Sababu ni nini kufa kwa matamasha makubwa ya Wasanii kama Fiesta?

Sababu ni nini kufa kwa matamasha makubwa ya Wasanii kama Fiesta?

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Matamasha makubwa ya wasanii tuliyokuwa tunayaona miaka ya nyuma kama Fiesta na mengine ya Vituo vya Redio naona yanazidi kupoteza mvuto, shida nini wadau?

Matamasha haya mengi imekuwa kiingilio ni bure, wakati miaka kumi iliyopita matamasha mengi miezi hii yalikuwa na viingilio tena vikubwa zaidi ya elfu 10 kwa mtu mmoja, na hali iliyopo sasa ni kwamba vijana waliyokuwepo sasa hawapendi burudani ama ni dalili za vyuma kukaza?
 
Msanii anaimba imba playback alaf mda. Wote anawaambia mnyanyue mikono juu , mara peleka kushoto , kulia , alaf anawaonyeshea mik nyie ndo muimbe , cha kushangaza na wao wanataka walipwe pesa ndefu kama wasanii wa Marekani ..... Kwa style hyo lazima matamasha yafe tuu
 
Nothing lasts forever. Taste inabadilika mkuu, watu wengi ambao miaka 10 nyuma walikuwa Konyagi die hard, sasa wamehamia K VANT.

Wale waliokuwa wanazi wa Double Kick sasa ndio wamehamia kwenye Smart Gin.

Tuliokuwa tunajaza matamasha ya Fiesta sasa tumeokoka, tuna upako, utatukuta nyumbani mwa Bwana.
 
Utandawazi labda.
  • Zamani ilikuwa tunanunua CD, leo sio rahisi.
  • Kumwona msanii ilikuwa ngumu, now simu zimerahisisha
  • zamani tulikuwa tunapakua nyimbo hadi kwa 500 mfano mc.wen.su lakini sasa tunarushiana kwa bluetoth tu
 
Msanii anaimba imba playback alaf mda. Wote anawaambia mnyanyue mikono juu , mara peleka kushoto , kulia , alaf anawaonyeshea mik nyie ndo muimbe , cha kushangaza na wao wanataka walipwe pesa ndefu kama wasanii wa Marekani ..... Kwa style hyo lazima matamasha yafe tuu
Hili nalo inaweza kuwa sababu Wenzetu wanaigeria walishafanya mabadiliko kitambo walishaachana na playback mfano burnaboy nazipenda show zake anatumia vyombo vyote kuimba Hadi ngoma za asili jamaa anapanda
 
Last weekend niliingia night club moja ambayo ilikua ikiniburudisha sanaa enzi hizo nikasema ngoja nikumbukie leo.
Daah nikakuta eti mziki unapigwa na kuna jamaa pembeni na dj anapiga drums kupandia ule mziki.
nikajiuliza nini hiki?
makelele tena sio mziki ule, nikahisi labda kwakua nimeshaanza kuzeeka, nikatoka zangu nikarudi home kulala.
 
Ruge kafariki na matamasha yake.
 
Ni ngumu kusikiliza mziki bar, labda uende grocery za ndichi utajichagulia hata wimbo.

Huko bar kubwa kubwa biashara kubwa ni nyapu, wale sijui ndo mamc wanaharibu sana burudani ya mziki bar. Anasimamisha mziki anaongea ongea tu.
Hata kucheza huwezi maana mda mwingi anaongea yeye, kama wimbo utachezwa dakika 1 basi yeye ataongea ongea sekunde 30 na wimbo utaplay kwa sekunde zilizobaki. Hapo bado dj hajaweka manjonjo yake na jingle zake.
 
Back
Top Bottom