Rwanda: Masharti kupambana na Covid19 yalegezwa

Rwanda: Masharti kupambana na Covid19 yalegezwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rwanda imetangaza kulegeza masharti ya kupambana na kusambaa kwa maambukizi ya Virusi vya Korona. Zikiwa zimepita siku nne baada ya Rais Paul Kagame na Mkewe kupata chanjo

Agizo litatekelezwa kuanzia Machi 16, 2021. Watu hawatatakiwa kutembea kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri na biashara zimetakiwa kuwa zimefungwa saa mbili usiku. Magari yataruhusiwa kuingia Kigali kutoka majimbo mengine

Watakao kuwa wana mikutano watatakiwa kutozidi 30% ya uwezo wa ukumbi wa mkutano. Kwa vikao vya watu kuanzia 20 watatakiwa kuwa kwanza wamepima na kuthibitisha kutokuwa na maambukizi

Wananchi wametakiwa kufuata Miongozo ya Afya kwa watakaokaidi watapewa adhabu.

1615883563479.png

1615883589128.png
 
Back
Top Bottom