Sababu ya Che Guevara kutua nchini Tanzania kwa siri

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mwanamapinduzi wa Argentina na shujaa wa mapinduzi ya Cuba, Ernesto che Guevara, alitumia miezi minne nchini Tanzania kati ya mwaka 1965 na 1966.

Aliingia kwenye ardhi ya Tanzania karibu mara tatu, kwanza kwa kuonekana na mara mbili kwa siri ,kati ya Februari na Novemba 1965.

Che alivutiwa na Tanzania sababu ilikuwa ni makao makuu ya harakati za mapinduzi kutoka kusini mwa afrika, Ilikuwa ni moja ya kitovu cha fikra za mapinduzi kwenye bara la afrika .baada ya miezi mitatu ya kusafiri kwenye nchi za Afrika tofauti kama sita, akihimiza mapinduzi, ilikuwa ni Tanzania iliyokuwa tayari kumsapoti che Guevara kwenye mipango yake na kuanzisha mapinduzi yake yajayo, Tanzania ilikuwa ni eneo la kwanza kwa operesheni za Cuba kukatiza ziwa Tanganyika na kutumia miezi saba kupigana nchini Kongo.

Che alitinga Dar es salaam Alhamisi, Februari 11, 1965 akitokea nchini China, akiwa na mkakati mmoja, kupata umoja na msaada kwa wanaharakati wa mapinduzi kuunda jeshi la umoja kupigana dhidi ya ubepari na majeshi ya ukoloni mamboleo huko Kongo.

Che alikuja Tanzania akiwa na mpango mkakati ,alitaka mapinduzi, kama palikuwa na eneo kubwa Afrika lililokuwa na wanamapinduzi wengi kutoka nchi tofauti karibu na uwanja wa vita mwaka 1965 basi lilikuwa ni Tanzania.

Vita vilipigwa nchi za jirani huko Msumbiji dhidi ya wareno. Wanamapinduzi toka Afrika kusini, Zimbabwe na Namibia walimiminika nchini Tanzania, Tanzania ilikuwa ni sehemu moja Afrika ambayo Che alikuwa na matumaini Kwa mipango yake kuwafundisha wapiganaji na kuimarisha kambi ya nyuma kwaajili ya vita vya kimapinduzi.

Che Guevara alitumia siku ya kwanza Dar es salaam na kuelekea Zanzibar kuhudhuria sherehe za Siku ya mapinduzi ya Zanzibar ,kwenye wikiendi ya Februari 13,1965, kumbukumbu ya sherehe iliahirishwa toka januari 12, hadi Februari 12,1965, sababu ya mfungo wa Ramadhani .kuhudhuria sherehe za kumbukumbu za mapinduzi ,kwa che Guevara ilikuwa ni alama ya kuanzia, kwa ziara ya Tanzania, Cuba ilitoa mafunzo ya kijeshi kwa marafiki waliokuja Zanzibar.

Hali ya usalama nchini Tanzania ilikuwa kubwa mwishoni mwa mwaka 1964, na kuanzia mwaka 1965 ugomvi wa kibalozi kati ya Marekani na Tanzania uliibuka ,Novemba mwaka 1964 baada ya kugundulika kwa taarifa ya mpango wa Marekani kuisaidia Ureno kuipiga serikali ya Tanzania.

Ugomvi ulikuja januari 11,1965 wakati kikosi cha Usalama Tanzania kunasa maongezi kupitia simu kati ya Mabalozi wawili wa marekani ,Bob Gordon na Frank Carlucci ,waliowasikia wakiongea kwa lugha ya siri kuhusu mpango dhidi ya serikali ya Zanzibar . balozi zote mbili za Marekani zilitimuliwa toka nchini Tanzania januari 1965.

Ulikuwa ni ugomvi kulingana na mmoja wa balozi wa marekani ,Don Patterson, ulimsababishia Nyerere kuangusha machozi wakati wa majadiliano na William Leonhart ,balozi wa marekani nchini Tanzania wakati ule.

