SoC02 Sababu za kukua kwa lugha ya Kiswahili Kimataifa na kudumaa nchini

SoC02 Sababu za kukua kwa lugha ya Kiswahili Kimataifa na kudumaa nchini

Stories of Change - 2022 Competition

King zack

New Member
Joined
Aug 20, 2022
Posts
1
Reaction score
0
SABABU ZA KUKUA KWA LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA NA KUDUMAA NCHINI

Kiswahili ni Lugha inayozidi kukua barani Afrika na duniani kote kadri siku zinavyozidi kusogea hili likidhihirishwa na maboresho na mabadiliko ya mitaala ya elimu katika mataifa mbalimbali barani Afrika ili kutoa mwanya wa kufundisha lugha hiyo ya Kiswahili

Mataifa ya Ghana, Madagascar, Nigeria na Misri ni baadhi ya mataifa yasiyokuwa ya ukanda wa Afrika mashariki yanayofundisha lugha ya Kiswahili mashuleni huku mataifa ya China, Korea kaskazini na Japan yakiwa ni miongoni mwa mataifa kutoka bara la Ulaya yanayofundisha lugha hiyo

Licha ya mafanikio hayo na mengine mengi ikiwemo pia Kiswahili kupitishwa na bunge la Afrika mashariki kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi katika mataifa ya jumuiya hiyo lakini bado Tanzania ambayo ni nchi mmiliki wa lugh hiyo haijaona umuhimu na thamani ya lugha hiyo

Mitaala ya elimu Tanzania kuanzia ngazi ya sekondari inadidimiza zaidi kukua kwa lugha hii kwani wanafunzi huisoma ligha hii kama somo na sio lugha ya kufundishia tena

Mbali na hivyo Serikali ya Tanzania pia licha ya kutambua kuwa asilimia kubwa ya watanzania enzi za ukoloni hawakupata elimu mashuleni lakini haijali kutumia lugha za mataifa mengine kama vile lugha ya kiingereza katika baadhi ya nyaraka na ofisi muhimu ikiwemo hospitali na mahakama

Ofisi nyingi za serikali zimeandikwa kwa lugha ya kingereza mfano (medicine room) badala ya chumba cha dawa, (medical lab) badala ya maabara ya matibabu sehemu ambazo watanzania wote wanatakiwa kupata huduma muhimu bila kujali elimu zao na uwezo wao wa matumizi na uelewa wa lugha hizo.

Bahati mbaya sana hata vyombo vya habari ambavyo vilitakiwa kuwa msitari wa mbele kukuza, kufundisha na kusambaza lugha ya kiswahili kwa ufasaha vimejikuta vikitumia zaidi kigezo cha lugha nyingine za kimataifa ikiwemo lugha ya kiingereza kama sehemu ya kujitangaza na kuonesha ukomavu wake zaidi.

Viongozi wote wa taasisi binafsi na za serikali hawawezi kuzungumza kiswahili pekee bila kuchanganya lugha ya nyingine ili kuonyesha ukubwa wao na uwezo wao wa kutumia lugha hizo badala ya kujivunia lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Vituo vingi vya redio na vipindi vyake majina yake ni ya kiingereza taasisi na mashirika mengi ya serikali na binafsi majina yake ni ya lugha ya kIingereza unadhani huku ndiko kukitangaza kiswahili kwa kizazi chetu chipukizi na kimataifa? La hasha tunatakiwa kupenda na kuthamini kilicho chetu kwani bila kufanya hivyo tusitegemee msaada kutoka kwa watu wengine.

NINI KIFANYIKE
Ili kukuza lugha ya kiswahili jitihada binafsi na mabadiliko ya sera ya elimu hasa mitaala na kuweka sheria za kusimamia matumizi ya lugha hiyo kwa ufasaha zianzishwe na kusimamiwa kwa taasisi zinazofuatiliwa na kuaminika zaidi na watu wengi ili kuwachukulia hatua wote wanaopotosha matumizi sahihi ya lugha hiyo mfano mzuri kuna maadili na sheria za taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji ambazo kila mtangazaji anatakiwa kuziishi kwanini pia sheria zisitungwe na kufuatiliwa ili kuilinda lugha ya kishwahili?

Pili serikali pia kukithamini kiswahili na kubadilishwa majina na maneno yote ya lugha nyingine mfano kiingereza hasa kwenye ofisi mbalimbali za Serikali na binafsi au kama sio hivyo ili kulinda pia uhusiano wetu na mataifa mengine basi ni vema hata zitakapotumika lugha za kigeni tuweke pia na tafsiri ya neno hilo mfano kwenye milango kama wameandika Pull basi kwenye mabano liandikwe neno Vuta kwani tunaolenga kuwapa huduma sio wasomi pekee.

Aidha kufanya mabadiliko ya nyaraka zote za serikali na za taasisi binafsi zisomeke kwa lugha ya kiswahili kama ilivyo kwenye katiba ya nchi basi na mikataba na maandishi yote yanayoilenga jamii yaandikwe kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili ili kuepuka changamoto ndogondogo mfano mahakamani na sehemu nyingine
 
Upvote 3
Well, inashangaza kukua kwa kiswahili kimataifa inachangiwa na Kenya kuchukua credit kwa kumiliki lugha ya kiswahili
 
Back
Top Bottom