SABABU KUU kwanini silipend jukwaa la SIASA

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Aman iwe juu yenu wakuu


Hizi ni sababu ambazo zimenifanya na zinanifanya nisilipende kabisa jukwaa la siasa

A) wachangiaji Wa jukwaa la siasa ni wachumia tumbo. Kwanini nasema hivyo kule kuna watu nahisi wametumwa kuja kusifia na kuponda, kuna watu wao ni wazee Wa kusifia tu na kuna wengine wao ni wazee Wa kuponda na kupinga haijalish kama maada ni nzur au mbaya

B) wachangiaji wamejaa mihemuko. Kwanini nasema hivyo wachangiaji wengi huchangia bila kujua maada inahusu nini na inatakiwa kuchangia nini, unakuta mtu kakoment ( aya kachukue buku saba yako)
(Ndo mbowe alivyo kutuma)
Unakuta mtu ana hoja ya msingi lakin akiisema anambiwa (nenden kwanza mkajenge ofis ya chama chenu pale ufipa ndo uje hapa) au unakuta mtu anaitwa nyumbu au lofa

C. Kule unaweza pata ugonjwa Wa moyo bure. Kwanini nasema hivyo ukikaa lile jukwaa unaweza jinyonga maana utakuna na kashifa nyingi za watu kama akina lowasa, ngeleja, chenge na wengine ambao wamepiga hela za selikar alafu wewe huna hata mia.
Mara uchumi umeshuka Mara umepanda Mara sijui bashite Mara sijui nini Mara dolla imeshuka Mara sijui ndege imekufa, yaan kuna vitu vinaweza kukufanya ukafa

D. Unaweza zeeka kabla ya umri wako kwanini nasema hivyo maana utaanza kuichukia nchi yako na kuona Mara mia ni bora usingezaliwa tz

Nawasilisha sababu zingine nitaendelea kuzindondosha hapa


LONDON BOY
 
Wewe ni kiokote tu kwani kabla hujajiunga jukwaa la siasa si lilikuwa linasonga tu? Andaa jukwaa lako la habari za kina amba ruty ambazo utapata wachangiaji wengi wa kaliba yako! Siasa inahitaji ngozi ngumu mathalan kuna namna nyingi za kufanya siasa lakini namna bora zaidi ni siasa ya harakati (political activism). Siasa ya harakati inadeal na masuala (issues) lakini siasa ya kawaida (conventional politics) inadeal na uchaguzi, madaraka, ushawishi na maslahi binafsi.
 
Kwa hiyo unapendelea jukwaa gani mkuu??
Huyo achana nae! Halafu mkuu,ninaomba unitumie muendelezo wa Ile makala yako nzito ya Biblia kwa jicho lingine! Tafadhali sana mkuu! Kule najua huwezi kuendeleza as wamevamia wale wandugu
 
Umeona sasa haya ndo majibu yenu watu Wa jukwaa la siasa sisi huku hatujazoea mipasho mkuu
 
Kusitishwa kwa siasa za majukwani kumepunguza ladha ya jukwaa la siasa jf, jukwaa hilo sasa imekuwa ni uwanja vita.
 
Kule ubinadamu 0%
utaitwa bwege
Nyumbu
Kibwengo
Lofa
Na matusi mengi makali.
 
kuna watu wanaumwaga magonjwa ya kitoto wakiwa wadogo yanawagharim hadi ukubwani
 
Lile jukwaa na ugonjwa wa moyo ni vitu vilivyo karibu sana hasa kama wewe ni mzalendo au ndo umeanza kutafuta maisha awamu hii... utaona madudu mengi sana ua serikali na kuzidi kukata tamaa ya maisha... maana kila post kule ni majanga tu au habari ambazo kwa namna moja ama nyngine hazina matumaini kwa mendeleo ya taifa... mi nshaachaga kwenda kule kitambo sana... mara usikie misaada imepungua... mara wawekezaji wanaondoka nchini.... mara benki hazitoi mikopo kwa watu binafsi..... mara sijui kodi imeongezeka yani ni presha juu ya presha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…