Sababu ya Waziri Bashe kukataa msaada wa mchele wa Wamarekani: Je, ni uwepo wa virutubisho, kutokuwa na utapiamlo nchini au hatuna shida ya mchele?

Bashe pale kaleta siasa tu. Wanasiasa Tz saivi wamekua na tabia kwamba ikitokea yakifanyika maamuzi yakaleta kelele kwa raia, basi wanaibuka kujifanya wapo upande wa raia huku wakitoa kauli za vishindo. Watu wasiopenda kufikiri ndo hua wanawaelewa
 
bashe amefanya la maana sana kukataa mchele, kama kweli amekataa. Tanzania hatuna njaa ya kuhitaji mchele toka marekani, labda ungekuwa umenunuliwa hapahapa ukasambazwa kwasababu upo. wameweka nini huko marekani, nani kasema Tanzania tunakufa na njaa hadi watuletee mchele? watu wenyewe siku hizi wanapaka homoni hadi kwenye nguo ili watu wawe na hormonal imbalance dunia iongezeke mashoga wawe wengi ili wapiganie haki dunia yote iweke sheria za mshoga. sisi sio manguruwe au mifugo ya kufanyiwa experiment kwenye vyakula. kuweni makini sana na hao wazungu. walitukosa kwenye corona, watatutafuta tu kwa kingine.
 
WAZUNGU HAWAJAWAHI KUTOA MSAADA USIO NA MREJESHO/FAIDA KWAO. KIUFUPI HAWAJAWAHI KUTUTAKIA MEMA
TAFAKARI KUHUSI MRADI WAO WA HIV/AIDS HADI LEO WAAFRIKA WANATESWA KWA KUTOKUJUA UKWELI WA HUO MRADI WA MAREKANI BARANI AFRIKA
 
Walikukosaje kwenye corona? 'Nchi hii ina wajinga wengi sana' alipata kusema NW wa Afya. Mimi ni nani nipingane na mtu mwenye data za afya zetu
 
Walikukosaje kwenye corona? 'Nchi hii ina wajinga wengi sana' alipata kusema NW wa Afya. Mimi ni nani nipingane na mtu mwenye data za afya zetu
mkuu, najua wewe mchele ule watoto wako hawatakula, wala wewe hautakula. kama basi nchi imejaa wajinga na unatuita wajinga, basi nenda kapike huo ubwabwa ule wewe na watoto wako.
 
mkuu, najua wewe mchele ule watoto wako hawatakula, wala wewe hautakula. kama basi nchi imejaa wajinga na unatuita wajinga, basi nenda kapike huo ubwabwa ule wewe na watoto wako.
Wewe ambaye watoto wako hutaki wale umejaribu kuwapelekea huo mchele wa ndani wenye uhitaji ili wasile huo wa nje? Wewe ni mtu wa hovyo kwa sababu unajaribu kuzuia jirani yako aliyelala njaa asipewe chakula na msamalia mwema ilhali wewe huwezi msaidia na hutaki kumsaidia?! Je, lengo lako ni ili afe njaa?
 
Bado..

Msaada wa mchele toka marekani..wangepeleka Congo!
 
Kupokea msaada wa Chakula wakati hatuna janga lolote ni Kuivua ngoa Serkali na Nchi nzima kiujumla, wacha tukaze ila Beshe aje na solution.
 
Elimu ya Tanzania imezalisha watu wajinga sijawahi kuona. Hivi wewe bila hao wazungu ungekuwa hai sasa hivi? Hivi wakisema kuanzia leo kila mtu ajifungie kwake, hakuna kuuziana, hujui hata hiyo simu unayoandikia ujinga kama huu hutakuwa nayo?
kwani wao bila waafrika wangekua hapo walipo?
kama maandishi yalitoka Misri nafikiri hii nchi ipo kwa wazungu!
Nafikiri pamoja na nia nzuri kwao lakini ni vyema Mahindi na mpunga vitoke kwetu na hayo madawa yakachanganyiwa hapa shida iko wapi?
 
mwenzetu umesoma wapi? wanapotoa watu waelevu waliotayari kukubali kila kitu cha mzungu bila kuhoji?
 
mwenzetu umesoma wapi? wanapotoa watu waelevu waliotayari kukubali kila kitu cha mzungu bila kuhoji?
Sijawahi kusema tukubali kila kitu cha mzungu bila kuhoji. Siyo cha mzungu tu ila hata cha hawa hawa wakoloni weusi, kina Bashe. Tatizo lipo pale unapohoji na hoja yako ni ya kipumbavu kabisa.
 
kwani wao bila waafrika wangekua hapo walipo?
kama maandishi yalitoka Misri nafikiri hii nchi ipo kwa wazungu!
Nafikiri pamoja na nia nzuri kwao lakini ni vyema Mahindi na mpunga vitoke kwetu na hayo madawa yakachanganyiwa hapa shida iko wapi?
Tulikuwa wapi tusione hilo tatizo mpaka mgeni alione? Hivi wewe unaamini kabisa kuwa serikali hii ya CCM inajali watoto wa shule kula? Hayo mahindi au mchele kama tunayo kwa nini hatuwalishi? Au wewe mwenzangu maisha ya vijijini huyajui? Mzungu yeye anatoa surplus aliyonayo. Una njaa unapewa msosi halafu unagoma eti upewe fedha! Hii ni akili?
 
Bashe pale kaleta siasa tu. Wanasiasa Tz saivi wamekua na tabia kwamba ikitokea yakifanyika maamuzi yakaleta kelele kwa raia, basi wanaibuka kujifanya wapo upande wa raia huku wakitoa kauli za vishindo. Watu wasiopenda kufikiri ndo hua wanawaelewa
Sahihi
 
Udini naushamba kwelimukoa yadodoma nakandayakati haliya utapia mlonikubwa waacheushamba uwezikumpangia mtuakusaidienini
 
Wewe unashindwa kutofautisha shida binafsi ya mtu na shida inayoikumba nchi. Tz haijatangaza baa la njaa. Kuwepo kwa baadhi ya watu wenye uhitaji wa chakula haihalalishi kuomba msaada wa chakula kutoka nje. Hii nchi si kame. Kusaidiwa basic need kama chakula inaleta taswira mbaya sana. Sijasikia nchini watu wanakufa kwa kukosa chakula. Tatizo ni maarifa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…