Biashara2000
JF-Expert Member
- Nov 9, 2013
- 649
- 547
Mambo zenu wanajamvi. Leo nimeona niongelee kuhusu kilimo na mchango wake katika kuongeza ajira kwa vijana wengi japa nchini. Katika vyombo vya habari kumekuwa na watu wengi wakiwa wanafanya majadiliano mbalimbali katika kuelewa ni njia gani zinaweza tumika kuondoa tatizo la ajira linalowakabili vijana wengi sana hapa kwetu tz. Watu hawa wamekuwa wakitoa maoni kwamba inabidi vianzishwe viwanda mbalimbali vinavyoweza toa ajira, ujasiriamali na pia kilimo. Lakini hili wazo la kilimo kama njia ya kutoa ajira limekuwa likipingwa na vijana wengi kwa sababu mbalimbali.
Leo nimeona nielezee sababu mbalimbali ambazo zinawafanya vijana wengi washindwe kuingia lwenye kilimo. Vijana wengi wamekuwa kila siku wakitoka wilayani na vijijini na kuja Dar wakiamini kuwa watapata ajira kirahisi. Hii imekuwa ni kinyume cha asilimia 901 ya vijana hao wanaokuja kwa kuwa wamekuta ajira hizo walizozitegemea hazipo, hivyo wamejikuta wakiishia kukaa mitaani bila shughuli hivyo wengine kushawishika kujihusisha na madawa ya kulevya, ujambazi, vibaka, wizi na kadhalika. Lakini kama wangejua kuwa unaweza tajirika kwa kilimo tena ndani ya muda mfupi tu iwapo utakifanya sawa sawa, basi nadhani wengi wangejihusisha nacho.
Kuna sababu mbalimbali zinazowafanya watu wengi wasijihusishe na kilimo.
1. Asilimia kubwa ya vijana nchini wamelelewa na jamii zao na familia zao kwamba mtu inabidi uende shule ili upate elimu ili uweze kuajiriwa. Ukiwakosoa wazazi wako kuhusu wazo hili, wanakujia juu. Hii ndio sababu kubwa inayowafanya vijana wengi waliokosa nafasi ya kwenda shule kuamua kuja mijini kutafuta kazi hivyo hivyo tu bila elimu kwa kuwa tu wameshaambiwa kuwa maisha ni kuajiriwa.
2. Watu wengi wanakihusisha kilimo na ushamba, ufukara, ujinga na umaskini. Pia inachukuliwa kama ni shughuli ya watu walioshindwa na maisha.
3. Inachukuliwa kama ni shughuli ngumu sana kufanya
4. Inachukuliwa ni shughuli yenye matatizo mengi unapoamua kuifanya
5. Inaonekana ni kazi inayohitaji mitaji mikubwa sana kuanza
Hizi ni miongoni tu mwa sababu nyingi zinazowafanya watu wengi waogope kufanya kilimo.
Ijulikane tu kuwa watu wengi sana wametajirika na kuwa mabilionea na mamilionea kutokana na kilimo tu. Watu hawa wanajulikana na wengine tunaishi nao mitaani kwetu. Mmoka wa watu hawa waliofanikiwa katika kilimo ni Masanja mkandamizaji. Unaweza ku google habari zake za kilimo kwenye mtandao na ukajionea mwenyewe.
Sasa tunafanya nini kupata suluhisho na matatizo hayo hapo juu? Zifuatazo ni suluhisho hizo.
1. Watu wanatakiwa kufahamu kuwa kuajiriwa si kila kitu katika maisha. Kujiajiri pia ni aina nyingine ya ajira. Nchi nyingi duniani watoto wanahamisishwa kuchagua aidha kujiajiri au kuajiriwa ndio maana vijana wao wengine wanaajiriwa na wengine kujiajiri na maisha yao kuwa mazuri. Kwa hapa nchini kwetu ni tofauti. Watu wanaamua kufuata wazazi wao walivyowaambia kwamba ni lazima wajiajiri. Fahamu kuwa ni sahihi tu kuamua kujiajiri.
