Rwanda yatangaza kugundua mafuta, kuungana na nchi nyingine zilizogundua mafuta miaka ya karibu kama Namibia, Uganda & Ivory Coast

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Usikute yamegundulika huko Mashariki ya Kongo, wanatuandaa kisaikolojia wakianza kuchimba wa wizi tusishangae wakiwa wauzaji wa mafuta.

Ila nawaona sympathyser wa Mr Slim mnajitahidi kumtengenezea PR
 
KENYA,UGANDA wameweza kutafiti na kutangaza.Sisi tuna nini?,kwa nini wao?Tulianza siku nyingi utafiti wa mafuta,lakini tupo kimya!Tanzania Tunaogopa nini?
Kama ni bonde la ufa,na kwetu limepita(Ziwa Tanganyika nalo lipo katika bonde la ufa).Wenzetu (Uganda)mafuta wamepata katika ziwa lilopitiwa na Bonde la ufa),iweje sisi hatufuatilii eneo hili?!

Somalia wana mafuta,nchi zinazotuzunguka wana mafuta kulikoni
Tanzania, tusiwe na dalili ya mafuta?!

Baharini mkondo unaounganisha na nchi za uarabuni utakuwa unafika hadi mipaka ya bahari ya Tanzania(Kwa nini sisi hatutaki kufuatilia kama nchi?!)

Makampuni yalisajiliwa kufanya utafiti wa mafuta,mbona majibu ya Tafiti hayatangazwi? wanakaa nayo kimya?!
 
Wamechelewa! Mafuta sio deal leo na kesho. Juhudi kubwa zinafanyika za kuachana na matumizi ya Mafuta, na zinaendelea vizuri sana.
Mafuta hayajawahi kuwa Deal sana kwa nchi husika zaidi ya Makampuni Husika yanayoform Cartels (Seven Sisters) ingawa sio hapa hata ukipewa makombo yanaongezea kwenye furushi....

That said ni aibu kwa Mtanzania kuwacheka hawa ambao kama wakifanikiwa kwa hilo huenda sisi kwa Akili yetu Tunatumia LPG Kupikia (Badala ya Umeme ambao tunao) basi na sisi tutakuwa wateja wao wa kununua hio LPG ambayo huku hatuna...

Kwahio utaona kwamba kama akili ni Nywele sisi tuna Vipara...
 
KENYA,UGANDA wameweza kutafiti na kutangaza.Sisi tuna nini?,kwa nini wao?Tulianza siku nyingi utafiti wa mafuta,lakini tupo kimya!Tanzania Tunaogopa nini?
Unashangaa kwanini hatufanyi Tafiti wa kitu ambacho huenda unaweza ukasema kinahitaji uwekezaji, wakati kuna kitu ambacho tunacho (UMEME) na bado watu wananunua LPG kutoka nje ili kupikia na Watunga Sera wanahangaika kumpa Mpikaji Kijijini Mitungi ya Bure ili awe Teja wa kununua kitu ambacho kina gharama zaidi ?

 
Hayo mafuta yatakua na kazi gani ikiwa tunaenda kutumia umeme na gesi asilia?
Matumizi ya mafuta hayataisha kamwe. Sema bei itapungua tu. Bado mafuta ndiko plastics zote zinakopatikana. Mitambo ya viwanda bado itatumia greese, heavy fuel n.k. bado lami kwenye ujenzi wa barabara. Hata huo umeme utazalishwa na mafuta ndiyo mchaji magari yenu kisanii mkijidai kulinda mazingira
 
Ukitaka kuchoma Mahindi ya jirani kila siku bila wasiwasi na asikuulize wewe lima kabustani kadogo tu nyumbani kenye mashina matatu tu kisha itangazie jamii una hekari kadhaa huko mbugani.
 
Are you serious 😐 ulaya yenyewe bado haijatoka huko ktk kutegemea mafuta
Kwa sasa gas ni potential sana kwenye maeneo mengi kuliko mafuta,ni revolution inayofanyika taratibu itafikia stage gas itahitajika zaidi kuliko mafuta ikisaidiwa na umeme
 
Kwa sasa gas ni potential sana kwenye maeneo mengi kuliko mafuta,ni revolution inayofanyika taratibu itafikia stage gas itahitajika zaidi kuliko mafuta ikisaidiwa na umeme
Nakubaliana na wewe ila sio leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…