bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Mwezi wa Aprili umefika na Bunge la Machi-Aprili limemalizika usiku wa kuamkia leo. Ni wakati mzuri watanzania tutumie muda huu kwendelea kutafakari maudhui iliyomo kwenye Katiba Inayopendekezwa na tufanye uamuzi sahihi bila kuyumbishwa na upepo na elimu za kila namna. Katika kipindi hiki cha mwezi Machi tumeshuhudia na kuona pia kusikia mengi. Tumeweza kubaini kama kambi kuu mbili na ndogo ya tatu kuhusu kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa. Kambi ya kwanza na ambayo imesikika sana na kuvuta hisia za waliowengi kwa mtazamo hasi na chanya ni ile ya wanaosema hapana kwa katiba hiyo. Moto huo ulishika kasi baada ya baadhi ya viongozi wa dini kuwataka waumini wao waisome katiba inayopendekezwa na kufuatilia vipindi vya wa elimu kwa umma kuhusu katiba i nayopendekezwa na hatimaye waipigie kura ya hapana. Kambi ya pili ni ile i liyobeba mtazamo wa serikali unaowataka watanzania kuisoma katiba inayopendekezwa na mwishowe kujitokeza kwa wingi kuigia kura ya NDIYO Katiba Inayopendekezwa. kundi la tatu ambalo lilikuwa ni dogo ni la wale wasio na upande. Kwenye hapana hawapo na kwenye ndiyo hawapo. Mumo humo kukazaliwa na wanaharakati waliotaka katiba isipite nao wakasema yao mengi tukayasikia. Wakaibu ka pia na opinion leaders ambao nao walitaka wafuasi wao waisome Katiba Inayopendekezwa wafanye uamuzi sahihi kutokana na walichokisoma. Cha kushangaza huo ushauri uliotolewa na kiongozi mmoja wa dini ushauri usio na upande wowote tafrani kubwa ikaibuka. Wapo waliomuunga mkono lakini hao hawakusikika sana ila waliosikika ni wale waliompinga na kumkashifu mzee wa watu hadharani bila kujali afya yake kwamba katika kipindi hiki afya yake ni mgogoro. Wakamsema karibu kila neno baya. Siwezi kuyarudia waliosema kwani nami nitakuwa nashiriki kumkashifu bila kujua Mzee wangu huyo. Katikakitu kilichoonekana kama sinema ya James Bond kwa wale. Waliokuwepo enzi za senama hizo mnakumbuka sinema hiyo ili yokuwa ikivutia:emptybath::lock1:Tulishuhudia mchunga kondoo akimshambulia mlisha kondoo kwa maneno makali kama wembe huku akikimbia huku na huku kusisitiza pointi zake akiwa na kundi fulani alilokuwa akikimbia nalo mchunga kondoo huyo. Sinema haikuishia hapo tuliona mchunaga huyo akiwa mikononi mwa ndugu zetu wanovaa sare fulani na kofia bapa wakiohojiana na mteule huyo. Nini kiliendelea! Si mteule kawa hawezi yaani kazimia na alipozinduka alijikuta ndani ya hospitali. Patamu hapo! La kumshukuru Mungu mlisha kondoo mwenye kundi kubwa la kondoo nchini akamsamehe mchunga kondoo. Akafanya kama bosi wake alivyowasamehe waliomtesa kwa kusema baba uwasamehe kwa maana hawajui walitendalo . Baada ya hayo yote nikakutana na kijana ananiuliza "Baba hivi Mahakama ya Kadhi iko ukarasa wa ngapi wa Katiba Yenu, nikamwambia Katiba ni hiyo hapo soma ila ninachojua hukana Mahakam hiyo kwenye katiba. Akasema mbona viongozi wetu wa dini wametwambia kuwa imo na ndo mana wanaipinga. Nikamjibu kuwa siyo kweli mahakama hiyo haimo. Kesho yake niliporudi nyumbani kijana alinipokea kwa furaha baada ya salamu aksema kumbe Kumbe Katiba hii ni nzuri sana nimeisoma. Hapo nami nikazidi kuuelewa kuwa wengi hawajaisoma Katiba Inayopendekezwa ndo mana wanalishwa kila uchafu na sumu toka kwa wanaharakati wa kimwili na kiroho. Ndugu niachie hapa na kukwambia kuwa soma katiba na uilewe kisha piaga kura ya Ndiyo kwa maana uzuri wa katiba hii nimeuona. KAZI KWAKO.:majani7: