Ili treni yetu ya kutoka dar kwenda Moshi iwe na tija, nashauri ikarabatiwe angalao ifikie kiwango cha kutembea masaa 10 tu. Tofauti na hapo watu wataachana na usafiri huo mapema sana. Angalao ninapotaka kusafiri usiku, basi iwe usiku kweli, angalao kuanzia saa moja usiku kutoka moshi na kufika Dar kabla ya saa 12 asubuhi ningekuwa mteja wa kudumu wa usafiri huo badala ya mwenendo wa sasa ambao mtu unautumia usiku na nusu ya masaa yako ya mchana.