Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Nchini Rwanda, wasichana sita na mwanaume mmoja wamekamatwa na Kitengo cha kuchunguza uhalifu - RIB kwa tuhuma za kuchapisha video za utupu mitandaoni.
Video ya mrembo mmoja anayeitwa Kwizera Emelyne ilisambaa mitandaoni akionekana akifanya vitendo vya ngono, vinavyochukuliwa kama utovu mkubwa wa maadili. Kwizera ni kiongozi wa kundi linalojiita "Rich Gang" kwenye mtandao wa WhatsApp linalohusishwa na vitendo hivyo.
Msemaji wa RIB Dr Murangira Thierry amesema vijana hao wa kati ya miaka 20 hadi 28 wanachunguzwa kwa kurekodi na kuchapisha video wakifanya vitendo hivyo na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameingilia kati na kuonya dhidi ya alichokiita, taifa kwenda mrama huku jamii ikitazama tu.