ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kama Rwanda yenye size ya Mkoa wa Mtwara inaweza kutangaza Utalii wake kwenye kwa kufunga mikataba ya Utalii na Klabu kubwa kama Arsenal na sasa Buyern Munich, hivi Tanzania inashindwa wapi?
Halafu unawasikia wale wanaojiita Viongozi wa Wizara eti wakisema Tanzania itafikisha watalii mil.5 mwaka 2025, watoke wapi? Je, tatizo ni kukosa akili,mikakati au vyote Kwa pamoja?
Hivi kwa Tanzania ni jambo gani ambako tunaliweza na tumelifanya kwa ufasaha?
----
Klabu ya Bayern Munich imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano wa kuendeleza soka na kukuza utalii wa taifa la Rwanda.
Ushirikiano huo uliozinduliwa katika mechi ya kwanza ya FC Bayern msimu huu, utashuhudia klabu hiyo ikifanya kazi mahususi na Wizara ya Michezo ya Rwanda kuanzisha chuo cha soka ili kuimarisha maendeleo ya soka.
Zaidi ya hayo, klabu hiyo itaonyesha chapa ya Visit Rwanda kwenye mbao za LED za siku ya mechi katika ukumbi wa Allianz Arena wenye uwezo wa kuchukua watu 75,000 na shughuli mbalimbali zitaandaliwa ili kukuza utalii na fursa za uwekezaji Rwanda.
Bayern inakuwa klabu ya pili kubwa kuingia mkataba wa kibiashara na Rwanda, Arsenal pia ni klabu yenye ushirikiano na taifa hilo.