mimi naomba watanzania wenzangu tupigie iwe cuf au chadema chaguo ni lako lakini usipigie ccm, utakuwa unatukuza ufisadi na kuulea, tunatakiwa tuanze upya kwani tumepotea.
kuna watu wametuibia saana na tuna wajua lakini tunaendelea kuwapigia kura
mfano Mzee kingunge na ujamaa wake kwetu sisi wananchi, wakati fam,ilia yake wanafanya umafia,
kuna viongozi wengi tu wanaiba na kuja kutuhonga chumvi, sukari na kanga, kapelo, wakati watu wa sehemu zao wamedumaa kielimu, mazingira, umeme , nyumba mbovu mbovu nk nk, ni juu yetu kuyakata haya.
sawa anasema ametengeneza barabara, blah blah, je katika kuzitengeneza hizo barabara ubora umezingatiwa? je gharama ni za haki au zingine ndio zimekwenda kuchangia chama? ukwepaji wa ushuru kwa viongozi na watu wao iwe wafanya biashara nk , je huku ndio kupiga rushwa na ubadhirifu? reli ndio hivyo wamewapa rites/wamejipa wenyewe mtaji kwa kukodisha vichwa badala ya kuvinunua? je huu ndio utawala bora aliyo leta?
madini yameondoka bila kuwapatia wahusika shule bora, barabara bora, usafiri uliyo bora, nyumba zilizo bora, elimu bora nk nk, walio neemeka ni viongozi na makuwadi wao, je huu ndio maisha bora kwa kila mtz? msidanganyike kwa yeye kuhudhuria mazishi, kupiga picha na vitoto, au wazee akijifanya ana wathamini saaana, kama kweli ana wathamini, serikali yake isingewazulumu/kuwaibia watu kwa mikataba mibovu inayopoteza mamilioni, angjikita katika kujenga shule/mahospitali mengi angefunga milango ya wizi na ukwepaji kodi, lakini badala yake amekuwa aakibariki mambo hayo kama teuzi nyingi anazo fanya zinaonyesha, mfano ni ATCL, TANESCO ya Idrisa, nk nk.
kumlea kagoda