Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Kwa mwanaume kufanya mapenzi ni muhimu. Kiasi kwamba mwanaume atatumia njia yoyote ili apate wa kufanya naye. Njia mojawapo ni kumdanganya mwanamke. Kumdanganya kazi, umri, mipango au chochote kizuri ili mradi alale naye.
Kwa mwanaume ambaye anapata shida kupata wa kulala naye, akitumia njia hii ni sawa na mtu asiye na kipato ila anaiba ili kuilisha familia yake.
Wanaume wanadanganya sababu ni chaguo lililopo kwa ajili yao. Hii mbinu inafanya kazi sababu mara nyingi wanawake hawaangalii ukweli wa nini kimemvutia kwa mwanaume.
Uongo unafanya kazi sababu unampa mwanamke kitu anachotaka (kifikra) na pia unapomdanganya ni kwamba unamuambia anachotaka kusikia. Ukimpa mtu kitu anachokitaka kifikra/kihisia atakupenda. Hivyo inakua rahisi kuku kubali.
Na anachokitaka mwanamke ni kutakwa na kuwa chini ya mtu mwenye uthamani, mwenye malengo, anayejiamini na anayeweza kumtunza. Mtu akimdanganya kwa hayo anampata kirahisi.
Pia sababu nyingine ni kuwa wanaume wengi hawajui jinsi ya kumwambia mwanamke ukweli bila kuanika kila kitu.
Mwanamke anapenda asikujue sana haraka. Japo anaweza kusema anataka akujue lakini sio haraka. Ukimuambia ukweli wote anakua hana sababu ya kuendelea kutaka kukujua. Unakua umemrahisishia kazi kiasi kwamba hapati motisha ya kuwa nawe. Wanawake wanapenda changamoto kwenye kukujua. Wanaume wawazi hawana changamoto kwa mwanamke.
Kwa mwanaume ambaye anapata shida kupata wa kufanya naye mapenzi, anaweza tumia njia hii ili kujenga kujiamini kwanza kabla hajaanza kujifunza kutongoza kwa kutosema uongo.
Kuna muda ukweli utakukosesha mpenzi, mfano;
- Upo na mwanamke halafu anakuuliza, “Hivi mara ya mwisho ulikuwa na mpenzi lini?”. Unakuta mtu ana miaka 27 na hakuwa na mpenzi muda wa miaka 5, uliachwa na ukamlilia arudi lakini wapi. Ukisema huo ukweli utapoteza nafasi ya kuwa naye. Ila ukidanganya kwamba ni hivi karibuni tu ulikuwa na mpenzi, unaweza kumpata.
Sababu wanawake wanapenda kuwa na mtu ambaye wanajua hata wanawake wenzake wanamtaka.
- Upo na mwanamke anakuuliza “Unafanya kazi gani?”. Lakini wewe kiukweli huna kazi na hujui utapata lini kazi, ukimwambia hivyo atakuona huna uthamani, atakukimbia, lakini ukamdanganya una kazi fulani (inayoendana na kazi uliyowahi fanya/ unayoitafuta lakini ina hadhi) atakuona wa thamani, sababu wanawake wanapenda kuwa na mtu mwenye uthamani.
Lakini haina maana ndio ukalie njia hiyo hiyo miaka yote, ni muhimu ujifunze kumvutia na kumtunza mwanamke kwa mfumo unaosema ukweli na unaomfanya mwanamke akutake mwenyewe.
Share na wengine wapate kujifunza.