Rwanda, Kenya, Uganda, DR Congo na jirani wengine waanza kupokea chanjo ya COVID 19. Burundi na Tanzania - NO DATA YET

Rwanda, Kenya, Uganda, DR Congo na jirani wengine waanza kupokea chanjo ya COVID 19. Burundi na Tanzania - NO DATA YET

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Katika nchi za Afrika Mashariki, inaonesha kuwa ni Burundi na Tanzania pekee ndiyo hazina virusi vya korona na kwa hiyo hawahitaji chanjo ya COVID 19.

IMG-20210203-WA0012.jpg

HOFU na WOGA ni roho za kuzimu na infact ndiyo lango kuu la nguvu za uharibifu na kifo....

IMANI kwa Mungu Baba Muumba wa vyote ndiyo UHAI na MAISHA ya binadamu yeyote...

Simuungi mkono wala kukubaliana na Rais wa Tanzania ndugu John Pombe Magufuli kwa karibu mambo mengine yote...

Lakini hili la IMANI YAKE juu ya gonjwa hili la kutengenezwa na mawakala wa SHETANI na KUZIMU na kuiambukiza kwa wananchi wake, naunga mkono na kukubaliana naye kwa 100%....

Huu ni mpambano wa kiroho. Rais Magufuli kachagua upande sahihi kabisa. Na ktk vita hii WANA WA MUNGU watashinda bila shaka...

Kwa hili nasimama na Rais wetu Magufuli. Namwombea kwa Mungu Baba ktk jina la Yesu Kristo wa Nazareth aindeleze imani hii na kamwe asiyumbe...

Si mapenzi ya Mungu watu waugue ugue magonjwa ya ajabu ajabu na kufa hovyo....

Kila mtu akiwa na imani kwa Mungu Baba muumba na kumtumaini yeye peke yake ktk mwana wake Yesu Kristo mwokozi wetu, shetani hana nguvu wala uwezo wa kufanya lolote...

Kwa IMANI hii aliyo nayo, natumaini na Mungu atambadilisha awe Rais mwema na mwenye utu katika nyanja zingine. Aache ukatili, ubinafsi, kiburi, kujikweza, wizi na ulevi wa madaraka na Mungu amsaidie kubadilika completely na kuwa na moyo wa TOBA....
 
Naomba hiyo Covid ikupate wewe na ikuulaze huku ukipumulia mashine alafu tuone huyo Magu atakusaidia nini.

Mnaleta siasa kwenye maisha ya watu kwa kuongea mambo ambayo hata ushahidi hamna.

Pathetic creatures!
 
Acha undezi wewe.
Wewe una mawazo mafupi sana ya kiroho na kimwili.
Nyinyi ndio mtakaoangamizwa kwa kukosa maarifa.

Yaani dunia nzima(Tanzania ikiwemo) inapigwa na Corona, watu wa Mungu (wanasayansi)kwa kutumia akili na maarifa waliyopewa na Mungu wanaumiza kichwa kupata chanjo, halafu wewe na akili zako fupi fupi unapiga domo kusema hutaki chanjo, sijui Corona imeletwa kutoka kuzimu nk.

Hivi wale mapadri, wachungaji na maaskofu, akiwemo mama Getrude Lwekatare, Mchungaji Miti Mingi nk. ambao Corona imewalaza kaburini wao walikuwa wapagani, hawamuamini Yesu au walikuwa wanamtumikia shetani?!

Yaani mtu na akili zako timamu unakataa kitu cha kisayansi (chanjo) na kwenda kushabikia vitu vya kiuwendazimu vya kuokoteza mizizi, sijui nyungu, sijui kula ovyo ovyo pilipili nk.
 
Kwa hiyo mleta mada unaamini unaweza kuponywa kwa imani ya mwingine? wacheni mchezo kwenye mambo ya kisayansi kwa kuleta mambo yenu ya nyungu, mnapandisha joto la miili yenu bure tu, tena na hili joto la Dsm ndio mnajiua haraka kwa ujinga wenu.
 
Serikali ikifikia hatua ya kuagiza hayo ma chanjo, tafadhari isinihesabie, maana stochanjwa
 
Nilivyosoma hapo no data... Inamaana wahusika hawana takwimu au hawapo ofisini...

No data Ni tofauti na Kuandika 0, sifuri Ina maana kubwa kwamba hamna mgonjwa
 
Acheni UTOPOLO hii kitu ..inauwa ...mambo ya majivu kuwa sukari TUTAVUNA
 
Nashauri vaccine iletwe ila isifanyiwe kampeni ili ataeona haina noma aende kuchanja na maninja kama JPM na mimi tuwasubiri tuone kitawatokea nini?
 
Tumeombewa ,na kuaminishwa kwa mungu kwamba Tz haina corona.
 
Naunga mkono hoja, hatuhitaji kufuata mkumbo kuchukua chanjo ya majaribio bila kujiridhisha kama kweli tunaihitaji.
 
Naomba hiyo Covid ikupate wewe na ikuulaze huku ukipumulia mashine alafu tuone huyo Magu atakusaidia nini.

Mnaleta siasa kwenye maisha ya watu kwa kuongea mambo ambayo hata ushahidi hamna.

Pathetic creatures!
Kijana wewe ni mpuuzi sana! Leo hii unamkejeli Mungu kisa chanjo za hao wanadamu ambao wameumbwa na Mungu mwenywe.

Ila nyinyi siasa zitawapekeka pabaya, kipindi kile napo hivyo hivyo ooh sijui Mungu ana kazi nyingi za kufanya lakini Mungu huyu huyu aliendelea kuwa nasi!

Chunga sana kauli zako kwa Muumba wako!!
 
Back
Top Bottom