Sababu ya Msingi kuachwa Lomalisa akaletwa Boka ilikuwa ni ipi?

Wewe ni Kolo,hakuna mwanayanga asiyefahamu kwasasa timu inachopitia!
 
Boka ana mbio lakini mbio zake hazina madhara Kwa wapinzani mkuu!
madhara mojawapo ni kumtisha adui, adui anasambaratika na kuanza kumfukuza huku ameacha defence wazi na cross zake zimekuwa hatarishi sana kwa adui. kwa kifupi huwezi kumlinganisha kabisa boka na lomalisa. kila mara lomarisa akiingia watu walikuwa wanashika moyo kujua muda si mrefu kuna kadi. na mguu wake ni mmoja tu wa kushoto ambao hata hivyo haumeneji kama aziz ki.
 
et sure boy ni bora kuliko aucho ukimuuliza sure boy umemwona mechi ipi hakuna jibu

timu kushinda kwa mbinde ndo raha
Kama Kuna shabiki wa Yanga ambaye haoni Yanga imeshuka Ubora atakuwa na tatizo la kiakili!
 
Mkuu Boka Hana maajabu,Lomalisa Krosi zake zilikuwa na Impact,huyo Boka niambie ni Krosi ngapi amepiga zilizo na Impact Kwa timu!,Lomalisa alijua kufinya na kuwapunguza wapinzani,Boka akishika Mpira yeye anachowaza ni mbio tu, wapinzani wameshamjulia na ndiyo maana Hana madhara Kwa wapinzani,labda Kimataifa huko ambalo hawajamjua lakini ligi ya ndani sidhani kama atakuwa na impact Kwa timu!
 
Mkuu hata uwe na kocha gani, timu haiwezi kuwa ktk level ile ile ya ubora muda wote, kilichobora kwetu sasa ni matokeo, licha ya kua tunapitia kipindi kigumu.
 
Muhimu pointi tatu zinapatikana kwenye kila mechi. Hayo masuala ya timu kucheza vizuri/vibaya yaachiwe kocha na benchi lake la ufundi.

Mkuu najua mashabiki wengi waganga njaa hamuekewi kitu,subiri timu ifungwe halafu Makolo watuzidi pointi kadhaa ndipo mtapofahamu ninachokisema!,kwasasa tunashinda papatu papatu mnafurahi?

Yanga siyo timu ya kushinda papatu papatu!
 
Mkuu acha Kuwa shabiki maandazi,Kwasasa Yanga anacheza vibaya na sometimes kutokuruhusu goal siyo kwamba timu

Mkuu acha Kuwa shabiki maandazi,Kwasasa Yanga anacheza vibaya na sometimes kutokuruhusu goal siyo kwamba timu inacheza vizuri!
Timu Gani inacheza vizuri zaidi ya Yanga kwenye ligi.

Kama Yanga inacheza vibaya
 
Kwa hiyo yale magoli dhidi ya Vitalo na wahabeshi, hayakuwa yanatengenezwa na pressing ya wachezaji wa Yanga?
 
Timu inacheza kila baada ya siku 2 au 3, wachezaji wengi wanaitwa timu za taifa, kumbuka hawa ni watu sio roboti. Ratiba ni ngumu. Timu imecheza na simba bila maandalizi ya kutosha, baada ya siku 2 imecheza na jkt then coastal kwenye uwanja mbovu. Keshokutwa icheze na singida then Azam. Wewe ungeweza?
 
Mkuu acha Kuwa shabiki maandazi,Kwasasa Yanga anacheza vibaya na sometimes kutokuruhusu goal siyo kwamba timu inacheza vizuri!
Wewe ni shabiki wa Simba acha ujinga mzee!!


Haya sio maneno ya Shabiki wa Yanga!!

Shida Yanga anahukumiwa kwa Standard na ubora wake alioujenga!!
 
Lomalisa ni bora sana kuliko boka! Lomalisa anatumia akili sana kila alipokuwa anapanda alikuwa analeta muunganiko mzuri na akina azizi ki! Boka ana nguvu na speed lakini ubunifu hakuna! Sijui kwa nn lomalisa aliachwa!
 
Labda nikujibu kitaalamu hoja yako kwa kufata sayansi ya Mpira na sio mihemko ya shabiki asiyejitambua na asiyeuelewa Mpira,

1) Yanga katumia energy kubwa sana kwa misimu 3 mfululizo uku akicheza mechi nyingi zaidi kuliko timu yoyote hapa Tanzania ndani na nje ya nchi ivyo kitaalamu lazima wawe na fatique na lazima uwezo wao upungue kwa kiasi Fulani ili kutengeneza energy mpya waliyopoteza ndio maana wanafanya game management kwenye Kila mechi( kuna mda watakushambulia na Kuna muda watakuachia ucheze wewe Mpira kwenye eneo lako awatumii nguvu kubwa)

2) Hoja ya pili inayofanya yanga aonekane kashuka ni kukamiwa na timu zote anazokutana nazo, ni jambo la kawaida kwa bingwa mara 3 mfululizo kukamiwa kwasababu Kila timu inakuwa inataka kumzuia asichukue Tena ubingwa ama zinakuwa zinataka kumfunga bingwa ili kuvunja mwiko wa kutokufungwa, matokeo yake yanaifanya yanga kupata wakati mgumu kufunga magoli mengi maana timu nyingi kwa sasa zinakaa nyuma ya Mpira azitaki kufunguka wanapocheza na yanga wanaona ni Bora wafungwe na timu nyingine magoli mengi lakini sio yanga!

3) Hoja ya 3 ni ratiba ya mechi na mechi kwa sasa sio rafiki, timu inacheza mechi Kila baada ya siku 3 na muda mwingine inatakiwa usafiri kwenda mikoani, ni changamoto nyingine utaweza kufanya mazoezi saa ngapi na kurudisha mwili kwenye utayali saa ngapi!

4) hoja ya 4 ni aina ya viwanja, yanga anayecheza uwanja wa Azam complex au taifa au kmc complex ni tofauti na yanga atakayecheza sokoine mbeya, Sheikh amri abeid Arusha, au lake Tanganyika kigoma, approach ya mechi kwenye viwanja kama ivyo lazima ibadilike uwezi kuweka Mpira chini ama Mpira kuflow kama viwanja vingine Bora, ivyo unaweza kuona yanga anapata shida ukadhani ameshuka kiwango lakini inakuwa ni namna ya kucheza kimbinu ili kupata point 3 muhimu kwenye ivyo viwanja vigumu na kuepusha majeraha kwa wachezaji wanaokuwa wanacheza kwa tahadhali ya kuumia!

Nafikiri nimekujibu vizuri hoja zako kama utakuwa umenielewa utakuwa umepata vitu vya kiufundi vinavyoifanya yanga ionekane imeshuka kwa sasa lakini aijashuka kama mnavyofikiria!
 
Lomalisa aliwatia Sana hasara dawasco alikuwa anamwaga majo hovyo


Mwanamke NI Kama mavi ya ngo'mbe ukiyaona nje Kama yamekauka tia mguu ndo utajua hakuna rangi utaacha kuona
 
Lomalisa ni bora sana kuliko boka! Lomalisa anatumia akili sana kila alipokuwa anapanda alikuwa analeta muunganiko mzuri na akina azizi ki! Boka ana nguvu na speed lakini ubunifu hakuna! Sijui kwa nn lomalisa aliachwa!
Nje ya hapo pia alikuwa mstaraabu sana ila kwenye uchezaji jamaa alikuwa anajua sana ku scan mchezo
Boka sijamuelewa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…