Sababu 5 kwanini unahitaji kufokasi kwenye njia moja ya kutengeneza fedha kwa wakati mmoja

Sababu 5 kwanini unahitaji kufokasi kwenye njia moja ya kutengeneza fedha kwa wakati mmoja

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Kuwa na sababu kuu inayokufanya uchague kuwekeza kwenye ardhi na nyumba. Sababu yako kuu ndiyo itakuwa ni chanzo cha hamasa ya kujifunza kwa umakini uwekezaji huu. Wengine hupenda majengo ya kupangisha.

Wengine hupenda kutumia nyumba kuombea mikopo ya kuwekeza zaidi na zaidi. Wengine hupenda uwekezaji huu kwa sababu baadhi ya mbinu za uwekezaji huhitaji muda machache sana ya usimamizi.

Wengine huchagua uwekezaji huu kwa sababu tayari wanazo nyumba ambazo walirithi kutoka kwa ndugu zao za karibu. Wengine hupenda uwekezaji huu kwa sababu ni moja ya sekta kumi (10) zinazoongoza kuwafanya wengi kuwa matajiri duniani.

Wengine hupenda uwekezaji huu kwa sababu una hatari ndogo sana ya kupoteza mtaji fedha wako. Wengine hupenda uwekezaji huu kwa sababu ni uwekezaji unaozuia fedha zako kutoathiriwa na mfumuko wa bei (infalation).

Wengine hupenda uwekezaji huu kwa sababu ni uwekezaji wenye njia nyingi za kutengeneza fedha kwa wakati mmoja.

Wengine hupenda uwekezaji huu kwa sababu ardhi ni bidhaa ambayo haizalishwi. Ardhi haiongezeki. Hivyo kila mwaka mahitaji ya ardhi huongezeka wakati ukubwa wa ardhi ni ule ule tangu mwanzo wa miaka ya dunia hii.

Je sababu yako ni ipi inakusukuma uhitaji sana kuwekeza kwenye ardhi na majengo?.

Uwekezaji Kwenye Viwanja Na Malengo Ni Mpana

Hutakiwi kuwekeza kwenye viwanja mwaka huu na mwaka kesho unawekeza kwenye majengo ya kupangisha.

Hutakiwi kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha ya familia mwaka huu na mwaka kesho unahamia kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha ya biashara.

Hutakiwi kuwekeza kwenye nyumba za kuhamishika (modular/mobile/manufactured homes) na kuhamia kuwekeza kwenye kumiliki majengo ya apatimenti kubwa mwaka kesho.

Kwa kufanya hivi, utakosa ubobezi kwenye akili zako na timu yako kwa ujumla. Ili uweze kujenga utajiri mkubwa sana unahitaji kubobea kwenye aina chache za majengo au ardhi.

Unatakiwa kuanza kuwekeza kwenye kundi la ardhi au majengo ulilochagua mpaka ufanikiwe. Kisha unaongeza aina nyingine ya ardhi au majengo.

Makundi Tofauti Tofauti Ya Ardhi Na Nyumba.

Aina mbalimbali za uwekezaji huu ni kama ifuatavyo;-

✓ Kununua na kuuza viwanja (land flip).

✓ Kununua ardhi ghafi, kuendeleza na kuuza viwanja (land development).

✓ Kumiliki na kupangisha majengo ya makazi ya familia chache.

✓ Kumiliki na kupangisha majengo ya biashara.

✓ Kumiliki na kupangisha majengo ya makazi ya familia nyingi (Multi-family rental houses).

✓ Kumiliki na kupangisha majengo ya wageni (lodging industry).

✓ Kumiliki na kupangisha nyumba zinazohamishika (modular/manufactured/mobile homes).

✓ Kutengeneza na kuuza nyumba za kuhamishika (nyumba za konteina).

✓ Kuwekeza kwenye miji ya mbali (long-distance real estate investing or virtual real estate investing in real world).

✓ Kumiliki ardhi na majengo kwenye ulimwengu wa kufikirika (virtual real estate investing in apparent world). Hapa ni pale unapomiliki fedha za kigitali za ardhi na majengo.

✓ Kununua na kuuza nyumba kwenye miji ya mbali (virtual wholesaling real estate).

✓ Kuwekeza kwenye ardhi na majengo maeneo ya mjini au majiji makubwa (real estate investing in urban areas).

✓ Kuwekeza kwenye ardhi na majengo maeneo ya pembezoni mwa miji au majiji makubwa (Real estate investing in sub-urban areas/peri-urban areas).

✓ Kuwekeza kwenye ardhi na majengo maeneo ya vijijini (Real Estate Investing in rural areas).

Kwa haya niliyo orodhesha hapa ni mambo mengi mno. Unahitaji kuanza na jambo moja tu kati ya haya kama kweli unahitaji kujenga utajiri mkubwa ndani ya muda mfupi.

