Rwanda yaanza mkakati wa kupima Corona Vijijini

Rwanda yaanza mkakati wa kupima Corona Vijijini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Wakati aina mpya ya kirusi cha Corona- Delta kikiripotiwa nchini Rwanda, serikali ya nchi hiyo imeanza mkakati wa kuwapima wakaazi kuanzia vijijini hadi mjini. Sambamba na hilo pia serikali ya Rwanda inakusudia kutoa vyakula katika familia zilizoathiriwa na agizo la kusalia ndani ambalo limewekwa kwa muda wa siku kumi kuanzia Jumamosi iliyopita kukabiliana na corona.

Serikali ya Rwanda imesema licha ya kuweka agizo la kutotoka nje kwa muda wa siku kumi katika mji mkuu Kigali na katika wilaya nyingine nane zenye maambukizo mengi, bado zoezi la kuwapima wananchi wengi kadri inavyowezekana litasaidia kubaini ni kwa kiwango gani virusi vya Corona vimesambaa nchini humo.

Zoezi hili la upimaji litafanyika kutoka ngazi ya kijiji ambapo wananchi wote wametakiwa kupimwa. Kwa kawaida mwananchi hutakiwa kujigharamia mwenyewe kipimo cha Corona, gharama yake ikiwa ni faranga elfu kumi sawa na dola kumi za Marekani.

Maoni ya wananchi yamekuwa mengi; "Nimefarajika sana kupimwa maana kwa kawaida inakuwa siyo rahisi kupata pesa ya kujigharamia kuchukua vipimo.Bahati nzuri nimekuta bado niko salama lakini hiyo haina maana kukiuka masharti ya kujiepusha na tatizo hili hapana." Mwananchi mwingine alisema kuwa "Corona haichagui yeyote kila mmoja anaweza kuathirika kwa hiyo nimefurahi kwa kuwa nimeweza kupima bure,nahamasisha na wengine kuja kupima maana wanaweza kuathirika pasipo kujua."

Waziri wa afya wa Rwanda Dkt. Daniel Ngamije amesema zoezi hili la upimaji linanuia kupata picha kamili ya jinsi virusi vya corona vilivyosambaa nchini.

"Hadi mwishoni mwa zuio la kukaa ndani tutakuwa angalau tumepima watu katika sehemu maambukizi mengi kama vile wilaya 8 na katka mjii mkuu wa Kigali.Lengo upimaji huu ni kupata taswira ya uzito wa tatizo la maambukizi miongoni mwa wananchi.Naili upate majibu sahihi lazima upime idadi kubwa ya wananchi ili iwe sampuli ya mikakati utakayochukua badaaye".


DW Swahili
 
Mnyarwanda amewekeza sana kwenye korona ila wafanyabiashara wa kule wamefilisika kabisa sijui hata wataanzaje maisha baada ya korona kwisha
 
Back
Top Bottom