Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,405
- 13,411
Jana usiku mida ya saa tatu usiku natoka kwenye mizunguko yangu ya siku kwenye daladala pembeni yangu alikua amekaa kijana rika moja tu na mimi. Mkononi kashikilia smart phone yake anachati macho hayana pazia, ilikua kila baada ya sekunde kadhaa messages zinaingia kuanzia texts za kawaida hadi WhatsApp. Messages kutoka kwa wadada na wakaka pia zikiwa na viemoji mbali.
Nikaanza kujitafakari na mimi text zangu za mwisho ilikua zile za kutakiana heri ya mwaka mpya tena zina blue ticks na response rate ni chini ya 30% text za kawaida ni kutoka Tigo kukujulisha promotion zao. Nimetafakari jibu nikapata network ya watu wangu wapo busy kama mimi au ni introvert character ndio chanzo.