..wengine ambao tunaishi karibu na misikiti na makanisa adhana na kengele ndiyo alarm clocks zetu za kutuamsha asubuhi.
..inawezekana Kagame kajipatia tenda ya kuagiza alarm clocks Rwanda, sasa hapo anajaribu kuondoa upinzani ktk soko/biashara.
mnajua maana ya religion tolerance, tusimsupport tu kagame tu, maeneo kama SA mbona kanisa na miskiti wanaendeleza mambo yao kama kawaida....sheria hiyo haifai TZ kwani sisi ni watu wa kupendana na umoja popote pale unapo mkuta m tZ hasa nje ya nchi na wenzake utaligundua hilo
Elewa mwandishi alichoseme.HAJAWANYIMA UHURU WA KUABUDU.Bali wamekatazwa KUPIGE KELELE? Mungu anayeyaona ya moyoni hata kabla hujayatamuka iweje leo mpige makalelele hivyo.hata kwa hao mabwana zetu dini zilipochipukia hawapigi kelele hivyo.Na mimi nakerwa kweli.Du ndugu yangu hapa nadhani unahitaji kuelimishwa tu, huo uchafuzi wa mazingira kwa sauti/kelele ni lazima viwango fulani vifikiwe ndio uchafuzi huo utimie, na kwa sauti za makanisa na misikiti nyingi hazifiki huko. Kwa karne hii kiongozi wa kuigwa si yule mbabe bali anayetawala kwa misingi ya kidemokrasia, hapa inamaanisha uhuru wa kuabudu pia. Kwa kigezo hicho tu Tanzania haipaswi kuiga kutoka kwa Kagame ila Kagame anapaswa kuja kujifunza hapa ni kwa jinsi gani raia wenye dini mbalimbali wamepewa fursa ya kuabudu na uhuru wao unalindwa katika katiba ya nchi(tazama ibara ya 19 katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2006.) Huo usumbufu kwa raia una maanisha raia gani tena ambao si waumini? unajua kwa sasa watu wasio waislamu wala wakristo ni chini ya asilimia 2 tu? tena wengi wa hao wanafuata imani nyingine na za kiyahudi, kibudha n.k ambazo zinasitiza umuhimu wa uhuru watu kuabudu.
Kama Generali Kagame kalewa madaraka, nivizuri apumzike awapishe wengine amabao bado wanakiu ya kuongoza nchi. Kwa serikali kuingilia uhuru wa kuabudu ni sawa na mwanadam kujichimbia kaburi yeye mwenyewe.Ni vizuri Bw Kagame ajifunze kwanza yanayotokea Notthern and South Ireland baina ya wakatoliki na wa Protestant,kiaha ajifunze yaliotokea nchini Afghanistani baina ya waislam na utawala wa kikominist chinin ya USSR. Kisha namuomba Bw Kagame arejeshe kumbukumbu zake za kihistoria kwa yale yaliotokea South America, baina ya Wkatoliki na srikali ya Fashist Samoza wa Sadinista.Siku zote wa Mungu ndio hushinda na sio watu wa shetani. Hii ni ishara ya wazi kuwa Bw Kagame sasa aanza kuporomoka kihadhi hasa baada ya kufanikiwa katika mageuzi ya kiuchumi tangu atawale nchi Rwanda takribani miaka 14 iliyopita. Ama kweli Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Sasa Kagame achafua mandhari ya mema yote aliyoyafanya kwa Wanyarwanda. Kama yeye ni an Atheist/Agronist, isiwe ndiyo sababu ya kuwazuwilia watu wangine kutekeleza yale yaliomo katika imani zao za kidini.Huu ni ushetani na kamwe hauwezi kuvumilika na hatimaye ni kuzuka vita vingine ambavyo vitapelekea kumwagika kwa damu za Wanyarwanda wasio na hatia bure breshi.Kagame hapo umechemsha kama si kupasha moto.
Hivi na nyinyi mna nyumba gani ambazo makelele ya nje yanaishia ndani? acheni kulaumu waumini jengeni nyumba bora ili muepuke kelele za mitaani, na pia mtusaidie na sisi na makelele yenu huko vyumbani yanatupa wakati mguu tunapopita karibu na madirisha yenu na watoto wetu....utasikia baba mbona mama nanii analia?
Jamani..sound doesnt matter peace is louder than voice -thats why we fall in to confrict!!
what you think is haven is a hell to some one who dont think so!!
Rwanda think that is not noise people are washiping !!
Rwanda acheni ubaguzi think kwanini ukae kwenye kelele...
sipendi hili wazo!!
Hili ni suala la mipango miji- Dogo kua na heshima na wakongwe!! hivi ume tumwa na serikali ya Rwanda nini?-hueleweki, kelele si ibada wewe,unawahubiria walioko nje au waliohudhuria?tena inapokuwa bugudha inafifisha hata maana ya ibada.njue kuna wagonjwa, wtoto wamelala,watu wamechoka halafu mijinga kuchaa inapiga kelele,si waislamu hata walokole wale wa kuimba kucha,baa miziki mtani,marufuku,big up baba kagame tutaiga mfano wako tukishaing'oa ccm
Hili ni suala la mipango miji- Dogo kua na heshima na wakongwe!! hivi ume tumwa na serikali ya Rwanda nini?-
Mipango miji waangalie wapi watoe au wajenge msikiti/kanisa la kakobe /ukumbi wa hip hop/ viwanja vya michezo-- huu wote ni upumbavu tuna shindwa nini kuandaa mazingira ili kuondoa vurugu zisizo kua na sababu!!...
mkileta mzaa nita wazalilisha!!
mipango miji wewe dogo hakuna tanzania tutasubiri hadi tufe,halamashauri bado saaana tuu,iliyopo tuondoe kelele kwanza mipango itafuata bidae kwani tushashindwa,hivyo huu uhuru wa kupiga makelele hovyo usimame,kwanza ni kosa kisheria kupiga makelele tosha kabisa kumtia mtu au kikundi hatiani!!so mipango wait till 2030 may be! kwani changes zinatokea at the speed of a snail!
kagame ana weza akawa mvuta Bangi tu au alisha wahi kufanya hivyo...Kagame is right, unajua kuabudu ni uhuru sasa isiwe taabu kwa watu wengine, halafu mimi sioni point watu kuanza kuchangia kuwa Kagame amepotea au amelewa madaraka, angelewa madaraka basi angepiga dini marufuku, lakini alichopitisha ni watu kuwa waastarabu na kuabudu pasipo kubughudhi wengine, kwani nani alisema pasipo abudu kimya kimya Mungu hasikii------------mimi huwa nakereka na haya mapokeo ya kusali huku watu wakilia na kupiga muziki utafikiri sasa watu wamefungulia dansi, tuwe waastarabu na tusali kwa utulivu nafikiri Mungu atatusaidia tu na kusikia maombi yetu.
Rom