Sababu ya Sunday Manara kuitwa computer

Sababu ya Sunday Manara kuitwa computer

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697
Majuzi mchezaji nguli (ligend) kuwahi kutokea hapa Tanzania miaka ya 70-hadi 80 Bwana Sunday Manara alialikwa kwenye studio za AZAM TV katika moja ya vipindi vyake vinavyohusu michezo.

Pamoja na mambo mengine mtangazaji alimwuliza nguli huyo sababu ya mashabiki kumpachika jina la computer maana Enzi za miaka 70 kulikuwa hakuna mashine hizo hapa nchini.

Nilishangaa sana Sunday Manara kujibu eti alikuwa hajui kwa nini mashabiki wa Yanga walimwita yeye ni computer.

Nichelewa kutoa ufafanuzi huu kwa sababu nilikuwa safari huko Manika Msumbiji sasa nimerudi na Sunday Manara akae tayari kujua kwa nini sisi mashabiki tulimpa jina la Computer.

Sababu ya Sunday Manara kuitwa computer ilikuwa ni baada ya mechi ya Kombe la taifa kati ya Morogoro na Pwani mchezo uliofanyika mkoani Tanga. Mwanzoni Taifa cup ilikuwa inafanyika uwanja wa Ilala, mikoa yote ilikuwa inasafiri kuja Dar kwa mashindano hayo ambayo yalikuwa ni maarufu sana na yalikuwa na msisimko mkubwa.

Kulikuwa na wachezaji kama Chuma, Namajojo toka Mtwara, Mohamed Nyange, Matata, Sued toka Dodoma, akina Manga,Jella, Njenje toka Morogoro, akina Lyimo, Idd toka Kirimanjaro, Kitwana Manara, Dilunga, Katinko, Amidu,akina Gobbos taka Pwani, Leopard Tasso Mkebezi toka Bukoba pia akina Antony Nyembo toka Mwanza n.k

Sasa siku hiyo ndo kukawa na mechi kati ya mkoa wa Pwani na Morogoro(pwani ya Enzi hizo ilikuwa inajumuisha na Dar-lle-Salaam) mwaka 1974 mkoani Tanga maana mashindano haya baadae yalianza kuchezewa mikoani. Ikafika sehemu Fulani ya mchezo huo kipindi cha kwanza tu Sunday aliipiga chenga ngome yote ya Morogoro au aliihesabu defence na kufunga goli.
Enzi hizo kulikuwa na calculator za kizamani zilizokuwa zinapatikana shirika la reli au Posta au bank zilikuwa zinatumika kufanyia hesabu wanajamii walikuwa wanaziita computer, zilikuwa za kuiumlishia hesabu ndogo ndogo tu. Sasa kwa kuwa calculator hizo za kizamani ambazo tulikuwa tunaziita computer zilikuwa zinamaliza kujumlisha haraka, na kwa kuwa Sunday aliipangua ngome ya Morogoro akaimaliza yote ndipo akafananishwa na calculator hizo, hapo ndipo jina lilikoanzia.

Waliopo karibu na Mzee Sunday wamjuze chanzo cha jina lake.
 
Back
Top Bottom