Che alikuwa Tanzania wakati wa kipindi hiki kigumu kwa utawala wa serikali ya Tanzania. Gazeti la " New York Times" lilibeba kichwa cha habari juu ya Marekani na ugomvi wa kibalozi wa Tanzania. Februari 15,1965 uliandikwa kwamba ,serikali ya Tanzania imemkaribisha che Guevara katikati ya uhasama huu, Nyuma huko Zanzibar, Ali sultan Issa ,waziri aliyeteuliwa mpya wa elimu ,alipewa kazi ya kumkaribisha Che Guevara, Ali alikuwa ni mjamaa aliyesoma Uingereza, alitumia muda mwingi nchini Cuba na China.

Kiukweli Ali alihakikisha maandalizi yalifanywa ili Che Guevara aishi kwenye nyumba ile.

Che na Ali walitumia masaa mawili kujadili mtazamo wa Che juu ya mabara matatu, Che Guevara alitaka kujenga jeshi la mapinduzi kutoka mabara matatu tofauti, Afrika, Amerika kusini, na Asia. Kupambana dhidi ya ubeberu ,wawili hawa pia walijadili uamsho kwa mapinduzi ya waafrika na fikra za waasi wa Kongo ,wapiganaji wa Uhuru wa msumbiji na kusini mwa afrika.
Che alitumia muda wake pia na Salim Ahmed Salim na familia yake huko Zanzibar.

Salim alikuwa balozi wa Tanzania Nchini misri, toka 1964 hadi 1965. Salim alimkaribisha Che Guevara kwenye nyumba yake kwa chakula cha mchana.

Mke wa Salim, Amne Ahmed ,aliandaa chakula kwa mwanamapinduzi huyu maarufu. Che na Salim walitumia masaa kadhaa, kujadili mapinduzi ya Cuba na nguvu ya harakati za ukombozi wa bara la afrika, Che alirudi Dar es salaam baada ya kutumia siku kadhaa huko Zanzibar.

Mipangilio iliandaliwa kwaajili ya mkutano kati ya Che Guevara na wawakilishi wa makundi ya vikosi vya mapinduzi takribani 50 kutoka nchi 10.

Balozi mwafrika wa Cuba Nchini Tanzania Pablo Rivalta na Juan Carretero, mkuu wa sehemu ya Latin ya Marekani wa idara ya usalama wa taifa nchini Cuba ,alichukua nafasi kuongea, mkutano ulifanyika ubalozi wa Cuba ,Upanga ,Dar es salaam.

Kwenye mkutano huu ndipo Che Guevara alipotoa wazo lake la kuunda jeshi lenye askari kutoka nchi za Afrika mbalimbali na kupewa mafunzo nchini Kongo. Che Guevara aliupa mpango huu jina la "Common Front".

Hiki kilikuwa ni kitendawili kigumu kwa makundi ya mapinduzi kukikubali. Wapiganaji wa Uhuru hawa walihitaji kampeni kwenye nchi zao zaidi, Che akakumbana na kikwazo hapo, baadaye akafanya maamuzi haraka sana, na kusema itakuwa vema akikutana na makundi haya moja moja , mikutano tofauti ikapangwa baadae kwa baadhi ya makundi.

Viongozi wa FRELIMO kutoka msumbiji walikutana na Che tofauti pekeyao, Orodha ya wahudhuriaji wakiwemo, Marceline dos Santos, Samora Machel na Eduardo Mondlane ,. Kwa mara nyingine tena, Che alichukua muda kuitaka FRELIMO kupeleka askari wakapate mafunzo na kupigana nchini Kongo, viongozi wa FRELIMO hawakufurahishwa na mpango huu ,nini kilifuata sasa? , ni majadiliano marefu kati ya Che na viongozi wa FRELIMO ,kulingana na Marcelinos dos Santos ,walimweleza Che kuhusu baadhi ya maelezo juu ya vita huko Msumbiji na Che aliwahoji juu ya madai yao hayo.

Majadiliano yakawa makali sana kati ya pande zote mbili hizi, Mondlane ,Rais wa Frelimo akawa na mashaka,mkutano ukaahirishwa ,lakini wakapata baadhi ya picha.

