Tetesi: Sababu za Dkt. Kalemani kutumbuliwa Uwaziri, genge lamponza

Vyovyote vile kalemani kaondolewa ili watu wapige hela. Nguzo za zege badala ya miti kutoka afrika kusini na mengine vigogo wanahusika kumng'oa. Ngoja tuone january na wapiga dili wenzake wakineemeka.
Kwa taarifa yako, aliyezuia kuagizwa kwa nguzo toka nje ya nchi ni profesa Sospter Muhongo ambaye pia ndiye pia alishusha bei ya kuunganishiwa umeme toka zaidi ya tshs milioni moja hadi tshs 375,000/= (hatua kubwa sana). Kalemani akaja kushusha umeme toka 375,00 hadi elfu 27,000 (ingawa ni kwenye maandishi tu uhalisia mnaujua) kingine alichofanya kalemani ni hiyo ya kushauri utengenezaji wa nguzo za zege ili kuepuka uharibifu wa nguzo kwa kuchomwa moto.
 
Kalemani ni mbishi na anakosa uelewa wa biashara. Lakini pia huko nishati watu wametafuta fursa za kurudisha mirija yao kitambo na waziri Kalemani ndio alikuwa kisiki. Yetu macho tu ...
 
Mimi nashangazwa na mambo mengi Tz., tokea nizaliwe mawiziri wa Tanzania ni hao hao, kalemani, mbarawa, simabcheweni, muhagama, sijuwi makamba, nchemba, ndugai yaani rais yoyote anaekuja ana deal na watu hawa hawa maanake nini na tumeambiwa Tanzania sasa ni taifa lina watu milioni 60 takriban.,

Kwa nini hakuna sura mpya? Huyo mbarawa na makamba toka enz za JK adi leo yaani Tanzania muna udhaifu sana kwenye teuzi., ndio mana waziri akitumbuliwa anarudi zake kutulia anajua tu atateuliwa tena na tena., nchi mbov sana
 
Sijui makala hii inauhalisia kiasi gani, na binafsi naamini hii inachangiwa zaidi na utaratibu wa usiri haswa katika taasisi za umma juu ya mambo ambayo kimsingi hayahitaji huo usiri"
My take: kulingana na uzoefu wa muda mfupi nilioupata kutokana na kufanya kazi kwa karibu na watumishi waliokuwa kwenye iliyokuwa wizara yake, itoshe kusema Mheshimiwa kuwa kiutendaji mheshimiwa alizingua katika maeneo critical lakini kisiasa, alizikonga nyoyo za wananchi ambao kwa kiasi kikubwa walifumbwa macho wasione nini hasa kinaendelea nyuma ya pazia.
 
Kama ni hivyo basi Kalemani ni mzalendo, anataka makampuni ya wazawa nayo yapate nafasi.

Kwa hoja hii huyu ni hero siyo adui
 
Kalemani siyo msafi hata kidogo. Apumzike.

Kule Masumbwe, Halmashauri ya Mbogwe aliamuru TANESCO wapeleke umeme kilometer zaidi ya 20 kwaajili ya kumnufaisha shemeji yake ambaye anachimba dhahabu na ana plant ya kuchenjulia dhahabu kutoka kwenye tailings, nje kidogo ya kijiji cha Mwabomba, wilayani Kahama.

Ili kuuficha uovu huo, umeme huo ulipokuwa unapelekwa kwenye plant ya shemeji yake kwa gharama ya TANESCO, nyumba 5 za wanakijiji cha Mwabomba ziliunganishiwa umeme, naye akajitokeza kwenye TV kusema kuwa Serikali imefikisha umeme kijiji cha Mwabomba, wakati mlengwa mkuu alikuwa ni shemeji yake.
 
Vyovyote vile kalemani kaondolewa ili watu wapige hela. Nguzo za zege badala ya miti kutoka afrika kusini na mengine vigogo wanahusika kumng'oa. Ngoja tuone january na wapiga dili wenzake wakineemeka.
Huna ufahamu wa kutosha kuhusiana na huyo Kalemani.
 
Kama makala ya gazeti hilo ni yakweli, Basi Kalemani atawatesa sana.
Kumbuka yupo hai, huyu sio marehemu.

My take,
Ametumbuliwa kwa uzalendo wake.
Akitetea wazawa.
Hii nchi ni ngum Sana.
Uzalendo wa kuumiza wananchi? Huo ni uwendawazimu wa hali ya juu.

Mtanzania anasafirisha kwa dola 47, mgeni anasafirisha kwa dola 6. Halafu kwa uwendawazimu tu, unasema apewe Mtanzania. We una akili kweli?

Tunahitaji Watanzania wazalendo, na siyo Watanzania wevi na majambazi. Hapa Kalemani kawa sehemu ya genge la Watanzania maharamia wanaowatesa Watanzania wenzao kupitia biashara ya mafuta. Hatujui Kalemani amekuwa anapata nini kutokana na kushiriki kwake kwenye huo uharamia. Achunguzwe. Na kama ikithibitika aliyafanya hayo kwa maslahi binafsi, afikishwe mahakamani kwa kutumia madaraka yake kujipatia manufaa binafsi.
 

Amevuruga mambo mengi sana. Wanamuitaje mzalendo? Urasimu na ujuaji wake umefukuza investors wakutosha. Ndio mnamuita mzalendo?
 
WATU wengine bwana,husubili WATU kuaribikiwa then waja na ngojera zao
 
Huoni sasa wewe kama ndio mpumbavu?

Huyo ni mwekezaji hata kama ni shemeji yake. kama ana hiyo miradi maana yake anaingizia selikali mapato.

Na kupitia yeye wananchi wengine watapata umeme!

Wtz iq zetu ni kidogo sana.
 
Kwa nn awe hero wakati kazi ya ku import mafuta wakipewa wazawa bei zinapanda?
Hujui chochote.

Fuatilia upandaji wa bei za mafuta kama sababu ni wazawa kuagiza
 
Hujui chochote.

Fuatilia upandaji wa bei za mafuta kama sababu ni wazawa kuagiza
Niko kwenye hii sekta tangu 2005 ndio sababu nakushangaa kumpa u hero huyu mwanasheria asiejua sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…