N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Humu JF na kwingineko kwenye Social platform kumekuwa na mijadala isiyoisha 'endless debates' juu ya magari madogo ya kutembelea vs yale makubwa na yenye injini kubwa...Binafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwanini hawa wanapenda yale na wale wanapenda haya!!...na huu ndio mtazamo wangu
MADAI YA WANAOPENDA MAGARI MAKUBWA SUVs
1. Wanadai kuwa yanakimbia sana
2. Wanadai kuwa yapo juu unapanda,sio kutumbukia.
3. Wanadai kuwa yanatunza heshima/fahari (prestige) kwamba una hela ya mafuta na matengenezo
4. Wanadai kuwa yanabeba mizigo na watu wa kutosha hususani kwa safari ndefu
5. Wanasema haya magari yanakwenda vizuri na kwa ufanisi kwenye barabara zisizo vizuri 'rough roads'
HOJA ZANGU KUPINGANA NA HAWA
1. Bei ndogo; Hawa jamaa mabibi na mabwana wao wanadai kuwa eti haya magari yao ni bana matumizi kwamba ni rahisi kuingia nayo road kuyapa service,kuyanunulia mafuta na hata kuyaosha, unalipa buku mbili tu jamaa anakuoshea gari na maji ya mfereji...Aidha wanasema gari hizi ni bei chee huko zinakouzwa kwa hiyo huhitaji kuchimba sana mfuko ukiwa na USD 1500 tu unapata kagari kako Japan.
2. Wanasema ni rahisi kuegesha; Si unaelewa tena watu wa siku hizi kila kitu wanataka rahisi rahisi tu, gari dogo lisilokuwa manual ambalo unaweza kuegesha kirahisi hasa ukizingatia kwamba hapa kwetu Tanzania ni 'watu' wachache sana wanaojua utaratibu mzuri wa kuegesha gari hasa huku mijini...wengi wanashindwa kuegesha magari makubwa kwa hiyo kagari kaduchu ni rahisi kuegesha.
3. Wanadai kuwa ulaji mzuri wa mafuta; hoja hii hata mimi naiunga mkono 'hutu tugari'Samahani kusema tugari, tunakula mafuta kidoogo sana...ukiweka ya buku Tano unafika kwako(kwa hili tuseme wote asante mzungu) sasa we fikiria gari kama Suzuki Jimny au Alto kana eti 540cc kweli haka ukiweka mafuta ya elfu kumi si unasahau!!!
4. Wengine wanadai kuwa magari haya madogo yana starehe Zaidi kuliko makubwa hasa zile Salons ukilinganisha na makubwa haya sijui kama kuna ukweli kwenye hili.
5. Wanadai kwamba wigo wa uchaguzi kwa aina ya gari ulitakalo ni mkubwa tofauti na yale makubwa.
HOJA ZANGU KUPINGANA NA HAWA
Sasa karibu kwa mjadala na usimaindi lugha iliyotumika Maisha sio magumu kihivyo utakuwa unayaongezea ugumu...jadili tu kwa upendo mwingi iwe una kabebi woka au kubwa j...
nyadikwa.
MADAI YA WANAOPENDA MAGARI MAKUBWA SUVs
1. Wanadai kuwa yanakimbia sana
2. Wanadai kuwa yapo juu unapanda,sio kutumbukia.
3. Wanadai kuwa yanatunza heshima/fahari (prestige) kwamba una hela ya mafuta na matengenezo
4. Wanadai kuwa yanabeba mizigo na watu wa kutosha hususani kwa safari ndefu
5. Wanasema haya magari yanakwenda vizuri na kwa ufanisi kwenye barabara zisizo vizuri 'rough roads'
HOJA ZANGU KUPINGANA NA HAWA
- Sio kweli kwamba mara zote magari haya hufanya vizuri 'off road' yaani nje ya barabara laini kv lami, baadhi ya haya ni mabovu sana na yanavunja sana shokamzoba,yanapoteza sana wheel alignment, ball joints na control arms sie tunaita 'mikono' case study prado,xtrail
- Magari haya sio Rafiki kwa matumizi ya mjini kutokana na uzito mkubwa (over 1 tonne per shaft)
- Magari haya hupata changamoto kubwa ya maegesho hasa katika miji yenye msongamano kama vile Dar es salaam
- Ajabu kubwa ni kwamba magari haya ni makubwa tu kwa umbo kwa nje lakini ndani hakuna ukubwa kiviile(kubwa jinga) mengi yana ukubwa wa injini mdogo tu mf CC 2000,1500 AU 3000 wakati some salon cars zina engine kubwa kuyaliko haya mashangingi….yanaonekana makubwa katika matairi, mabampa nk lakini hakuna ukubwa kiviile.
