Sababu ya Gari nyingi ndogo ni Petrol na nyingi kubwa ni Diesel Engine ..!

Sababu ya Gari nyingi ndogo ni Petrol na nyingi kubwa ni Diesel Engine ..!

KndNo1

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2021
Posts
627
Reaction score
2,049
Sababu kubwa ni uzito wa engine na matumizi ya gari..

1. Kupata nguvu ya kusukuma gari(hp) kwenye engine ya petrol ni rahisi kuliko diesel.. Kwahiyo utakuwa na engine block ndogo kwenye petrol kulinganisha na diesel.. Engine block ndogo itakuwa nyepesi hivyo kupunguza uzito wa gari..kwenye gari ndogo ni uzito ni ishu.. Uzito unaathiri performance ya gari.. Hii pia ni tip ya kupunguza ulaji wa mafuta.. Usiwe na mizigo mingi kwenye gari kama sio lazima.. Ukiangalia race cars huwa wanatoa vitu vingi kupunguza uzito kwenye gari mpaka redio..!

2. Gari ndogo ni saloon cars.. Matumizi yake yanahitaji Horsepower zaidi kuliko Torque.. Petrol engines zipo vizuri kwenye kutoa horsepower wakati Diesel engines zimejikita zaidi kwenye torque..!
Mfano hizi engines mbili za Landcruiser 200(Viete) zina displacement, cc almost sawa
1UR FE (petrol) ina 347 hp na 460 Nm
1VD FT (diesel) ina 268 hp na 650 Nm..!
 
Kwa haraka haraka.. Torque ni uwezo wa gari kufanya kazi..
Horsepower ni uharaka wa gari kuifanya hiyo kazi..!
Kwahiyo gari nyingi za diesel(torque kubwa) zina uwezo wa kufanya kazi kubwa ngumu ila kwa spidi ndogo(horsepower ndogo)..
Wakati petrol sio heavy duty ila zinafanya kazi kwa haraka zaidi ya diesel..!
 
Logically sio rahisi gari kuwa na horsepower nyingi kuliko Torque.. Sababu Torque ndio uwezo/nguvu ya gari.. Horsepower ni uharaka wa kuitumia hiyo nguvu ya gari..!
 
Kwa haraka haraka.. Torque ni uwezo wa gari kufanya kazi..
Horsepower ni uharaka wa gari kuifanya hiyo kazi..!
Kwahiyo gari nyingi za diesel(torque kubwa) zina uwezo wa kufanya kazi kubwa ngumu ila kwa spidi ndogo(horsepower ndogo)..
Wakati petrol sio heavy duty ila zinafanya kazi kwa haraka zaidi ya diesel..!

Torque sio uwezo wa gari kufanya kazi....motor zina torque...hata unavofungua nut una apply torque pale

Torque is just twisting force
 
Hp ni zao la torque times engine speed over 5252

There is no way hp ikawa kubwa zaidi ya torque..over
 
Back
Top Bottom