Sababu 8 muhimu kwanini biashara au huduma yako inahitaji kuwa na Website

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
3,211
Reaction score
993


Kama walivyo wamiliki wengi wa biashara ndogo au za kawaida, unaweza kudhani biashara yako haitafaidika ikiwa utaiweka kwenye website/tovuti au unafikiri ni gharama sana kumiliki website. Au labda unadhani kwavile pengine wewe hutumii computer basi hata wale ambao wanategemewa kuwa ni wateja wako nao pia hawatumii computer.

Kumbe ndivyo sivyo. Wakati mwingine hata wale wenye biashara kubwa kabisa unashangaa hawana website!

Zifuatazo ni sababu 8 muhimu kwanini biashara au huduma yako inahitaji kuwa na website bila kujali ukubwa wa hiyo biashara:

1. Biashara yako ndogo itapata kuaminiwa


Siku hizi, wateja wengi wengi zaidi hutafuta bidhaa au huduma wanazohitaji kwenye mtandao wa intaneti. Biashara yako ndogo itapata kuaminiwa ikiwa utaipa website. Bila hivyo, wateja wale ambao wangeweza kuwa wako wataendelea kwenda kwa washindani wako ambao wameweka biashara zao kwenye mtandao. Kama tayari unayo website lakini haipo kisasa zaidi au haiendani na wakati uliopo unao uwezo wa kutaka irekebishwe ili kuipa biashara yako muonekano wa kitaalam na hata kuaminiwa zaidi.

Website inaweza kuwa msaada mkubwa kwa wale wafanyabiashara wanaofanya biashara zao kutokea nyumbani kwani huna duka la kuzionyesha hizo bidhaa au huduma yako mbele ya mtu yeyote.

2. WEBSITE inaokoa pesa zako


Kwa vile labda biashara yako siyo kubwa au maarufu sana unaweza kudhani labda hutaweza kumudu gharama za kuwa na website yenye muonekano wa kitaalam zaidi, hata hivyo ni gharama zaidi kutokuwa nayo. Ingawa gharama za uundaji wa website zinatofautiana sana toka kwa mtengenezaji (designer) mmoja hadi mwingine, lakini ikishakuwa imeundwa ipo juu, gharama zake za uendeshaji mara nyingi hazizidi elfu 10 au elfu 20 kwa mwezi.

Ukilingalisha na gharama ya tangazo moja kwenye gazeti au TV, wakati ungeweza kuwafikia wateja wako wengi kwa kuwa na website yako na ambayo unaweza kuziorodhesha bidhaa nyingi kadri uwezavyo na zikaonekana kila siku masaa 24/7. Website ndiyo njia rahisi kabisa katika kuitangaza biashara yako.

3. Itakuwa chanzo cha taarifa kwa wateja wako


Ifikirie website yako kama ni kipeperushi au katalogi yako iliyopo hewani muda wote. Ni rahisi na haraka zaidi kurekebisha au kubadili (update) taarifa yoyote kuhusu bidhaa yako na huduma katika website yako muda wowote kuliko katika gazeti, hivyo kurahisisha taarifa kwa wateja wako kujuwa kuna bidhaa gani mpya, ni lini bidhaa mpya itawasili, kuna matukio gani yajayo, promosheni mhimu, au kutambulisha huduma nyingine yoyote katika biashara yako.

Tofauti na kwenye magazeti ambapo matangazo yako yanaweza kupitwa na wakati kirahisi (outdated) na hili linaweza kutokea siku ya pili tu maana mtu akishasoma gazeti la leo siyo rahisi kesho kulisoma tena gazeti hilo hilo, website yako inabaki kuwepo hapo hapo ikitoa taarifa na habari zilizopo na hata zitakazofuata 24/7/365.

