Sababu za kupanda bei kitunguu 2015

Gagurito

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2011
Posts
5,600
Reaction score
806
Wakuu mwaka huu 2015 umekuwa tofauti sana na mwaka jana wa 2014. Soko la kitunguu limekuwa gumzo mwaka huu, mkulima kauza gunia moja la kg 100 mpaka Tsh. 250,000 shambani wakati mwaka wa jana miezi hii bei ilikuwa inachez kati ya Tsh. 30,000-50,000.
Nimefatilia kwa umakini sana juu ya mabadiriko haya yenye kufuru kubwa ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na madalalil wa masoko ya ilala, temeke na kinondoni, sababu za kupanda kwa bei ya kitunguu ni hizi hapa;
  • Kufanya vibaya kwa kilimo cha vitunguu vya Singida kutokana na kuibuka kwa ugonjwa ambao uliweza kuua mbegu za wakulima wengi hivyo kusababisha wachache kumudu na uazalishaji mdogo.
  • Wafanyabiashara na Walanguzi wa vitunguu toka Kenya, Uganda na Commoro mwaka huu wamekuja kwa kasi sana, ushindani wao ndio haswaa umepelekea kupanda kwa bei.
  • Kufanya vibavya kwa vitunguu vya Arusha na Moshi kutokana na hali mbovu ya hewa na kuibuka kwa magonjwa.
  • Hasara ya mwaka 2014 ilipelekea wakulima wengi kutokulima kwa kasi kwa eneo kubwa kama ilivyokuwa mwaka jana.
  • uzalishaji wa gharama umepelekea kupanda kwa bei ya kitunguu sokoni.
  • ushindani wa madalali katika masoko ya ilala, temeke na kaliakoo kumewezesha kutokuwa na mawasiliano ya karibu kati ya wao kwa wao kama wafanyavyo siku zote.
ANGALIZO: MWAKA HUU WA KICHEKO, UJAO 2016 NI KILIO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…