2. Kilimo kinahusishwa na umaskini, ufukara na ushamba kwa kuwa katika maisha yao wamekuwa wakiwaona watu wanaotumia jembe la mkono na kufanya kilimo cha kizamani wanavyohangaika na hawafiki popote, hivyo kutishika na kuona ni cha watu maskini. Pia kutokana na sababu ya kwanza hapo juu, watu wengi wamelelewa kuamini kuwa kuajiriwa ndio kitu cool na si kilimo au kujiajiri. Ujasiriamali pia nao unapigwa vita na baadhi ya watu wakiamini nao pia ni ushamba. Kieleweke pia kuwa kilimo kikifanya kisasa kinabadilika kutoka kuwa cha kishamba au umaskini na kuwa cha kisasa na kitajiri. It is ok kufanya kilimo.
3. Kilimo sio kigumu kufanya kama kikifanya kisasa. Kijana ukimwambia rudi kijijini ukafanye kilimo yeye anadhani unamwambia nenda kachukue jembe la mkono ukalime. Jambo ambalo anarudi kwenye sababu ya pili hapo juu kuwa kilimo ni cha maskini. Kilimo cha siku hizi kinahusisha matrekta, power tillers, mbegu bora, mbolea (kuna maeneo mengi nchini huhitaji mbolea), umwagiliaji (hutegemei mvua za magumashi), mazao yenye soko la uhakika (kama unafanya kilimo kisicho na soko miaka nenda rudi kwa nini unaendelea nacho), kilimo kuchukuliwa kama biashara na si shughuli ya kujikimu, na kadhalika.
4. Unaweza punguza matatizo mengi yanayohusishwa na kilimo iwapo utakifanya kitaalamu kwa kuwashirikisha ma bwana shamba wa serikali ambao hata hivyo sio gharama kuwatumia kwa kuwa ni wa serikali.
5. Kilimi hakihitaji mitaji mikubwa kuanza. Mambo ya matrekta nk yasikutie woga, Siku hizi karibu kila wilaya na kijiji wana matrekta au power tillers ambazo zinakodishwa kwa wakulima ambapo wewe mkulima unalipia tu mafuta na kutumia vifaa hivyo kulimia. Pia havili mafuta sana. Shamba ambalo ungetumia mwezi mzima kulima na mkono unatumia siku 2 kulima kwa trekta au power tiller. Pia kufanya kilimo si lazima wewe kama wewe ndo ushike jembe au ufanye shughuli zote. Ishu kama kupalilia pale kijijini kuna vijana wengi hawana ajira unaweza watumia wakupalilie kwa ujira mdogo sana. Pia pembejeo nyingine nyingi siku hizi zinapatikana kwa urahisi katika maeneo mengi nchini ingawa sehemu nyingine zina matatizo kidogo. Hivyo huhitaji mitaji mikubwa kama inavyodhaniwa katika kufanya kilimo.
Vijana wanashauriwa kuamua kujaribu. Unwaeza tenga miezi mitatu hivi kwa ajili ya kujaribu kilimo. Kajaribu ukishindwa basi rudi mjini na endelea kubangaiza. Kwa mfano kulima ekari moja ya mahindi bila kutumia utaalamu wa kisasa unapata gunia 3 za mahindi ila ukifanya kitaalamu unapata gunia 15 20. Unaona tofauti yake? Pia kuna mbegu za kisasa siku hizi badala ya kulima mahindi kwa miezi 6 unapata mazao ndani ya muda mfupi kati ya miezi 2 na 3. Pia kwa mijini kama una eneo dogo unaweza fanya kilimo cha greenhouse ambacho kimewafanya watu wengi kuwa mamilionea.
Kwa kumalizia tu ningependa kutoa ushauri kwa vijana wengi turudi wilayani na vijijini tuwatumie wataalamu wa kilimo tufanye kilimo. Kilimo sio ushamba tena. Kinalipa. Muulize masanja mkandamizaji.