4. Website inapatikana muda wote


Tofauti na duka au ofisi yako ambayo ukifika muda fulani jioni lazima uifunge ukapumzike, website haina muda wa kufungua wala kufunga. Wewe unaweza kuwa umelala usingizi saa nane za usiku lakini kuna mteja anapekuwa na hata kuagiza bidhaa katika website muda huo!

Website ipo hewani masaa 24/7/365 wazi kwa yeyote popote alipo iwe Tanzania au popote duniani ili mradi tu awe na intaneti, na sasa kwa mapinduzi yaliyofanywa katika simu kila mtu ana intaneti mkononi mwake!. Kwa maisha ya sasa ya kutingwa na shughuli nyingi, wateja wengi wanapenda kutafuta bidhaa na kuagiza kupitia mtandao wa intaneti ili kutopoteza muda na gharama.

5. WEBSITE inakuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi.


Iwe unauza bidhaa au unatoa huduma yoyote, website yako itakuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi siyo wa eneo lilipo duka lako au huduma yako tu bali popote pale duniani watu watakapohitaji bidhaa au huduma kama yako. Kwahiyo kama biashara yako ipo Dar, website yako inaweza kumuonyesha na kumuuzia bidhaa mteja aliyopo Mbeya muda wowote katika siku.

Mara nyingi nikiamka asubuhi nakuta ripoti kwenye website yangu kuwa fulani bin fulani alikuwa kwenye website yako akisoma ukurasa fulani saa nane usiku na akajaza fomu kuwasiliana na mimi au ameniachia email yake niwe namtumia makala zangu!, umeona? unaweza kuwa umelala usingizi kabisa lakini kuna watu wanaperuzi website yako popote walipo duniani.

Unauza korosho upo Mtwara na wateja ni wachache hapo ulipo? Weka website unaweza kuwauzia hata waliopo Uingereza na Marekani ili mradi zina ubora unaokubalika. Unadhani huwezi kuuza bidhaa au huduma yako kwenye mtandao? Usisahau hata magari na nyumba vinauzwa kwenye mtandao!

6. Website inakupa njia ya kuonyesha kazi zako, bidhaa na huduma zako


Haijalishi ni biashara ya aina gani unafanya, website ndiyo namna pekee nzuri kuonyesha kazi zako. Kwa kujumuisha au kwa kuzionyesha kazi unazozifanya (portfolio) au kwa kujumuisha ukurasa wa picha za kazi unazozifanya na hata kuwa na ukurasa wa shuhuda toka kwa wateja wako namna walivyohudumiwa na wewe, website inakupa namna ya pekee kujitangaza.

7. WEBSITE inaokoa muda


Kutoa maelezo ya kila bidhaa kwa wateja wako uso kwa uso ni kazi ngumu na inayohitaji muda na wafanyakazi wengi, hii ni hata iwe ni kwa simu, email au kipeperushi (brochure) bado ni jambo linalopoteza muda mwingi. Lakini ukiwa na website kazi yako ni kuorodhesha bidhaa zako moja baada ya nyingine pamoja na maelezo yote kuhusu hiyo bidhaa hadi bei yake, linabaki kuwa jukumu la mteja kubonyeza bidhaa anayoitaka kuisoma na hata kuagiza huku wewe wakati mwingine ukiwa umelala usingizi kabisa.

Wakati huo huo inahimizwa kuweka bidhaa mpya kwenye website yako kadri zinavyoongezeka dukani kila siku au mara kadhaa katika wiki. Wakati website yako imeshaundwa na tayari inafanya kazi, inabaki inapatikana kwa wateja wako muda wote bila mwisho au muda wa kufunga huku ikiokoa muda kwa upande wako. Na unajuwa muda ni nini? Muda ni mali (Time is money)!.

8. Website inaboresha ubora wa huduma yako kwa wateja wako


Labda unauza bidhaa ambazo ni nzuri kwa mazingira au haziharibu mazingira na ungependa kutoa maelezo juu ya namna ya kuitumia au namna ya kuitupa mara baada ya kuitumia au labda wewe ni mhasibu na unapenda kuwapa maelezo mhimu wateja wako juu ya namna ya kurahisisha utunzaji wa vitabu vyao vya mahesabu.