Mkutano uliozaa matunda ni wa kati yake na waasi wa Kongo walioishi Dar es salaam , Tanzania. Laurent Kabila na Godefrei Tchamlesso, na baadae Gaston Soumialot.

Che alifanya kama mikutano mitatu na waasi wa Kongo nchini Tanzania. Februari 1965.

Alipendezwa sana na kabila , Che Guevara aliandika kwenye diary yake kwamba Kabila " Amenifurahisha sana mimi" aliwakilisha mpango mzuri na kuitambua Marekani kama adui mkubwa ,hili ndilo hasa lililomfurahisha Che Guevara ,waasi wa Kongo waliukubali vizuri mpango wa Che, mpango wa mwanzo ulikuwa kutuma wacuba 30 kuwafundisha mafunzo waasi, Che hakuwaambia viongozi wa waasi wa Kongo wala viongozi wa Tanzania kwamba yeye binafsi ataongoza kikosi cha Wacuba. Mpango wa Cuba usingeliweza kufanikiwa bila ya msaada na kubarikiwa na serikali ya Tanzania ,Rivalta akaitisha mkutano kati ya Che na Rais Nyerere Ikulu.

Che alipata fursa ya kuongea na Nyerere ,waziri wa mambo ya ndani ,Abdulraman Babu na makamu wa Rais Rashidi Kawawa ,Rivalta alikuwepo kwenye mkutano pia ,mkutano ulikuwa na mafanikio Che Guevara alieleza kwa uongozi wa Tanzania kuwa Cuba itasaidia harakati za Kongo za kujikomboa ,Cuba itasaidia waasi wa Kongo kwa kuwapa vifaa na mafunzo.

Serikali ya Tanzania iliwaahidi wakyuba kwamba wakufunzi na vifaa vya kijeshi vitapewa usalama wa kupita kwenda Kongo.

Che alibaki Tanzania toka Februari 11, hadi 18 ,1965, Aliandaa mkutano wa waandishi wa habari Dar es salaam Februari 18, kabla ya kuondoka.

Che aliwaambia waandishi wa habari kwamba ziara yake Afrika imefanikiwa kwenye uwezekano wake wa " Common Front" dhidi ya ubeberu na ukoloni ,aliwaambia waandishi wa habari kwamba " common front" itajumuisha nchi za Latin America , nchi za kiafrika za kijamaa ,nchi za Asia, Wamerikani walikuwa wakifuatilia kwa ukaribu ujio wake Dar es salaam

Gazeti la" New York Times" likaibuka na stori dhidi ya mkutano wa waandishi wa habari na Che Guevara jijini Dar es salaam Februari 19.

Che akaondoka Tanzania hadi Misri na pia Algeria ,hakurudi Cuba mpaka machi 14, 1965, Safari ya Tanzania ilikuwa na mafanikio ,aliwashawishi waasi wa Kongo kukubali msaada toka Cuba ,Che na Rivalta wakapata kibali cha serikali ya Tanzania kuwaruhusu kusafirisha wakufunzi wa Cuba na vifaa vya kijeshi Kongo. Ndoto ya Che Guevara ya vita dhidi ya ubepari ilizinduliwa kwenye pwani ya ziwa Tanganyika na kuwa ya ukweli. Maandalizi yalipangwa kwa askari wa Cuba kwenda kupigana nchini Kongo, Askari wa Cuba walipaswa kusafiri hadi Tanzania kwanza halafu waingie kwa siri Kongo Che Guevara na watu wake waliwasili Dar es salaam Aprili 19,1965. Balozi Rivalta alipokea simu toka Cuba ikimtaka kwenda kuwachukua Wacuba watatu uwanja wa ndege Dar es salaam, hakuambiwa watu hao ni kina nani ,hakutambua ni sehemu ya watu wanaokwenda kupigana Kongo.

Che alipita kwenye uhamiaji wa Tanzania akitumia jina la Ramon Benetiz ,jina halikutoa mashaka yoyote juu ya utambulisho wa kweli wa mtu aliyebeba paspoti ya kibalozi. Alinyoa ndevu zake ,akivaa miwani ,na alivaa vifaa maalum kubadilisha muonekano wake.

