Uchaguzi 2020 Sababu kuu ya Lissu kushindwa, asilimia 80 ya Watanzania wanaishi Vijijini hawamjui Lissu ni nani, Magufuli anajulikana kila kona Vijijini

Uchaguzi 2020 Sababu kuu ya Lissu kushindwa, asilimia 80 ya Watanzania wanaishi Vijijini hawamjui Lissu ni nani, Magufuli anajulikana kila kona Vijijini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
CHADEMA wamekuwa wakijipa matumaini hewa kuhusu mgombea wao Lissu kushinda wakisema yuko popular sana. Wakisema wanalalia mtaji wa kura za 2015 ambapo Lowasa alipata kura milioni sita.

Kitu kimoja wanasahau Lowassa alikuwa Waziri Mkuu muda mrefu na Waziri aliyejulikana sana vijijini ambako asilimia 80 ya Watanzania ndiko wanaishi na ndiyo sababu yake moja kubwa kuzoa kura nyingi.

Rais Magufuli anafahamika vijiji vyote Tanzania nzima na ndiko wapiga kura wengi walioko, siyo mijini.

Hata mijini Lissu anajulikana miji michache, hasa kwa vijana wanaoshinda mitandaoni, hasa wa Dar es Salaam ambao wengi hata kujiandikisha kupiga kura wengi hawajajiandikisha. Ni washabiki tu wa siasa za mitandaoni.

Pigo kuu la kubwagwa Lissu litatoka vijijini. Natoa siri ya wazi kabisa bila kuficha. Vijijini huyu Lissu hawamjui.Ofisi za CCM zipo kila kijiji na hakuna mwanakijiji asiyemjua Magufuli ni nani.

CHADEMA waliwekeza viofisi vya hapa na pale vya kuzuga kwa msajili mijini viofisi vichache tu lakini vijini vijiji vingi hawako huko ndiko pigo zito la Lissu litatokea.

Ndiyo maana hata mapokezi yake utakuta walikuwa wengi vijana wadogo; hakukuwa na watu wazima na hata maeneo aliyopita watu walikuwa kama wakimashangaa hivi, na watu wazima walikuwa wala hawana hamasa naye, ni vijana mmoja mmoja tu pembeni mwa barabara alimopita walioonyesha hisia za kumshangilia hapa na pale. Ikamlazimisha mpiga kamera afiche kupiga kamera kwa aibu akawa haonyeshi kabisa walio pembeni mwa barabara msafara unamopita.

Kamera yake ikajikita tu kwenye vijana walioko kwenye msafara wake. Anayebisha aangalie hizo video za msafara wake toka uwanja wa ndege hadi makao makuu Kinondoni; camera imekwepa kabisa kuonesha watu waliojipanga kando ya barabara kuogopa aibu sababu hawakuwepo na waliokuwepo hawakuonyesha hisia za kumshangilia. Angalia kamera inawaonesha walioko barabarani tu, ambao wengi walikodiwa kumsindikiza.

Mpiga picha yeyote akiangalia tu anajua walipiga picha tu za kudanganya wazungu pembeni mwa barabara hakuwa na washangiliaji! Pamoja na jiji la Dar kuwa na umati wa watu full time.

Angalia usanii wa CHADEMA Lissu anapungia mikono wasindikizaji pembeni mwa barabara hakuna wapungia mikono.

 
Pigo kuu la pili la Lisu litatoka kanda ya ziwa nyumbani kwa Magufuli.Kanda ya ziwa ndiko kuna wapiga kura karibu nusu ya wapiga kura wote Tanzania kutokana na population yao ,
Kule ni ngome ya CCM na kwao Magufuli na ndiko alikopata kura nyingi uchaguzi uliopita

Kanda ya ziwa ndiko huamua nani awe mshindi sababu kuna wapiga kura wengi kuliko popote Tanzania
Hahahaha jitahidi kujidanganya! Narudia endelea kujifariji tu
 
Pigo kuu la pili la Lisu litatoka kanda ya ziwa nyumbani kwa Magufuli.Kanda ya ziwa ndiko kuna wapiga kura karibu nusu ya wapiga kura wote Tanzania kutokana na population yao ,
Kule ni ngome ya CCM na kwao Magufuli na ndiko alikopata kura nyingi uchaguzi uliopita

Kanda ya ziwa ndiko huamua nani awe mshindi sababu kuna wapiga kura wengi kuliko popote Tanzania


Huko kanda ya ziwa pia ni huku:

Madhila ya Barabara Rusahunga -Rusumo

Ipo tofauti ya kanda ya ziwa, Chatto na usukumani wasikoelimika yaani ambako ujinga tololo ndiyo kwao. Rejea tafiti za TWAWEZA.
 
