Sababu za kuto chagua upinzani 2010

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
5,565
Reaction score
843
Kuna sababu nyingi naona ni heri serikali ya chama cha mapinduzi kuliko serikali ya chama chochote cha upinzani tulionao. Hii ni kwa sababu hata kama CCM kime tupa baadhi ya sababu ya kuto kichagua bado naamini upinzani haujatupa sababu ya kuwa chagua na hilo ndilo la muhimu kuliko yote.

1.Upinzani mara nyingi umebaki kusema nini CCM haijafanya badala ya kukazania kutuambia nini wao wata fanya tofauti. Ni vigumu sana kuwa sikia wapinzani pale kunapo kuwa hamna maneno dhidi ya upinzani. Upinzani wetu upo REACTIVE badala ya kuwa PROACTIVE!

2.Vyama vyetu vya upinzani ni vyama vya uchaguzi tu. Ni vyama vichache na mara chache sana vinavyo jinadi kabla ya uchaguzi.

3.Wengi wa wapinzani walio kuwaga CCM na serikalini hawana track record nzuri na wengi wao inaelekea siyo wapinzani wa kweli bali wali hama kambi baada ya kuona hawana masilahi CCM.

4.Japo vyama vya upinzani havipo madarakni lakini bado kuna baadhi ya vitu wangeweza kufanya kusukuma gurudumu la maendeleo nchini. Sija sikia chama chochote cha upinzani kikiwa na program zozote za kijamii. Sijawahi(I could be wrong) kusikia chama chochote cha upinzani kikichangia aidha hali au mali wakati maafa yanapo tokea. Kumbuka kutoa ni moyo si utajiri.

5.Hata upinzani kuna baadhi ya watu ni mafisadi. Tumesikia wengine ambao wame pata utajiri wao kwa biashara zisizo halali au hata kuiba fedha za vyama vyao. Je hawa wakipewa serikali hawata endeleza ufisadi huo huo tena katika njia kubwa zaidi?

Baada ya kutafakari kwa muda mimi naona bado CCM ni chama "bora" kuliko chochote cha upinzani. Naamini kabisa kwamba bila baadhi ya watu wanao ichafua CCM bado kingekua chama imara. Nadhani baada ya enzi za Nyerere kuisha kule kupokezana kwa madaraka kulienda kwa kundi bovu badala ya kundi imara na kundi hilo ndiyo lime set precedent ya mambo yote yanayo tokea sasa. Bado sijaona upinzani wa kweli Tanzania. Ni mtazamo wangu tu.
 
mbona vyama vya upinzani vinachangia matukio kama kawa, ipende nchi yako iepushe na mumiani
 
Huna jipya wewe tushawazoea nyie makatibu wa mafisadi. Chunguza vizuri utaona kwanini wapinzani wanapaswa kuchaguliwa 2010
 
Nadhani baada ya enzi za Nyerere kuisha kule kupokezana kwa madaraka kulienda kwa kundi bovu badala ya kundi imara na kundi hilo ndiyo lime set precedent ya mambo yote yanayo tokea sasa. Bado sijaona upinzani wa kweli Tanzania. Ni mtazamo wangu tu.
Kwa mtazamo wangu maneno yako hapo juu MwanaFalsafa ni sawa na mwanamme kusema pamoja na mke wangu kutembea hovyo hovyo nje ya ndoa lakini sijaona mwanamke mwingine yeyote atakayenifaa zaidi yake
 
mbona vyama vya upinzani vinachangia matukio kama kawa, ipende nchi yako iepushe na mumiani

Ok niambie wewe nichague chama gani kuiepusha na mumiani na taja sababu ya kwa nini unadhani hicho chama kitakua any better?....

BTW unaweza kunitajia mifano ya hayo matukio kama reference? Tunashare information mkuu.
 
Huna jipya wewe tushawazoea nyie makatibu wa mafisadi. Chunguza vizuri utaona kwanini wapinzani wanapaswa kuchaguliwa 2010

Waweza kuniita chochote unacho taka. Ninge kua na mawazo kama yako ningekua shujaa wako....samahani we don't think alike. Nime chunguza na hii ndiyo conclusion nliyo fikia. Hauja nipa sababu ya kufirikia otherwise. Panga hoja zako na kuja kivingine.
 
Kwa mtazamo wangu maneno yako hapo juu MwanaFalsafa ni sawa na mwanamme kusema pamoja na mke wangu kutembea hovyo hovyo nje ya ndoa lakini sijaona mwanamke mwingine yeyote atakayenifaa zaidi yake

Je kama hao wanawake wengine wanatembea hovyo zaidi nifanyeje? Kama kwa analogy yako vyama ni mwanamke niambie wewe "mwanamke" yupi kati yao ni bora zaidi? Karibia kila mtu aliye changia ameonyesha characteristic moja ambayo ni kupinga bila kutoa sababu au hoja. Yale yale ya upinzani kusema CCM au serikali ime kosea nini bila kusema wao watafanya nini.
 
Naona watu wengi humu wanakosa the point. Sijasema wala kumaanisha kwamba CCM hakina makosa. Napoint out kwamba TANZANIA HATUNA CHAMA MBADALA! Mpaka sasa sijaona argument ya chama kipi kinafaa badala ya CCM na kwa sabab zipi. Mimi nimetaja sababu zangu za kwa nini upinzani hazifai. Sioni mwingine akipinga kwa sababu.
 
Soma tovuti ya Chadema kwa kusudi la kujua maadhimio yao...
 
Tulishalijadili sana hili swala mkuu, angalia hii thread; japo tuliishia kutukanwa but as days going on....