Rivalta aliyemuelewa Che vizuri hakumtambua kabisa, hadi pale kuna muda Che alipomwambia Rivalta " usiwe mjinga na chukulia kawaida " hapo ndipo Rivalta alipomgundua Che, rafiki yake wa zamani kwenye vita vya Cuba vya mapinduzi.

Rivalta akamchukua Che, Askari mwafrika wa Cuba Victor Dreke na Jose Maria ,Martinez Tamayo, kwenye Hotel jijini.

Balozi wa Cuba Rogello Oliva aliwapakia kwenye gari na kuwapeleka kwenye nyumba takribani kilometa tano nje ya jiji la Dar es salaam.

Ubalozi wa Cuba uliandaa makazi haya kwaajili ya operesheni hiyo, nyumba ilikuwa na shamba dogo na ilikuwa nje ya mji hapo Ilikuwa 1965,Che na watu wake hawakubakia kwenye nyumba ile kwa muda mrefu, kulingana na Dreke, Rivalta akaenda kule shambani Usiku mmoja ,na kuwachukua baadhi ya wacuba kwenye ziara jijini Dar es salaam .

Hakuna uhakika kama Che alikuwemo kwenye hiyo safari fupi ya jijini Dar es salaam sababu tayari alishayaona maeneo mengi ya jiji mara alipotembelea Dar es salaam miezi miwili iliyopita, Che akawapa watu wake majina mapya kulingana na namba za kiswahili ,Alimpatia Dreke jina ' Moja' ,Tamayo akaitwa 'mbili' na yeye akajiita ' tatu' makazi ya Dar es salaam yalikuwa mafupi , Che alitamani azame Kongo kuanza kazi, kukaa muda mrefu Dar es salaam ndio nafasi kubwa kwa maadui kugundua mpango wao, serikali ya Tanzania haikutaarifiwa uwepo wa Che pale Dar es salaam ,haijulikani serikali ya Tanzania iliarifiwa uwepo wa che lini,

Che alitumia Siku moja jijini Dar es salaam ,aliondoka tar 20 April na kikosi cha watu 14, Tchamlesso na polisi wa Tanzania kadhaa waliwasindikiza wacuba ,jeshi la polisi Tanzania liliungana nao kuhakikisha hawapati tatizo lolote njiani ,wanaume hao walisafiri kwa makundi katika magari matatu ,Land Rover moja ,Mercedes Benz tatu, na Jeep mbili, magari yalibeba baadhi ya silaha za kutumia Kongo, Wacuba akiwemo Che Guevara waliendesha zaidi ya kilomita 1700 ,toka Dar es salaam hadi kigoma .

Ilikuwa safari ndefu kwenye barabara ya tope iliyochukua siku mbili ,kikosi hicho kilichelewa sehemu moja sababu walipaswa kusubiri Kongo,che pale alipokuwa haendeshi gari alisoma Ramani kuhusu Kongo.

Kundi lile liliwasili kigoma Usiku Aprili 22,1965, Kigoma lilikuwa ni jiji lenye watu takribani 70,000 wakati ule, Kongo ilikuwa takribani km 50, ukivuka ziwa Tanganyika ,moja ya Ziwa lenye kina kirefu duniani, kigoma ulikuwa mji wenye pilikapilika nyingi ,wakimbizi walikuwa wakitoroka Kongo na askari waasi walikuwa wakiingia na kutoka kwa makundi ,Wacuba Wakajigawa makundi mawili ,Che ,Dreke, Tamayo, Zerquera ,na kundi la wacuba wengine walikwenda kwenye makazi ya Sinfua, Mkuu wa mkoa wa Kigoma,.
Che na wenzake walitumia Usiku mmoja tu kigoma ,Mkuu wa Mkoa wa kigoma ,Sinfua ,alimuonya Che, wakati wa majadiliano yao kwamba waasi wa Kongo walikuwa hawana adabu ,Che aliamini baadae kwamba Sinfua alikuwa yupo sahihi ,Wacuba wakapanda boti kabla ya Usiku wa manane Aprili 23,1965, kwenda Kongo .

