Sababu kwanini Diamond atazidi kufanikiwa kuliko wasanii wengine

room

Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
61
Reaction score
102
Unadhani kwanini pamoja na kuwa kinywaji na brand maarufu duniani, Coca-Cola inaendelea kumwaga fedha nyingi kwaajili ya matangazo?

Kampuni hiyo hutumia zaidi ya dola bilioni 3 duniani kote kwaajili ya matangazo kila mwaka. Kwanini sasa wanahitaji fedha nyingi kiasi hicho kujitangaza wakati kila mmoja katika dunia hii anaijua Coca-Cola?

Ni hivi – matangazo hayakukumbushi uende kununua soda pale unapokuwa na kiu – lahashaa! Kazi yake ni kuhakikisha jina lake linakaa zaidi kichwani kwako, na ni jina ndilo unalolinunua. Kwahiyo watahakikisha wanajitangaza ili ile nembo ya Coca-Cola ikae daima kichwani kwako.

Mfano huu unahusiana vipi na Diamond? Kwa ukubwa wote alionao, mashabiki wote hao alionao, kwanini bado anaendelea kuzipigia promo ngoma zake kiasi hicho? Kwa hatua aliyofikia, anaweza kuachia wimbo na kutoa link mara moja tu na mashabiki wenyewe wakashughulika nao, lakini hafanyi hivyo. Akitoa wimbo ataupigia promo kwa kuweka post kibao kila siku.

Promo kwa msanii ni kama tu ilivyo matangazo kwa makampuni kama Coca-Cola. Kwahiyo Diamond anafanya kile kile makampuni makubwa yanafanya – kuhakikisha anaijenga brand yake kwenye mawazo yako kiasi ambacho huwezi kumsahau wala kumkwepa.

Hii ndio maana hata video zake zimekuwa zikipata views nyingi kwa muda mfupi na kuwazidi wasanii wengi wakubwa wa Afrika ambao huwa hawasumbuki kupiga promo kubwa kwa nyimbo zao.

Hivyo, ni sahihi kumuita Diamond supastaa anayeutreat muziki wake kama underground. Licha ya ukubwa alionao, staa huyu bado anauchukulia muziki wake kwa mtazamo ule ule msanii mpya huwa anakuwa nao – kwamba hakuna anayenijua hivyo nahitaji kuisukuma zaidi kazi yangu.

Mfano, tangu video yake ya Salome imetoka, ameshapost kwenye Instagram (followers milioni 2.8) picha au video zinazoipromote ngoma hiyo zifikazo 39, katika kipindi cha siku 7 tu! Katika kipindi cha siku 7, ameshapost Facebook (likes milioni 1.6) kupromote wimbo huo, mara 28. Anafanya hivyo Snapchat, anafanya hivyo Twitter pia – kila siku.

Video ya P-Square, Bank Alert imetoka Septemba 18 na sasa hivi na views milioni 1.58, nyuma ya Salome yenye views milioni 2.3 na huku ilitoka siku 2 mbele. Tangu muda huo, Peter Okoye mwenye followers milioni 1.8 Instagram, ameweka post za kuupromote wimbo huo 6 tu!

Simaanishi kuwa kila msanii Afrika anapaswa kufanya kama anavyofanya Diamond, bali nakuonesha jinsi gani anavyochukulia kazi yake kwa mtazamo sawa kama ambavyo kampuni kama Coca-Cola inafanya. Kwamba licha ya ukubwa walionao, wanafanya kazi kwa mtazamo kuwa hakuna anayewafahamu. Ni ngumu kuchuja kwa msanii au kampuni yenye mentality hii.

Bongo5.com
 
Asante sana kaka,ngoja tuwasubiri waje wasanii wenye sauti nzuri kuliko Hadija koppa,pia wenye kujua kupiga live kuliko Ottu huku wakiwa hawamiliki hata gita,huku yule wanayemuita hajui kupiga live anamiliki vyombo vyote a.k.a ana bendi iliyokamilika.
 
Unajua mimi ni mshabiki mkubwa wa ali kiba,
Ila kiukwel uhalisia upo hivii
Diamond kwa sasa yupo juu ya ali kiba , kiba kwel ana sauti ila kuna vitu vingi sana diamond kamzid kiba,
 
Umesahau na swala la kiki anavyolitumia kujipromote ili kila siku azungumziwe yeye tu sasa wasio na akili wanajua jamaa kweli anafanyaga ivyo vitu kumbe ni kiki tu.
 
Wcb bwana hawaishiwi vituko
 
Anajua kupiga live zaidi ya Ottu Jazz Band...
Lakini hana hata chombo kimoja cha muziki..!
Nafikiri Ali Kiba atakua ameiona comment yako...
Au mashabiki zake wa kufa na kupona watampa taarifa..!!!
 
Kukosekana kwa hayo yote ndiko kumemfanya msanii mwenye nyimbo tamu mno Belle 9 aonekane wa kawaida wakati ni mkali kupita maelezo,hebu fikiria wimbo kama burger movie selfie ungepata promo za kutosha ingekuwaje!!!!
 
Jay z mwenyewe pamoja na ukubwa wa jina lake akitoa wimbo lazima aufanyie promo la maana... Who are you by the way?(In Idd Amin Dada's voice) eti utoe tu wimbo utegemee mashabiki wakufanyie promo....hiyo kitu haipo....
 

Nonsense.
 
kufananisha nyimbo ya Diamond na P ,SQUARE ni matusi,nyimbo salome kwanza ni remix wote tunajua nani alitoa salome.
Haya kuna makosa yale yale yanajirudia,kuiga mavazi ya kipopo,nyimbo nzima na wasanii wote wamevaa mabazee ya kipopo na vibakora,ance vile vile wamecopy kwenye nyimbo za wapopo km we ni mwangaliaji.
tofauti iliyopo ni kwamba nyimbo salome itasikilizwa haraka na view wengi kwa muda mfupi badae 0,bank alert ipo pale na itakuwepo utaikuta ina heat hata miaka 3 mbele.
swaga pia msanii wenu anaiga tena zaidi kwa hao p,square.
Sina wivu na ni mzalendo haswa,ila diamond ajaribu kutafuta brand yake ya muziki,miziki yake ya zama
 
congrats to ya bro,umechambua vizuri.mond anajua kumarket muziki wake.
 
Kufanya analysis ya mambo kama haya kwa Tanzania ni kitu kigumu bali ukiona hata magazeti yasiyo ya udaku kama haya yameanza kuhoji basi ujue kuna kitu. Kuna wengine wana mapesa mengi sana na wako kwenye mchakato wa kuyatakatisha hivyo huwezi kujua nani ni nani, tuachie tu muda utatujuza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…