Sababu kuu tatu za kuweka akiba

Sababu kuu tatu za kuweka akiba

Kaaya10

Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
37
Reaction score
53
Hizi ndizo sababu kuu tatu za kuweka akiba

Dharura. Tunaweka akiba kwa sababu tunajua kuna dharura itatokea na utahitajika kuwa na akiba, dharura sio kwamba hazijulikani hapana, usichojua ni itakuja lini na kwa kiwango gani. Kuna watu wakipata dharura na wana akiba awaitumii eti kwa sababu ni akiba, ujue hujui sababu ya kuweka akiba.

Manunuzi/malipo. Tunaweka akiba kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali na malipo ikiwepo ada za shule, vifaa vya nyumbani, ardhi na vitu vngine vingi.

Kukuza utajiri/kipato. Hapa ni pale unapoweka vitu akiba lakini katika hali ya kuzalisha. Unanunua shamba au nyumba ambayo baadae itapanda bei au utakua unapata kodi na kukuza kipato chako. Unaweka pesa benki kwa riba au unanunua hisa za makampuni ili upate faida baada ya kipindi Fulani cha muda.

Hizi ndizo sababu kuu tatu za kuweka akiba, ongezea za kwako
 
Maisha haya utaweka akiba basi?
Ni kufyeka zote
 
Back
Top Bottom