Che na watu wake wakatumia miezi 7 wakipigana Kongo, Tanzania ilikuwa muhimu sana kwa operesheni ya Cuba huko Kongo, Che hakukaa miezi hiyo saba Kongo bila ya ushirikiano na serikali ya Tanzania, ,kitovu cha operesheni ya Kongo kilikuwa ubalozi wa Cuba jijini Dar es salaam vifaa vyote vilipitia Tanzania kisha kwenda Kongo.

Uwepo wa Che Guevara nchini Tanzania ulikuwa haufahamiki kabisa ,watu wachache sana walielewa uwepo wake katika Tanzania na Kongo pia.

Mataifa ya magharibi hayakuelewa pia uwepo wa Che, Larry Delvin ,chifu wa kituo cha CIA Kongo, alidai kwamba aliripoti uwepo wa Che oktoba 1965, lakini walimpuuza, Taarifa za hivi punde zilidai Wamarekani walikuwa na meli Bahari ya Hindi ,ukingoni mwa Afrika mashariki wakifuatilia mawasiliano kati ya ubalozi wa Cuba, Dar es salaam na Askari wa Cuba Kongo, ukamataji wa mawasiliano hayo haukumaanisha kwamba Wamarekani walielewa Che alikuwa miongoni mwa askari ,hata kama walikuwa na wasiwasi.

Kuna taarifa moja ilionyesha uwezekano kwamba kuna mtu alielewa wapi alipo Che kipindi kile, umbea uliibukia Cairo ,Misri na Dar es salaam oktoba 1965 kwamba Che na Soumialot waliuawa huko Kongo.

Taarifa hii ikamlazimisha Soumialot kuitisha mkutano wa waandishi wa habari ,Dar es salaam ,oktoba 17,1965, Gazeti la "The Times" la London likaripoti mkutano wa Soumialot na waandishi wa habari siku ileile, Oktoba 17,1965, Soumialot aliwaeleza waandishi kuwa yupo fiti na hai, alikataa madai kwamba Che yupo Kongo na kwamba aliuawa kwenye "Ambush" hali ikawa mbaya kwa wakyuba mwishoni mwa Oktoba 1965, kundi la mamluki weupe na askari wa Kongo wakiongozwa na Mobutu sese seko na Muairish mamluki aliyeitwa Mike Hoarse ,walianza kuwazingira wacuba mwezi oktoba ,kuondoa mambo hatarini kiongozi wa Kongo Joseph Kasa- vubu alikwenda kwenye mkutano wa OAU Ghana toka Oktoba 15,hadi 21,1965 na kuahidi kuwaondoa mamluki wageni ,aliwataka wakuu wa OAU watoe tamko vikosi vya kigeni viondoke Kongo, Nyerere akamwita balozi Rivalta na kumtaka Wacuba waondoe vikosi vyao.

Che na watu wake wakavuka ziwa Tanganyika na kuingia kigoma Novemba 21,1965, Oliva na balozi mwingine wa Cuba aliyeitwa Coloman Ferrer ,walikuwa Kigoma kuwakaribisha che na askari wa Cuba kurudi kwenye ardhi ya Tanzania .
Polisi wa Tanzania walikwenda kwenye boti na kuchukua silaha zote, Che akaenda kuoga kubadili nguo na kula chakula.

yeye na watu wake walilala kwenye ukumbi wa chumba cha mapokezi kigoma. Hii ilikuwa ni safari ya tatu na ya mwisho kwa Che kuingia Bongo.

