Sababu ya kujiita Mtoto Wabibi

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
451
Reaction score
294
Kihistoria mimi ni mtoto pekee kwa mama yangu yani wa kwanza na wa mwisho ( kitinda mimba na kifunga mimba). Mama alifariki nikiwa na umri wa miaka 2 na miezi 7 hivi.Lakini mapema baada ya kuacha kunyonya aliniacha kwa mama yake ( bibi) na yeye kuendelea kutafuta maisha kwasababu fulani ambazo ilimbidi afanye hivyo lakini baada ya kama mwaka alirudishwa akiwa amefariki hivyo sikupata kumjua vizuri mama yangu na kubakia kuona picha tu hadi leo hii.

Cha ajabu sasa, toka nipo tumboni, bibi alionesha upendo sana kwa mama yangu tofauti na kawaida yake na hadi nazaliwa chini ya mikono ya baba, bibi alionesha upendo sana japo ilikuwa ni sehemu(mikoa) tofauti na hatimaye nikatokea mimi.Hata baada ya kunipata mimi,bibi alihamishia upendo wake wote kwangu ndipo kuninyang'anya kwa mama na kuishi na mimi hata kabla mama hajafariki.Na kadri siku zilivyosonga ndipo upendo ulipozidi kwangu.

Katika mazingira hayo tulikuwa tunaishi kama wajukuu wake ishirini na tano na zaidi kwani tulikuwa tumejitenga na mji kidogo ambapo ndugu tu ndio wanaishi hapo.lakini ni bibi alionesha dhahiri upendo wake kwangu zaidi kuliko kwa wengine na wao walijua dhahiri kuwa mimi napendwa na bibi.

Udogoni mimi nilikuwa mkorofi sana ya kupigana,utundu na usumbufu ilikuwa ni kawaida yangu lakini havikupunguza upendo wa bibi kwangu na kadri umri unapokwenda alizidisha upendo na alikuwa anapenda kunitania sana kuwa eti nipo kama mumewe (babu) ambaye alifariki kitambo sana kabla hatujazaliwa.

Upande wa darasani nilikuwa vizuri sana tena sana kitu ambacho kiliniongezea upendo kwa bibi na hata ile mimi kusifiwa sana huku na huku kutokana na uwezo wa darasani alinipenda sana.Ikafika wakati akawa anachukizana hadi na watoto wake kwa sababu yangu yani nitende baya au zuri,yote kwake ni bora.Ukinigombeza tu kidogo asikie au nikaseme basi atalala mbele na wewe.

Nilipoingia form six tu mwanzoni,nikapata taarifa bibi kafariki na nilikuwa shule ya mbali kidogo.Nilihisi dunia imebadilika na imekuwa jehanamu.Isitoshe hadi anafariki hospitali alikuwa anataja tu jina langu jamani niitieni fulani alisisitiza sana lakini hakuniona hadi mauti inamfika.

Jamani upendo wa bibi ni balaa na sijawahi kupata upendo kama huo hadi leo yani iwe kwa baba mzazi,ndugu au hata mpenzi (sijaoa nina mpenzi).
Nimemisi upendo wa bibi kwani sasa hata ndugu tu kukujulia hali ni vigumu kila mmoja bize na yake au labda itokee shida ndio utawaona au uwe unawatafuta wewe.Bibi amenifundisha upendo kwa vitendo nimemmisi sana.Yani kwa upendo wake hata angekuwa mchawi basi angenirithisha uchawi.

KUPENDWA NI RAHA SANA KATIKA MAISHA.

Na hii ndio sababu ya kujiita Mtoto Wabibi.

Nitakukumbuka daima

R.P.I my glandmother
 
Stori yako inatufundisha nini?

Huo ni uhalisia wa maisha yangu.haujalazimishwa kucomment.Tambua watu tumekuwa katika mazingira tofauti.
Mnaudhi sana watu kama nyie ambao mmezoea kushinda kwenye majukwa ya mapenzi.
 
Huo ni uhalisia wa maisha yangu.haujalazimishwa kucomment.Tambua watu tumekuwa katika mazingira tofauti.
Mnaudhi sana watu kama nyie ambao mmezoea kushinda kwenye majukwa ya mapenzi.
umeleta post, kuna tatizo kuulizwa? Kawaida ukileta post JF ujiandae na suali la aina yoyote na sio kupanic, unachotakiwa kufanya ni kuidefend post yako ili watu waweze kuitambua zaidi, sio uhitaji pongezi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…