SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wanasema kwa mpira wa sasa, magoli mengi yanatokea kwenye mipira ya kutengwa.
Wengi wanadai Denis Kibu sio mchezaji mzuri kisa hana magoli au assist nyingi ila wanasahau ni mmoja wa wachezaji wenye kuchezewa faulo kuliko mchezaji mwingine katika ligi ya NBC (ni mtazamo tu ila sina takwimu rasmi).
Shida inakuja sehemu tatu.
Kwanza, Simba ya msimu huu haina wapigaji wazuri wa faulo. Jiulize, ni magoli mangapi ya faulo na penati waliyokuwa wanafunga kina Saidoo na Chama yaliyokana na faulo alizochezewa Kibu? Sasa hivi hakuna wapigaji hao ingawa Simba inapata faulo nyingi sana nje kidogo tu ya 18.
Kuna mechi niliona hadi Kibu mwenyewe alipiga faulo nikasema kweli Simba msimu huu haina wapigaji.
Pili, waamuzi hawamtendei haki kisa ni mchezaji anayeonekana anatumia nguvu kwa hiyo kuna faulo nyingi ambazo haziitwi kisa waamuzi wanadhani hawezi kuangushwa kama anavyoanguka.
Tatu, kuna faulo ambazo haziitwi kwa sababu kuna kitu kidogo Kibu anakosea. Kibu akishaona beki anakuja, hajishughulishi tena na mpira na hafanyi tena juhudi za kuingia na mpira ndani, anakuwa kama anategea na kusubiri aguswe ndiyo maana marefa wanameza filimbi.
Pia hakuna faulo itaitwa wakati uko karibia na mstari halafu unaelekea direction ya kuutoa mpira nje badala ya uelekeo wa goli. Mifano ni mechi ya derby zile faulo alizofanyiwa na Mudathir na Bacca.
Kibu anafanyiwa faulo nyingi za namna hii. Ajifunze kuhakikisha ana timing nzuri hata audokoe tu mpira uelekeo wa goli kabla yeye hajaguswa badala ya kujaribu tu kuulinda mpira usiguswe na mpinzani, penati zake zitaongezeka sana.
Mwisho wa siku, Simba ifanyie kazi kupata wapigaji faulo ndiyo itamfaidi Kibu na anachokifanya uwanjani. Leo hii hadi Zimbwe anapiga faulo za Simba wakati ni mmoja wa wachezaji walio na uwezo mdogo sana wa kupiga mipira mirefu.