Saa nne na nusu Dar es Salaam - Morogoro, haina siha kwa uchumi wetu

Malalamiko sana yameshatolewa ila wateule hawajui hili maana wao wana blue lights au zile 50km/hr haziwahusu, yaani wapo above traffic rules, T1 ni highway, ondoa pedestrians, bodaboda, bajajis, uchafu wa matuta toa wote na hii barabara ijengwe upya sio kuitia viraka
 
Dar es salaam mpaka Morogoro ni umbali usiozid kilometa mia mbili lakini muda unaotumika kwa sasa hasa mabus ya Abiria ni masaa manne mpaka matano.Hii haina tija kwa uchumi wa nchi.Ni lazima lifanyike jambo la haraka.
Zamani watu waliokuwa wakisafiri kwa treni kutoka mikoani walipokuwa wanafika alfajiri Morogoro walikuwa wanashuka na kupanda Coasta kwenda Dar ambazo zilikuwa zikitumia saa mbili tu kufika Kariakoo ambapo ndipo ilipokuwa stendi ya mikoani baada ya kuhamishwa kutoka Kisutu. Unbungo ilkuja baadae sana miaka ya 90s
 
Nishawahi endesha gari toka Mwenge dar mpaka round about ya Morogoro pale morena nafikiri ni foleni tupu, njia nyembamba, malory mengi, ma trafic wapuuzi.

Soln: Train tu basi.
 
Eti highway ina limit ya 50kph😬?! Highway ina tuta kama mnalima viazi😡, highway ina njia moja kwenda moja kurudi😮‍💨, mtu unataka kuingia au kutoka highway hakuna njia ya kuchanganyia spidi au kupunguzia spidi yabidi aliye nyuma yako apunguze kutoka 120kph mpaka 20kph kukusubiri uchanganye au upunguze kutoka hiyo highway🤬🤬🤬, highway ng'ombe wanavuka barabara🤧.

Kuna haja ya kwenda Ujerumani (autobahn) au USA watu wakajifunze nini maana ya highway na inatakiwa iweje.
 
Zamani watu waliokuwa wakisafiri kwa treni kutoka mikoani walipokuwa wanafika alfajiri Morogoro walikuwa wanashuka na kupanda Coasta kwenda Dar ambazo zilikuwa zikitumia saa mbili tu kufika Kariakoo ambapo ndipo ilipokuwa stendi ya mikoani baada ya kuhamishwa kutoka Kisutu. Unbungo ilkuja baadae sana miaka ya 90s
Stendi ya Moro ilikuwa Magomenimapipa, baada ya basi moja kupata ajali na kuua abiria wote kasoro mmoja aliyekuwa siti ya nyuma kushoto hizo basi zilisimamisha safari bila shuruti.
 
Magomeni mapipa stendi ilihamishiwa baadae sana mwishoni mwa miaka ya 90 baada ya ujio wa 'usafiri wa Chai Maharage'
 
Duh! Chai Maharage kitambo sana,ilikua maarufu kwa zile Gari aina ya KIA za mizigo zilitumika kubeba abiria,zilikua zinakatwa ubavuni ili iwe kama dirisha ili kuingiza hewa na mwanga.
 
Chai Maharage kwa sasa ni maarufu Unguja hasa unapotaka kwenda miji ya shamba kama Mangapwani hadi Vikokotoni
 
Stendi ya Moro ilikuwa Magomenimapipa, baada ya basi moja kupata ajali na kuua abiria wote kasoro mmoja aliyekuwa siti ya nyuma kushoto hizo basi zilisimamisha safari bila shuruti.
Again mkuu imetoa mfano ambao unajidhihirisha ni jinsi gani watu wapo wajinga, accident it's someone fault sio bahati mbaya, inapotokea ni lazima uchunguzi ufanyike ili kujua chanzo ili isitokee tena, T1 ni barabara ya 70s muda wake ulishaisha kitambo mno we need a new,modern highway, angalia ile kitonga pass bado tunatumia technology ya miaka hiyo, pale ilitakiwa tupapanue,tujenge Arrester, tuweke pit stops za lazima kwa heavy vehicles ili tudhibiti speed zao, kinachofanyika sasa ni politics na traffic officer's wanaojificha kwenye zile blind corners ili kuchukua fedha kwa wanao overtake hii ni craze
 
I concur with you 100%!!! The state of corruption never changes at all
 
Dar es salaam mpaka Morogoro ni umbali usiozid kilometa mia mbili lakini muda unaotumika kwa sasa hasa mabus ya Abiria ni masaa manne mpaka matano.Hii haina tija kwa uchumi wa nchi.

Ni lazima lifanyike jambo la haraka.
Tatizo la muda wa kusafiri vs kilometers za umbali Tanzania ni kubwa! Yaani imefikia hatua huwezi kufanya calculations na zika make sense! Kwanini:
1. Tumeruhusu miji ikue pembezoni mwa barabara kushoto na kulia (tunaita maendeleo).
2. Hakuna tena hifadhi ya barabarani (yale mawe ya Tanroads hayana maana tena)
3. Vibao vya 50 vimetapakaa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa barabara
4. Trafiki na tochi zao wapo barabarani kuvuna pesa kutokana na hivyo vibao
5. Kuna matuta hadi kwenye highways!
6. Barabara zetu nyingi zipo chini ya viwango (Waziri wa ujenzi wa kipindi kile alituibia sana)
7. Barabara nyingi ni finyu lakini zina mambo mengi sana malori, boda boda, daladala, waenda kwa miguu, mabasi, baskeli, guta, mifugo, n.k

Muda mwingi unapotea safarini! Na hapa duniani asset mojawapo kubwa ni muda!
 
Magomeni mapipa stendi ilihamishiwa baadae sana mwishoni mwa miaka ya 90 baada ya ujio wa 'usafiri wa Chai Maharage'

Again mkuu imetoa mfano ambao unajidhihirisha ni jinsi gani watu wapo wajinga, accident it's someone fault sio bahati mbaya, inapotokea ni lazima uchunguzi ufanyike ili kujua chanzo ili isitokee tena, T1 ni barabara ya 70s muda wake ulishaisha kitambo mno we need a new,modern highway, angalia ile kitonga pass bado tunatumia technology ya miaka hiyo, pale ilitakiwa tupapanue,tujenge Arrester, tuweke pit stops za lazima kwa heavy vehicles ili tudhibiti speed zao, kinachofanyika sasa ni politics na traffic officer's wanaojificha kwenye zile blind corners ili kuchukua fedha kwa wanao overtake hii ni craze
Kitonga ilianza kwa kupitisha magari toka upande mmoja kisha kuruhusu magari ya upande mwingine! Hiyo ndiyo Kitonga ya 50's, na ilikuwa juu zaidi kuliko hivi sasa ipo chini zaidi. Tatizo la Kitonga ni mainjinia kutotaka kutumia zege badala yake wanatumia lami ambayo husukumwa na magari yateremkapo mlima, pia huenda hawana zana za kuipanua au kuchimba mahandaki.
 
Pale ni ulaji pesa zilitoka kupanua barabara kuwa njia nne lakini wapi wakala mafisadi kwa kuingia mikataba ya ovyo kwa barabara nyembamba.
 
Back
Top Bottom