Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Jambo hili huwa lenye kuacha Watu wengi sana mdomo wazi kwa kile huitwa wanawake hawajui wanataka nini.
mada ya leo kwanini mwanaume mwema sana, muaminifu,hana michepuko, anajali sana,ni mnyenyekevu sana,ni mstaarabu sana,hapendi ugomvi wala migogoro,hanywi pombe, havuti bangi wala sigara huwa anaachwa ghafla baada ya kujitoa mhanga kwa kumsaidia, kumfariji, kumliwaza, kumtetea Mwanamke mwenye huzuni, simanzi, majonzi,upweke uliopitiliza, mwanamke mwenye kupitia kipindi kigumu sana kifedha, mwanamke ambaye ametelekezwa na ujauzito au watoto?
Mada ya leo kutoka ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI inakwenda kuangalia jambo hilo kwa muhtasari.
kuna sababu mbili hapa.
1.SIFA ZENYE KUFANANA HUWA ZENYE KUSUKUMANA,NA SIFA ZENYE KUTOFAUTIANA HUWA ZENYE KUVUTANA (POLARITY)
Mahusiano ya kimapenzi hujengwa kwa POLARITY,ni tofauti na mahusiano ya urafiki ambayo hujengwa kwa kuzingatia sifa zenye kufanana iwe sifa mbaya au nzuri.Yaani urafiki unajengwa kwa kanuni ya ndege wenye rangi moja huruka pamoja.
Mahusiano ya kimapenzi hujengwa kwa POLARITY yaani tofauti ya sifa.
Kila mtu anakuwa na sifa za kiume (Masculine) na sifa za kike (feminine)
japokuwa sifa za kiume (Masculine) huonekana zaidi kwa wanaume, vilevile sifa za kike (feminine)huonekana zaidi kwa wanawake
SIFA ZA KIKE (FEMININE BEHAVIOR)
-Upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa,kuomba msamaha,kulea (nurturing),ulaini (softness), kubembeleza, kujishusha lakini baada ya kuumizwa hugeuka king'ang'anizi (needy),kutaka ukaribu uliopitiliza (clinging),kutishia kujiua,au kujitoa mhanga kwa kuhatarisha uhai.
SIFA ZA KIUME (MASCULINE BEHAVIOR)
-Kujoshughulisha,kuwa na msukumo wa nje, kuthubutu, kueleza mahitaji bila woga, kujiamini, kujiongoza/isiyohitaji kuongozwa au kupewa maagizo,yenye kutaka uhuru,yenye kuhoji kwa mantiki (logic)
hulka ya kiume (Masculine behavior) ikijeruhiwa kuonyesha tabia kama ubabe, ukali kupitiliza, misimamo mikali, kulazimisha mambo,kutaka kutawala watu kimabavu,kiburi, ujuaji,ubishi,utemi.
Hivyo basi ikiwa wewe upo na sifa za kiume (Masculine) mwenza wako anakuwa na sifa za kike (feminine) bila kujali jinsia yake,na ikiwa wewe upo na hulka ya kike ( feminine) mwenza wako anakuwa na hulka ya kiume (Masculine) bila kujali jinsia yake.
Kwa maana kwamba
-Ukiwa mpole kupitiliza unapata mwenza mkali kupitiliza
-Ukiwa mvumilivu kupitiliza unapata mwenza asiekuwa na uvumilivu
-Ukiwa unajali sana unapata mwenza ambaye anakupuuza sana
-Ukiwa unapenda kumfariji sana, kumliwaza, kumtetea mwenza wako unapata mwenza ambaye ni mzigo kwako kwa maana anakuwa na huzuni sana,upweke uliopitiliza,hasira kupitiliza,majonzi mazito kila siku.
Ukiwa mwanaume mkali kupitiliza ukipata Mwenza mkali kupitiliza utaibuka ugomvi kwa kuanza kufokeana, kutoana dosari za muonekano, kutukanana, kujibizana, kugombana,kupeana kashfa na tuhuma za usaliti, kutishiana kuachana
na ikitokea wewe ni mwanaume mpole kupitiliza ukipata Mwenza mpole kupitiliza mtajikuta mnakuwa marafiki wa karibu lakini panakuwa hakuna mahusiano ya kimapenzi baina yenu.
upole sifa ya kike,ukali sifa ya kiume.
