Saa 1 usiku Dar, saa 12 asubuhi niko Moshi and vice versa

mkaliman

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2014
Posts
878
Reaction score
1,110
Ili treni yetu ya kutoka dar kwenda Moshi iwe na tija, nashauri ikarabatiwe angalao ifikie kiwango cha kutembea masaa 10 tu. Tofauti na hapo watu wataachana na usafiri huo mapema sana. Angalao ninapotaka kusafiri usiku, basi iwe usiku kweli, angalao kuanzia saa moja usiku kutoka moshi na kufika Dar kabla ya saa 12 asubuhi ningekuwa mteja wa kudumu wa usafiri huo badala ya mwenendo wa sasa ambao mtu unautumia usiku na nusu ya masaa yako ya mchana.
 
Kwa reli ipi mzee

Huwa naitumia barabara ya mombo frequently .

Reli ipo Karibu Sana na barabara imechoka Sana nyasi zimeota Kuna siku mvua ilinyesha pale korogwe ilikopita marufiko yakatokea ikawa haionekani.

Usafiri wa treni ni nafuu ila wakarabati hio reli kwa kubadilisha mataluma na kuinuia udogo baadhi ya maeneo Kama inawezekani.

Bila chuki .
 
Mazigazi, ]Maoni yangu kwa serikali ni kuiboresha na kuifanyia marekebisho makubwa badala ya kuiungaunga na kurejea safari za miaka ya 90.
 
Hatua moja baada ya nyingine. Muda si mrefu SGR ya Dar, moshi, Arusha, Musoma itaanza
Thubutu yako! :-: huwa nashindwa kuelewa why we launch big projects wakati hii mingine ikisuasua.,kwa nini tudiende step by step
 
Nalipongeza shirika la reli TRC kwa kufanyia kazi maoni ya wananchi, japo bado hawajaweza kufika Moshi au Dar saa 12 asubuhi lakini wameweza kuingia Mkoa wa Kilimanjaro saa 12 asubuhi na baadaye Moshi na Dar saa 2 asubuhi. Tumebakisha masaa 2 tu tuweze kufikia matamanio ya wananchi na wapenzi wa usafiri wa Treni ya Kaskazini nikiwemo mimi. Nasubiri kwa shahuku kubwa siku moja treni itoke saa 12 jioni ifike saa 12 asubuhi Moshi. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki TRC, Mungu mbariki Injinia Kamwelwe (w), Mungu mbariki rais wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…