Kwa kujumuisha ukurasa wa ‘Maswali na Majibu' (FAQ), kuongeza makala au kutuma ujumbe kwa barua pepe kwa wateja wako ili kujibu maswali yao wateja wako, inaweza kukurahisishia kuwapa taarifa juu ya nini kipya au kinaendelea katika biashara au huduma yako. Hii ndiyo rahisi kuongeza ubora wa huduma yako kwa wateja wako bila wao kulazimika kupiga simu au kufika dukani kwako moja kwa moja.

MUHIMU

1. Tupo katika ulimwengu wa intaneti na ulimwengu upo kwenye intaneti.

Karibu asilimia 80 ya wateja wanatumia intaneti kutafuta bidhaa mbalimbali wanazohitaji kabla hawajanunua. Siku hizi wateja wengi kwanza wanaweza kufikiri huenda kampuni au biashara yako ipo kwenye mtandao na wataitafuta lakini mwisho wa siku wanagunduwa haupo! Wengi wa washindani wako huenda tayari wameweka biashara zao kwenye mtandao, usiendelee kuruhusu riziki yako iendelee kwenda kwa wengine sababu ya kutokuwa na website yako.

2. Kumbuka kuweka bidhaa mpya kila mara kwenye website yako.

Hakikisha katika kuiunda website yako, inaundwa katika mfumo ambao utakuwezesha kuongeza bidhaa zingine au mpya kila mara na kwa namna rahisi kabisa ambayo kila mmoja mwenye uelewa wa kawaida wa kufungua na kusoma email akielekezwa mara moja anaweza kuifanya. Website ambayo ina maliza wiki, au mwezi bila kuongezwa bidhaa hiyo itakuwa na nafasi ndogo kushindana na wengine.

3. Tumia mitandao ya kijamii kuinadi website yako
.

Mara baada ya kuiunda website yako usitulie na kudhani sasa kila kitu kitakuwa sawa, tumia muda mwingi kuinadi kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, goole+, youtube, instagram na kadharika.

Hakikisha kuna namba ya simu inayotumia pia whatsapp ili iwe rahisi kwa wateja wako kuwasiliana na wewe na wewe kuwatumia maelezo mengi zaidi kwani kwenye whatsapp unaweza kuandika meseji yenye ukubwa hata wa kurasa 2 unaweza pia kutuma picha, video na kadharika. Inashangaza kuona kampuni haina hata simu yenye whatsapp inayojulikana kwa wateja wao.

Je utahitaji kutengenezewa website kwa ajili ya biashara au huduma yako? Au unahitaji kufundishwa kutengeneza website? Tuwasiliane +255769142586 pia whatsapp kwa namba hiyo hiyo.
 
Umejitahidi kujiuza vyema. Nitakutafuta unitengenezee kwa ajili ya kampuni yangu. Kazi njema.
 
Umejitahidi kujiuza vyema. Nitakutafuta unitengenezee kwa ajili ya kampuni yangu. Kazi njema.
Ahsante mkuu, hakuna matatizo tuwasiliane

Gharama zako zikoje mkuu
Mkuu nashukuru kwa swali lako. Gharama inategemea na website yenyewe inahusu nini ila kwa haraka haraka ni kati ya laki na nusu hadi milioni 3. Kwa sasa nina ofa kwa website/blog ya mtu binafsi (personal website) ambayo ni laki na nusu kwa yeyote anayetaka kuwa na web binafsi, kwahiyo kama unaweza kusimama wewe kama wewe kwa jina lako ukachagua topic moja ukafundisha wenzio, mimi nipo tayari kukuundia kwa laki na nusu tu. Tuwasiliane.


Asante braza kazi nzuri

Ahsante mkuu, tupo pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…