MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 716
- 1,143
Pamoja na mengi sana yanayoendelea kwenye kampeni lakini nina sababu tatu tu zitakazonifanya niwapigie kura wagombea wote wa CCM.
Kwanza ni kitendo cha kuufikisha umeme kijijini kwetu kwa mara ya kwanza.
Miaka yote nilikuwa sina wazo la siku moja umeme kuwaka kijijini kwetu kwani hata makao makuu ya wilaya kipindi hicho Kasulu hapakuwa na umeme.
Hata makao makuu ya mkoa Kigoma mjini walikuwa wakipata umeme mara mbili tu kwa wiki. Hivyo umeme kufika kijijini kwetu imesababisha niwapigie kura CCM japo ni wajibu wao kuleta umeme.
Pili, ni kuleta na kusambaza maji ya bomba kijijini kwetu. Tukekuwa tukochota maji mitoni toka udogo wetu japo tumezungukwa na mito mingi lakini ilikuwa ni adha kubwa sana. Leo mama amachotea maji uani kwake lazima niipigie kura CCM na wagombea wake japo ilikuwa wajibu wao kutuletea maji.
La tatu na la mwisho, ni kutuletea huduma za mitandao ya simu. Zamani kuna mlima Kabhuye ukifika tu pale unakaribishwa na meseji ya Vodacom wishes you good journey and stay in Burundi wakati bado upo ndani ya Tanzania.
Kila muda unaongea na wazazi hata kama upo Horohoro Tanga. Ni kwa sababu hizo nitampigia kura Philip Isdory Mpango kuwa mbunge wangu na John Pombe Magufuli kuwa rais wangu.