Ulikuwa ni uchungu mkubwa kwa Che ,operesheni Ilikuwa imefeli ,lakini matarajio ya kuendelea na mapambano yalibakia makubwa. Coloman alipokea maelekezo kumchukua Che na watu wake wachache waliochaguliwa kurudi Dar es salaam ,kundi hili likaondoka kwa gari kwenda Dar es salaam .Coloman alielezwa kujulisha ubalozi maeneo walipo, Coloman alielezwa kujulisha ubalozi wa Cuba kuhusu wanavyoendelea Alipiga simu kutoka morogoro kujulisha ubalozi maeneo walipo, Coloman na Che walikwenda kwenye nyumba inayomilikiwa na Mkurugenzi wa Magereza Tanzania ,karibu na airport wakati watakapofika Dar es salaam ,Che na jamaa zake waliishi Usiku ule kwenye nyumba
hiyo, Coloman alikwenda kumwangalia Che siku ya pili yake na kumpelekea baadhi ya vifaa, Che alitumia tena Siku mbili au tatu kwenye nyumba hiyo karibu na Airport, nje ya jiji la Dar es salaam , kwenye chumba chenye vitanda viwili juu ya ubalozi wa Cuba Upanga, nje ya jiji la Dar es salaam , alitumia tena miezi minne kwenye chumba hicho bila hata kutoka nje .

Che alijiweka bize pale Dar es salaam ,alitafakari kuhusu mapungufu ya operesheni Kongo na kujipanga kwa hatua zijazo. Che alikuwa wazi kwa kitu kimoja ,alihitaji kupigana .
Ingawa hakuwa na uhakika wapi ataanzisha kampeni zake zijazo dhidi ya ubeberu ,hakutaka kurudi Cuba, kufeli kwa operesheni Kongo kulimuumiza sana Che ,wacuba walifanya siri kubwa kwa uwepo wa Che nchini Tanzania, watu wachache sana wa ubalozi wa Cuba walielewa uwepo wa Che, kulikuwa na watu watatu tu walioruhusiwa kuingia chumbani mwa Che Guevara ,Rivalta ,Oscar Fernandez mell, Padilla, na Delfin ,opereta wa simu.

Che alitumia muda wake akisoma ,kucheza chess ,na kuandika diary kwa uzoefu alioupata Kongo. Alitumia miezi minne bila kutoka nje kwa watu wengi sio kitu rahisi ,hilo halikuwa shida kwa Che ,Wacuba wachache walikuwa na che kipindi hicho hawakuonyesha shida ya aina yoyote ,Che aliukaribisha mwaka mpya wa 1966 akiwa Dar es salaam akiwa na Rivalta ,Padilla na Fernandez mell, Che alitumia muda wake kucheza chess. Kusoma na kuandika.

Alitumia muda wake kwenye diary ya Kongo ,alimsimulia Ferrer kwa mdomo na Ferrer aliandika sentensi kwa usahihi ,che alirudia na kusahihisha maandishi ya mwishoni.

Kipindi ambacho ni cha muhimu kwa che akiwa Tanzania ni baada ya kutembelewa na mke wake, Aleida March kwa siri, Februari 1966, Aleida na Che walitumia mwezi kwenye chumba chenye vitanda viwili ,kulingana na Aleida huu ulikuwa muda kwa wawili hawa waliotumia ,walitumia Usiku na mchana pamoja kufidia muda waliopoteana ,wawili hawa hawakuwahi kutumia muda mwingi Pamoja tangu waoane mwaka 1959.

Hivyo ilikuwa ni Dar es salaam Che aliweza kutumia muda wake kuwa pamoja na mkewe ,Che akaondoka Dar es salaam kwa siri machi 1966 ,alikwenda Prague ,Cuba na mwishowe Bolivia ambapo aliuawa kwa msaada wa CIA . kama ilivyokuwa ujaji wake wa siri ndivyo ilivyokuwa uondokaji wake kwa siri pia, Alikuja Tanzania kutafuta njia kupigania vita vya mapinduzi , vita dhidi ya ubeberu na ukoloni mamboleo, ,alikuwa na matumaini, alitaka kujenga jeshi ambalo litashinda ubepari huko Kongo ndoto hizo hazikufaulu ,bado che aliacha alama isiyofutika eneo hili la Afrika che aliacha hadithi ya kujitoa kafara na utayari.
 
D

Dunia hii ya leo watu kama akina Che, Mwl Nyerere , Nkwame na wengine kama wao ni ngumu sana kuwapata
 
Back
Top Bottom