SABABU HASA YA SISI KUENDELEA KUCHELEWA

SABABU HASA YA SISI KUENDELEA KUCHELEWA

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Si kwa sababu ya kutokuwa na fedha, kama wengi wanavyofikiria, wala ufisadi (ingawaje unachangia), wala si ukoloni!
Sababu kubwa ni viongozi wasio na maono wasiojua priorities, na wasiojua dunia inaelekea wapi. Hilo, ongeza juu yake 'ubinafsi na ukosefu wa uzalendo'.
Kwa nini twahitajia viongozi wenye maono. Chukulia mfano mdogo tu. Katika miaka 50 ijayo nchi zitakazofanya vizuri ni zile ambazo watu wake wana elimu, hasa ufahamu wa kompyuta. Sasa hebu angalia hali yetu hapa Tanzania! Wakati nchi zote za Ulaya siku hizi kila mwanafunzi ana laptop na kwa kweli mara kadhaa husomeswa akiwa nyumbani, sisi.....sidhani hata kama hili limeanza kufikiriwa. Kisa? Eti ni ghali sana na Tanzania haina pesa hizo!
Lakini ukitazama kwa uhalisia jambo hili si ghali kama kuna mipango na utashi. Kikubwa ili laptop itumike ni umeme. Hivi Tanzania inashindwa kuweka solar panels katika kila shule, halafu kukawa na 'charging points' wanafunzi wanapokuja asubuhi wanacharge? Bei za laptop zimeshuka mno, na nchi inaweza kuingia katika mkataba wa kuuziwa kwa bei hafifu ikiwa si kwa biashara, na pia inaweza kuweka viwanda vya kuzitengeneza. Thamani ya V8 moja inaweza kununulia laptop za shule 10,000! Anza kwa ku-share baina ya wanafunzi kama wanavyofanya Rwanda. Wanafunzi wawili laptop moja.
Na ndiyo hivyo Tanzania inavyozidi kuachwa nyuma kwa vile vipa umbele vyetu (priorities) si vya kutufanya tuendelee. Na maendeleo ni ya watu, si vitu. Mtandao Tanzania umekuwa ni Luxury kiasi kwamba ni watu wachache wana internet majumbani, ukitoa ya vifurushi.
Haya si mambo ya fedha na umaskini, ni ya kuweka vizuri priorities.
Sasa tuwatazame Wanyarwanda baada ya miaka kumi watakuwa wapi kulinganisha nasi!
 
Nape anataka bandari ya bagamoyo ndiyo kipaumbele chake pamoja na masharti yake yeye anataka suala la babake ndiyo litekelezwe.
 
Vipa umbele vyetu!
 
Back
Top Bottom