Sababu za kusoma India na si Tanzania wala US!!!



That is a Good point!

Sasa ni nani atakaejenga vyuo?? Vyuo vinajengwa kisiasa. Mtu anajenga chuo kikuu, huku akimulika ni kwa kiwango gani atashinda uchaguzi wa 2010, 2015 ..... badala ya kuangalia ni watu wangapi watakuwa wameelimika, baada ya miaka minne ijayo! Shame on Tanzanian leaders..

Tunawaponda wahindi, lakini kiuhalisia wanatuzidi mpaka sasa! Sisi tunaendekeza ufisadi, shule za kata kata elimu, urasimu, undugunization, urafiki-nization kwenye maofisi na taasisi zingine. Mie naamini Tanzania haitaendelea hata siku moja, UNLESS, atokee dikteta mtakatifu!!!
 

The closest thing we had, and in my opinion we will ever have, is Nyerere.

Jinsi nchi inavyoenda inaonekana kama miaka inavyozidi kwenda mbele ndivyo demokrasia itakavyozidi kuongezeka na nafasi za udikteta zitakavyozidi kupungua.

Na pia jinsi ufisadi unavyozidi ku take over, huku vitoto vidogo vikifundishwa ufisadi na baba zao na kuandaliwa kuchukua nchi, usitegemee kutakuwa na mtakatifu atakaye raise kwenye ngazi. Kwanza ili kupata ofisi lazima uhonge na kuchukua michango ya mafisadi, sasa utakatifu utatoka wapi?

Na jeshi la Tanzania hata halioti kufanya mapinduzi.

Kwa hiyo kama unategemea "dikteta mtakatifu" sahau.

Tulishakuwa na Julius Caesar wetu, aliitwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, fupa lilimshinda.

Kama unaangalia "a benevolent dictator" fupa lililomshinda fisi mbwa ataliweza?
 

Natamani angefufuka lakini ndo hivo tena.. Ilishatoka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…