-Kulinda sifa ya kiume,kulindwa sifa ya kike.
-Kuhudumia sifa ya kiume ,kuhudumiwa ni sifa ya kike.
Hivyo basi pale ambapo mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu kupitiliza, king'ang'anizi, mstaarabu sana,anajali sana,anaomba msamaha haraka,anasamehe haraka,hapendi ugomvi wala migogoro,anajisshusha sana inakuwa ni sifa za mwanamke sio sifa za mwanaume kwa mantiki hiyo Mwanamke akija kwa mwanaume wa aina hiyo anakuja kama rafiki tu sio mwenza ,au anaweza kuja pale ambapo Mwanamke ametelekezwa na ujauzito au watoto,pale ambapo Mwanamke amefukuzwa na mwenza wake kisha hana pa kwenda.
endapo mwanaume mpole kupitiliza , mvumilivu sana, mnyenyekevu kupitiliza, king'ang'anizi, mstaarabu sana atafanya kazi ya kumfariji, kumliwaza, kumtetea,kumpa ushauri, kumbembeleza,kumpa fedha nyingi sana kwa ajili ya kuhudumia mtoto au ujauzito, kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama, kumjengea,kusaidia ndugu wa Mwanamke.
wakati huohuo mwanaume mstaarabu sana akiwa na matarajio kwamba baada ya Mwanamke huyo kujifungua,au kusoma mpaka chuo kikuu,au kufanikiwa kiuchumi waje kujenga familia imara inakuwa kinyume chake.
baada ya Mwanamke kusimama vizuri kiuchumi,baada ya kuanza kupendeza,kuwa mwenye furaha,baada ya kumsahau ex wake zile hisia za kumpenda mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu kupitiliza,, king'ang'anizi huanza kuondoka ghafla.
sababu ni kwamba Mwanamke akiwa na furaha,amani na utulivu anapoteza hisia za mapenzi kwa mwanaume mstaarabu sana badala yake anakuwa anahitaji mwanaume mkali ili kubalance yaani (Upole+ukali)
chenye kufanya mwanamke kumchoka mwanaume mstaarabu ni kwamba huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu ni sifa za mwanamke sio mwanaume hivyo kwa sababu anakuwa anahisi wanaishi wanawake wawili ndani ya nyumba ndio maana huanza kuonyesha dharau waziwazi atamsaliti ghafla,atajenga mahusiano na wanaume wasiokuwa na malengo naye au anaweza kurudiana na ex wake ambaye hana malengo naye kwa sababu mwanamke amekuwa na amani, furaha na utulivu sasa anahitaji mwanaume Rijali ili kubalance.
mwanaume mstaarabu sana analeta hisia urafiki yaani urafiki wa Mwanamke na Mwanamke badala ya hisia za mapenzi zenye kuhusisha mwanamke na mwanaume.
Hisia za mapenzi kwa Mwanamke hazitokei kwa mwanaume kuwa mstaarabu sana bali kwa kuleta hekaheka hivyo atakwenda kwenye hekaheka huko kwa mwanaume ambaye ni player boys/ bad boy ambao wanampa ujauzito na kumtelekeza kisha anarudi kwa mwanaume mstaarabu sana kwa ajili ya kupata faraja na fedha kwa ajili ya kumhudumia mtoto au ujauzito ambao ametelekezwa nao.
kwa kurahisisha ni kwamba mwanaume mstaarabu sana anafaa kwa ajili ya kumfariji, kumliwaza, kumtetea Mwanamke ambaye ametelekezwa na ujauzito au watoto lakini sio kuishi na Mwanamke mwenye hulka ya kike kama huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu kwa sababu sifa hizo zipo kwa Mwanamke haiwezekani Mwanamke kuvutiwa kimapenzi na Mwanamke mwenzake.