Rwanda Extends a Helping Hand to Haiti After Devastating Earthquake

Hii si kweli. Rwanda hawajatupita. Wana nini sisi tusichonacho?


La hasha! Rwanda wametupita sana maana wana uongozi wa kueleweka.
  1. Rwanda wana raisi na wasaidizi walio na international exposure ambayo inawapa vision, na utendaji tofauti na wa serikali ya JK.
  2. Kikwete ana exposure ya kijiweni (JK). Raisi wetu ni 'Localised' kimawazo, kiuzoefu na hasa kiutendaji.
Ila sina shaka kuwa akisikia Rwanda wametoa na yeye hata kama alikuwa hana wazo hilo atajaribu kujishaua.
 
Kikulacho ki nguoni mwako. Tuna matatizo hilo likowazi na Dawa ya tatizo sio kulikimbia bali kupambana nalo. TZ tunaweza kabisa kufanya maajabu.Ila tumekumbatia mno mambo ya shortcut na deal za kujihujumu sisi wenyewe mpaka tumefika sehemu akili zetu zimeacha kuhangaika kutafuta solution za matatizo yanayotuzunguka.Imagine Rwanda wanaonyesha njia...to me that is what leadership entails!
Tunataka tuone tena mfano gani maana sisi hatuna lolote la kuonyesha zaidi ya hadithi zisizo kwisha na uongo uliokithiri.
 

Mwanakijiji
Huwezi kuilinganisha Tanzania na Rwanda wenzetu wako mbali kwa kila jambo.Sisi wenyewe tunahitaji msaada wa almost kila kitu how can we help them?do we have that capacity especially katika mwaka huu wa uchaguzi?
 
Tulisaidia saana enzi zile za Mwalimu. Ngoja tupumzike kidogo. Rwanda wameona Haiti inastahili kusaidiwa kuliko sisi majirani zao kwa maafa ya Same na Kilosa? Rwanda inatengeneza ukaribu na Marekani kwa kila jambo.
 

Hili nimelipenda sana, kwa kuongezea sifa nyingine ya rais wetu mambo muhimu kwake si muhimu na mambo yasiyo muhimu kwake ndio muhimu. Mfano anaweza kucheza muziki milimani city huku wananchi Same (wapiga kura wake) wakipoteza maisha na asitoe hata kajitamko na anaweza kuagiza kocha wa soccer toka Brazil lakini hawezi kumfukuza kazi gavana aliyethibitika kutusababishia hasara ya mabilioni sh.
 

Mtu wa kijiweni (JK), mpira na kutalii ndio vilivyopo akilini mwake. Kazi ya uraisi imemshinda na ukweli unaonekana hivi sasa kuwa hakupaswa kupewa hata hiyo miaka 5.
 
Mugabe pia aliwahi kutoa msaada kwa wahanga wa tufani huko New Orleans USA. Lakini washirika wetu wa maendeleo wakitoa misaada huwa tunasema kuna kitu wanapata ama wanavizia kitu fulani. Tujiulize, kwa kufanya hivyo Rwanda inapata nini?
 
Blessed is the hand that giveth than the hand that receiveth.
Watch this space and see the blessings that will pour upon Rwanda.
 

Hahahaa... that's a good one
 
this is one of those times that you inspire 'hope' ... kesho kuna mtu ataambuka MA!

HIvi hawa Wanyarwanda wanafikiri wao ni kina nani hadi watoe msaada wakati taifa kubwa kama TZ halina uwezo wa kutoa msaada?

Ni uamuzi tu sasa unasema rwanda mbona DR Congo nao wametoa $2.5m? Si kweli kwamba Tanzania haiwezi kutoa msaada mbona tulitoa msaada wa madawa kwa Zimbabwe?
 
Mugabe pia aliwahi kutoa msaada kwa wahanga wa tufani huko New Orleans USA. Lakini washirika wetu wa maendeleo wakitoa misaada huwa tunasema kuna kitu wanapata ama wanavizia kitu fulani. Tujiulize, kwa kufanya hivyo Rwanda inapata nini?

Mkumbuke Haiti ni waafrika wenzetu na misaada tutawapa tu siyo lazima leo kwani itachukua karne moja kuijenga upya nchi hiyo.
 
Wakati mwingine tusimuonee bure Kikwete, ni nchi ngapi hazijapeleka misaada haiti tena tajiri??? Mwacheni rais afanye kazi zake hata wanaompigia kelele mkiwekwa pale huenda ndo hali itakuwa mbaya.
 
Hatuna haja ya kushindana na Rwanda ktk kutoa misaada kwani hali ya kiuchumi na kisiasa ndani ya Rwanda si sawa na Tanzania.

Ipi hali yake ni Nzuri? Hivi usd 100,000 ni shilingi ngapi za madafu jamani zinazidi gharama ya Nyumba ya Ndulu?
 

Nakataa, nakataa, nakataa. Rwanda hawajatupita. Unless mfafanue "wametupita" kivipi na kwenye nini lakini kama kimaendeleo....hell no. Rwanda ni nchi ya dunia ya tatu kama zilivyo karibu nchi zote za kusini mwa sahara.

Hivi mnadhani serikali ya Tanzania haina dola laki moja? I'm sure we can match if we want to. Na kutoa msaada wa dola laki moja Haiti si swala la kutupita kimaendeleo. Ni swala la ubinadamu tu.

Bado nakataa. Si Rwanda, si Kenya, si Burundi....wote tuko dunia ya tatu.
 
Hizi zote ni Kanuni za Mungu katika mutoaji. Sasa babu yangu sisi hata msaada wa mablanketi tunashindwa sasa haya ni matatizo makubwa sana na tena Haiti ni rangi moja na sisi. Hapa Mungu huwa anawabariki wale watoaji zaidi kuliko sisi tunategemea kupewa zaidi.
 
Kwani kusaidia kuna rangi?
 
DRC wamechangi dola millioni mbili na nusu kusaidi wahanga wa Tetemeko huko Haiti ingawa wachambuzi wa mambo ya CONGO wanasema pesa hizo zingetumika kusaidia kupunguza matatizo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi inayoikabili nchi hiyo.
SOURCE; VOA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…