wa mataifa hayo ya kibepari wauaji Wote walitiwa mbaroni na Kesi yao iliendeshwa haraka na viongozi hao waliadhibiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa hii ilitokana na kuzima uchunguzi zaidi wa kubaini uhusika wa Uberigiji yenyewe katika uhusika wake.
Hata hivyo mauaji ya Rwagasore yalichochea machafuko kitu kilicho ilazimisha Uberigiji kutoa uhuru kamili (absolute Independence) kupeleka hali hiyo nchi ikapata uhuru wake kamili tarehe 1 julai 1962.
Huyu ndie Rwagasore (Shujaa) wa Burundi ambaye historia yake haitafutika vichwani kwa warundi.
[emoji117][emoji420]Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
[emoji2400]Wako Mjoli wa Historia ya ulimwengu na diplomasia ya dunia......
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
[emoji2398] Copy rights of this article reserved
[emoji2400]written by Comred Mbwana Allyamtu
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com