- Kutokana na kujengwa kuwa midude mikuubwa , haina uimara na uthabiti yawapo barabarani...ni miongoni mwa private cars ambazo hazina balance ukilala mbele kisawasawa...we jaribu kutembea spidi zote na hii midude kwenye kona za Iyovi ni machache sana kati ya haya yana uthabiti kwenye kona tunaita cornering stability, ukikosea kubalance speed kwenye kona unalala nalo...tofauti na vibebi woka unatembea tu viko stebo.
- Gharama za matengenezo ni kubwa wengi wanalialia tu, nina mifano hapa usilete povu kwamba ooh tuna hela...kama zipo komboeni haya magari yenu yanaziba nafasi.
1. Bei ndogo; Hawa jamaa mabibi na mabwana wao wanadai kuwa eti haya magari yao ni bana matumizi kwamba ni rahisi kuingia nayo road kuyapa service,kuyanunulia mafuta na hata kuyaosha, unalipa buku mbili tu jamaa anakuoshea gari na maji ya mfereji...Aidha wanasema gari hizi ni bei chee huko zinakouzwa kwa hiyo huhitaji kuchimba sana mfuko ukiwa na USD 1500 tu unapata kagari kako Japan.
2. Wanasema ni rahisi kuegesha; Si unaelewa tena watu wa siku hizi kila kitu wanataka rahisi rahisi tu, gari dogo lisilokuwa manual ambalo unaweza kuegesha kirahisi hasa ukizingatia kwamba hapa kwetu Tanzania ni 'watu' wachache sana wanaojua utaratibu mzuri wa kuegesha gari hasa huku mijini...wengi wanashindwa kuegesha magari makubwa kwa hiyo kagari kaduchu ni rahisi kuegesha.
3. Wanadai kuwa ulaji mzuri wa mafuta; hoja hii hata mimi naiunga mkono 'hutu tugari'Samahani kusema tugari, tunakula mafuta kidoogo sana...ukiweka ya buku Tano unafika kwako(kwa hili tuseme wote asante mzungu) sasa we fikiria gari kama Suzuki Jimny au Alto kana eti 540cc kweli haka ukiweka mafuta ya elfu kumi si unasahau!!!
4. Wengine wanadai kuwa magari haya madogo yana starehe Zaidi kuliko makubwa hasa zile Salons ukilinganisha na makubwa haya sijui kama kuna ukweli kwenye hili.
5. Wanadai kwamba wigo wa uchaguzi kwa aina ya gari ulitakalo ni mkubwa tofauti na yale makubwa.
HOJA ZANGU KUPINGANA NA HAWA
- Speed; Aisee hutu tugari tunakuwaga tuzuri ila twingine hatuendi kabisa kwa sababu mbalimbali ikiwemo huo udogo wake wa injini nk
- Kwenye barabara zetu za Afrika ambazo nyingi bado hazina lami ni mateso sana kuendesha gari ndogo hasa kama unaishi mabonde kuinama...aisee utapata tabu sana hasa wakati wa mvua….kwa sie wazee wa spana tunapenda hali hii iendelee tupate rizki Zaidi.
- Nafasi; Tuache utani hutu tumotokaa tuna nafasi finyu sana hasa kwa abiria wa nyuma na kama ni mrefu ndio kabisaaa maana goti linagongana na kiti cha mbele...halafu kama safari ni ndefu utafika magoti kama yamepigwa misumari!
- Mizigo; ukibebesha mzigo mzito, uwe ni wa abiria au wa mizigo ya kawaida , jiandae kutuletea tufix huko chini maana mineso yote itakuwa ishaenda kwao.
- Katika uhalisia ulaji wa mafuta sio hoja kwa sababu bado hatuoni kama hilo linawasaidia , wangapi wana injini ndogo lakini wanaogopa hata kuwasha AC eti mafuta yataisha!!
- Heshima; hili lipo wazi, huku kwetu Afrika ukiwa na gari kubwa unaheshimika Zaidi, hata uenyekiti wa serikali ya mtaa utapata...Siasa imeleta haya refer magari ya wabunge nk...
nyadikwa.