Rwanda, Burundi na Umoja wa Falme za Kiarabu zimeongezwa kwenye orodha ya nchi zilizowekewa marufuku ya kuingia nchini Uingereza

Rwanda, Burundi na Umoja wa Falme za Kiarabu zimeongezwa kwenye orodha ya nchi zilizowekewa marufuku ya kuingia nchini Uingereza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rwanda na Burundi zimeunganishwa na Tanzania, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Afrika Kusini ambazo pia zimewekewa marufuku hiyo na Uingereza.

Hatua hiyo inalenga kudhibiti kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Afrika Kusini, na marufuku hiyo inaanza kufanya kazi siku ya Ijumaa saa saba kwa saa za Uingereza.

Raia wa Uingereza, Ireland na raia wenye haki ya makazi nchini Uingereza wataruhusiwa kuingia lakini kwa sharti la kujitenga kwa siku 10 wakiwa nyumbani.

Watu wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii walitembelea Dubai majuma ya hivi karibun ,pamoja na kuwepo marufuku ya kusafiri iwapo hakuna ulazima wa kusafiri.

Walisisitiza kuwa safari zao ni kwa ajili ya kazi, lakini idara ya usafiri imesem misamaha yoyote ya kusafiri ambayo kawaida ipo haitakuwepo, ikiwemo kusafiri kwa sababu za kibiashara.

Pia safari za moja kwa moja za ndege za abiria kutoka Uingereza kwenda Umoja wa falme za kiarabu zitapigwa marufuku.

Dubai

Kwa nyongeza ya nchi hizo inamaanisha kuwa nchi 33 zimewekewa marufuku hiyo mpaka sasa.

Waziri wa usafiri Grant Shapps amesema abiria wanaoruhusiwa kuingia Uingereza watahitaji uthibitisho kuwa hawana maambukizi ya virusi vya corona kabla ya kuwasili, vinginevyo watapigwa faini ya pauni 500.

Uwanja wa ndege wa Dubai umesema kuwa ndege za moja kwa moja zinazotarajiwa kuwasili Uingereza baada ya saa saba, saa za Uingereza zimeahirishwa na umewaambia abiria waliokuwa wakitarajia kusafiri wasiende uwanja wa ndege.

Shirika la ndege la Etihad pia limesema ndege zake zq abiria wake wanaokwenda Uingereza zitaahirishwa mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa na wanafanya mipango na wateja wao kuhusu mipango ya kusafiri.
 
United Arab Emirates, Burundi and Rwanda added to travel ban. The government has today (28 January 2021) taken the urgent decision to ban travel to the UK from the United Arab Emirates ( UAE ), Burundi and Rwanda to prevent the spread of the new variant originally identified in South Africa into the UK .2 days ago
1611988377776.png

www.gov.uk › Transport › Aviation

Travel bans extended as United Arab Emirates, Burundi and ..

Haya wazee wa "Saccos" mnao furahia mkiona Bongo wamewekewa vikwazo story nyingi , mara hatupimi, hatufuati masharti ndio maana, tunawekewa vikwazo sasa sijui hizi Nchi nazo wanafuata sera ya Bongo
 
Huu uzi inamaana wale vibwengo wa Ufipa hawajauona ama vipi.
 
Rwanda basi achilieni wananchi wajilinde, kama juhudi zote hizo bado wanasema hamjafanya kitu, njooni muungane na Tz katika kupambana na hilo janga,
 
Na Rwanda imo hii iliyotunyanyasa kuwa tz ina Covid!?
Amakweli Dunia hadaa walimwengu ni shujaa.
 
Mmh Rwanda hii hii yenye kusifiwa na mapambano dhidi ya Corona!!🤔
 
Huu mchezo wa Corona unachekesha sana.
Muingereza yeye ndo Ana wagonjwa wengi .lakini Cha ajabu yeye ndo anakuwa wa kwanza kuwakataza wenzie wasiende kwake
Coronaa ikihamia kwenye ubongo ni MBAYA sana
Screenshot_20210131-095959.jpg
 
Upepo umebadilika kuwa kirusu cha South Africa
United Arab Emirates, Burundi and Rwanda added to travel ban. The government has today (28 January 2021) taken the urgent decision to ban travel to the UK from the United Arab Emirates ( UAE ), Burundi and Rwanda to prevent the spread of the new variant originally identified in South Africa into the UK .2 days ago
View attachment 1689672

Back
Top Bottom