Makundi yote ya hapo juu unaweza kuwekeza kwa kutumia mbinu zifuatazo;-

✓ Kutoa huduma za mikopo ya ardhi na majengo (servicing mortgages).

✓ Kumiliki majengo ya kupangisha tu (holding rental houses).

✓ Kununua na kuuza majengo (house flipping).

✓ Kutoa ushauri unaohusu ardhi na majengo (real estate consultancy services).

✓ Kumiliki viwanja kwa lengo la kuja kuuza baada ya miaka 10, 15, 20 na kuendelea (land banking).

✓ Kununua na kuuza viwanja ndani ya miaka miwili (2) tu (land flip).

Sababu 5 Kwanini Unahitaji Ubobezi Kwenye Aina Ya Viwanja/Majengo.

Unahitaji kubobea kwenye aina moja ya ardhi na majengo kwa sababu aina zote hizo hutofautiana kwenye mambo yafuatayo;-

✓ Tabia za hali za masoko yao (real estate markets).

✓ Ujuzi wa usimamizi bora katika kila aina (Unique management skills).

✓ Mbinu za mauzo matangazo ( marketing and sales strategies).

✓ Njia za kupata mitaji fedha (financing real estate).

✓ Upekee wa eneo ambapo aina ya ardhi au nyumba ipo (location, location, location).

Kwa maneno haya machache ninakushauri uwe mbobezi wa aina chache za majengo au viwanja na ujenge mafanikio makubwa ndani ya muda mfupi.

Hatua Sita (6) Za Kubobea Kwenye Aina Chache Za Majengo Au Viwanja.

MOJA.

Jifunze elimu ya msingi ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Jifunze maarifa yote ya msingi ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Hii itakusaidia kuchagua eneo linalokufaa kujenga utajiri mkubwa.

Baada ya kujifunza kutoka kwa wabobezi washauri wa ardhi na majengo unaweza kuachana nao au ukafanya maamuzi ya kuwekeza.

Kwenye hatua hii unatakiwa kujifunza kutoka kwa angalau wabobezi watano (5) wa ardhi na majengo. Kisha utamchagua mmoja wa kuendelea naye kwenye safari yako ya kujenga utajiri mkubwa kupitia ardhi na nyumba.

MBILI.

Chagua aina moja hadi tatu za ardhi na majengo.

Kisha Jifunze kila kitu kwenye aina hizo tatu (3) ulizochagua. Hapa unatakiwa kujifunza chini ya uangalizi wa menta au kocha uliyemchagua kwenye hatua ya kwanza hapo juu.

TATU.

Chagua aina moja tu ya ardhi au majengo ambayo inakufaa kuanza kujenga utajiri mkubwa kupitia ardhi na majengo.

Jifunze kila kitu kwenye aina ya majengo uliyoamua kuwekeza. Mfano; mimi nimechagua nyumba za familia chache.

Kwenye hatua hii unatakiwa kujifunza kwa vitendo kwa 80% na asilimia 20 zinazobaki unajifunza kwa nadharia. Menta au kocha wako ndiye atakuwa kiongozi wako mkuu wa jinsi ya kufanya haya.

NNE.

Chagua mbinu bora inayokufaa kwa ajili ya aina ya ardhi au majengo uliyochagua.

Mfano; kutoka hatua ya kwanza. Mimi nimechagua majengo ya familia chache. Je nitakuwa napangisha au nauza ndani ya miaka miwili (2) tu baada ya kumiliki).

TANO.

Anza uwekezaji wako ukiwa na kocha wako.

Utakapopata mafanikio makubwa unaanza kuongeza aina nyingine ya majengo au aina ya ardhi. Kwa kufanya hivi, utapunguza sana makosa ya kiuwekezaji.

Hivyo ndivyo unaweza kubobea na kujenga utajiri mkubwa kwa haraka kupitia filamu katika ardhi na majengo.

SITA.

Rudia hatua ya kwanza hadi hatua ya tano.

Hapa unatakiwa kurudia hatua hizi pale unapotaka kuhamia aina nyingine ya majengo. Hivyo utaanza kujifunza misingi yote kama hukuwahi jifunza hapo mwanzo.

Akili yako ya sasa itakuwa tofauti sana na ulivyokuwa mwanzo. Hivyo utajifunza maarifa sahihi kwa haraka haraka na kuchagua aina ya majengo ya kujenga utajiri wako kwa haraka.

Kama hauna muda wa kufanya yote haya jenga timu bora itakayokusaidia kufikia lengo lako kuu la kujenga utajiri mkubwa ndani ya muda mfupi kupitia uwekezaji wa ardhi na nyumba.
 
Back
Top Bottom