Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Ryanair kuwalipisha abiria wake huduma za choo
Saturday, February 28, 2009 1:28 AM
Shirika la ndege la safari za bei rahisi Ryanair linategemea kuanza kuwalipisha abiria wake kila watakapokuwa wakitumia vyoo vya ndege zake katika safari zake zote.
Shirika hilo la ndege lenye maskani yake nchini Ireland limeamua kuanzisha mpango huo utakaokuwa wa kwanza katika huduma za ndege angani ili kuwalazimisha abiria wake kutumia angalau paundi moja wakiwa kwenye ndege hizo.
Akiongea katika kipindi cha asubuhi cha BBC mkuu wa shirika hilo Michael O'Leary alisema " tumefikiria kuweka mashine za kuingiza sarafu za paundi moja kwenye milango ya vyoo vya ndege zetu ili kuwafanya abiria watumie angalau paundi moja wakiwa kwenye ndege".
"Tunafikia njia za kuzifanya safari zetu ziwe za bei rahisi zaidi lakini tunafikiria pia njia za kuingiza fedha ili tuendelee kushusha bei za tiketi zetu".
Akizungumzia hatua hiyo mkuu wa utafiti wa jarida la But Which? Holiday alisema "Inaonyesha kwamba Ryanair inataka kuchuma fedha za haraka haraka, pia Ryanair imeonyesha jinsi gani wanavyojali faida kuliko faraja za abiria.
Msemaji wa kampuni pinzani ya safari za bei rahisi easyJet alisema kwamba kampuni yao haina mpango wa kuwalipisha abiria wake watakapotaka kutumia vyoo vya ndege zao.