Kuna aliyekuwa akijulikana kuliko Bashite? Chezea wajumbe.

Kama kwa Watia Nia, Oct. 2020, Wajumbe sasa ni sisi.

Anayekubalika kwani anajificha? Mbona ni yule:

IMG_20200804_210728_515.jpg


Kama huyo unayemtabiria ushindi hayajui hayo, tukutane October.
 
Pigo kuu la pili la Lisu litatoka kanda ya ziwa nyumbani kwa Magufuli.Kanda ya ziwa ndiko kuna wapiga kura karibu nusu ya wapiga kura wote Tanzania kutokana na population yao ,
Kule ni ngome ya CCM na kwao Magufuli na ndiko alikopata kura nyingi uchaguzi uliopita

Kanda ya ziwa ndiko huamua nani awe mshindi sababu kuna wapiga kura wengi kuliko popote Tanzania
Unafahamu yanayoendelea Kanda ya Ziwa juu ya Magu?? Muda utasema ukweli.
 
Hiyo barabara ya rusahunga hadi rusumo watumiaji wakubwa ni malori ya nje na yanayotoka dar es salaam ambao sio wapiga kura walio wengi wa kanda ya ziwa .

Hiyo siyo wilaya za Ngara na Biharamulo?

Hakuna watanzania wanaoshudia vishindo hivi vya awamu ya 5?

Wasubirini wajumbe. Documentary nzuri kuhusiana na barabara hii kuu iko mboni:

Kama mtanzania wa leo ni yule wa jana tukutane October.
 
Kilimanjaro na Arusha wengi walichoma kadi za kupigia kura na kuapa hawaji piga kura baada ya Lowasa kupigwa chini nenda mwenyewe kawahoji Chadema waliopiga kura 2015 hawataki kupiga kura tena.Kazi mnayo kuwahamasisha warudi kupiga kura tena

Nendeni wenyewe mkahoji muwaulize Chadema waliopiga kura 2015 kuwa utaenda kupiga kura?

Mikoa hiyo ya kaskazini ilikuwa ngome ya Lowasa aki ji brand kama mwamba wa kaskazini na alishinda kura nyingi za asante mwanetu .Lisu sio brand nane ya kaskazini ,Hana brand name kanda yeyote!! Magufuli ni Brand Name ya Kanda ya Ziwa.Tundu Lisu hakujenga brand name hata ya kanda yake tu ili akitaka kugombea uraisi awe ana brand kubwa na ngome kanda fulani!! kwake hakuijenga hana kanda!! anategemea abebwe mgongoni na mbeleko kwenye hizo kanda!!! Na mbowe uwezo wa kumbeba Lisu kanda ya kaskazini mwisho kilimanjaro .Arusha na Manyara ni ngome za Lowasa na Sumaye ambao chadema waliondoka bila hata kuambiwa asante .Wenyewe wana hasira na Chadema wenye watoto wao hivyo Mbowe ubavu hana wa kumbeba Lisu Mikoa ya Arusha na Manyara.Masai mtu wao Lowasa ambaye CHadema walimtema Lisu Hawamjui

Kanda zingine zote hakuna kiongozi mwenye brand name wa kumbeba Lisu Ukiondoa tu Mbowe lakini kanda zingine hamna kitu watu wanajulikana tu kwenye majimbo yao Sio kanda .Lisu angekuwa alijiandaa uraisi alitakiwa kujenga brand name very strong walau kwenye kanda moja na kuwa household name .Kujihakikishia kuwa hiyo kanda ndio ngome yake ya kumbeba lakini hana! anategemnea kura za huruma za kuokoteza hapa na pale!!! Very wrong political strategy

Kiufupi hakujiandaa kuwa Raisi .Duniani kote hakuna uraisi wa kushtukiza watu hujiandaa kwa muda mrefu kwa strategy strong
CCM mkubali kuwa mmesha likoroga, Kuna dada ameelezea baba yake amestaafu na mafao yake hajalipwa, amekua akizungushwa kwa miaka mitatu. Amepata stroke sasa na familia inaamini kabisa stress za kutolipwa mafao yake zimechangia pakubwa. Familia nzima inaiona serikali ya CCM ni chanzo. Sahauni kura za familia hii na si moja tu.

Vijana wamemaliza chuo 2015 mpaka leo wako mtaani. Mnawaambia wajiajiri bila hata kuwasaidia mazingira ya kujiajiri huko. Sahauni kura za kundi hili.
 
Back
Top Bottom