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ni-kustahili-dhamana-ya-uongozi-wa-taifa.html


Mimi naona kuna kila sababu ya kuchagua wapinzani, naona sababu 100 na 200, za kuchagua wapinzani, CCM should go. Tatizo sio kuwa sioni wapinzani wa kuwachagua, hapana, wapinzania hawajajitoa kiasi cha kuwaaminisha kuwapa dola. Zambia mchungaji kalala jela miaka 3 akilazimisha serikali ijiuzulu, hapa sio kuwa tu hatujaona wachungaji, bali vyama vya upinzani.

If you go back in those days of yore, you will actually see, akina Mtikila, Bob Makani, Mrema, Lipumba Marando n.k walikuwa wanatisha na kuweza kuvuta umati.

Kilio changu ni vyama vya siasa vitafute mbinu za kupata kura kutoka kwa wananchi, na hii itawezekana tu wakicheza karata safi ya siasa,kujitoa, na kujisafisha!

Vyama vya siasa kupata kura ndogo ni aibu jamani., maana yake wananch iwamewakataa! hii haijalishi mtabisha kiasi gani humu JF!

Kutokuwa na upinzani mkali kwa JK ni alama tosha kabisa ya kushindwa, kuondoka ulingoni, na kuweka matumaini bungeni kwa Samuel Sita, ambaye naye ni CCM!

Mwanafalsafa sababu zipo ndugu nyingi tu, swala ni kuwa hawapo wa kuwachagua. period!

BOMU ambalo tusingependa litokee, ni kuwa vile vyama vyenye wabunge wachache, vikipoteza nafasi zao, basi upinzani kwa heri!

I will stand on this, sioni sababu ya kujidanganya kuwa wapinzani tutashinda ili hali hamna dalili, sipendi tupakane mafuta , ili hali mvua inanyesha, tunabisha hainyeshi.

Najua hii topic ni zile zinazofanywa nitukanwe sana na kuambiwa mnafiki, najua nikitukanwa nitapewa pole na kuangalia mbele, UKWELI UNAISHI

Chonde chonde wapenda taifa hili tuwaamshe hawa wapinzani, tunawapenda naam, lakini upendo wa kweli ni kuambiana ukweli!

Hivi ukiondoa Dr. Slaa jamani semeni ukweli nani mwingine mnamsikia japo akikohoa?

na ukitaka upime performance , basi Mtikila kawapita wote!
 
. Hii ni kwa sababu hata kama CCM kime tupa baadhi ya sababu ya kuto kichagua bado naamini upinzani haujatupa sababu ya kuwa chagua na hilo ndilo la muhimu kuliko yote.


unachosema ni ukkweli kwa sababu unaagalia shilingi kwa upande 1ja.Mbona wapinzani wamejitahidi kuonyesha kwa nn uwachague.Kashfa BOT, EPA,RADAR wamekuwa wazi kuzikemea bungeni. try too look the other side of the coin





B]Kuna njia nyingi za kufanya jambo lile lile .Kutokana na mfumo uliopo wa kisiasa usio na haki, uwelewa wa watanzania wengi kuridhika na kasumba ya amani na utulivu, etc. wapinzani wanawaonyesha wananchi the other side of CCM

Zaidi CCM yenyewe ni Reactive na si Proacctive. Cheki mfano wa hizo kashfa. kama CCM ingekuwa reactive which the rulling party should be then tungekuwa mbali.


MwanaFalsafa1 said:
2.Vyama vyetu vya upinzani ni vyama vya uchaguzi tu. Ni vyama vichache na mara chache sana vinavyo jinadi kabla ya uchaguzi.

Hii ni kutokana na mfumo. vyama vinafanya kazi katiko mfumo mgumu sana. Jaribu kifikiria CCM ingekuwaje kama Viwanja vya CCM kirumba Mwanza , Ali Hassan inyi tabora, ofisi mbali mbali na mali zote walizopata kutokana na watanzania kukatwa kodi zingerudishwa serikalini




MwanaFalsafa1 said:
5.Hata upinzani kuna baadhi ya watu ni mafisadi. Tumesikia wengine ambao wame pata utajiri wao kwa biashara zisizo halali au hata kuiba fedha za vyama vyao. Je hawa wakipewa serikali hawata endeleza ufisadi huo huo tena katika njia kubwa zaidi?

Mzee kwa kusema baadhi haya maneno hata CCM wamo wa aina hii. Zaidi CCM wamezoea wizi kiasi cha kwamba wanakwapua mchana kweupe. Huoni kuwa wapinzani hata wakiwa mafisadi wataiba kwa aibu.CCM hawana aibu ya kuiba


Baada ya kutafakari kwa muda mimi naona bado CCM ni chama "bora" kuliko chochote cha upinzani. Naamini kabisa kwamba bila baadhi ya watu wanao ichafua CCM bado kingekua chama imara.

Si chama Bora.kingekuwa chama bora kingewatimu wanaokichafua. Chadema wakishindwa akufukuza Mbowe unaweza kuelewa lakini ni vigumu kuelewa kwa nini CCM isiwanyanganye kadi wanaochafua jina la chama. Huoni kiwa CCM yenye miaka takriban 40 kuwa sawa na CHADEMA, UDP,CUF,TLP ni aibu.

NB
kuliko kumchagua mbunge mbovu wa CCM bora uchague mbunnge mbovu wa upinzani . Ata Add value,efectiveness na Efficency ya bunge
 
Soma tovuti ya Chadema kwa kusudi la kujua maadhimio yao...

Now we are getting somewhere. I have seen 2 reasons just from your one statement why the oposition doesn't get elected.

1.You are giving me a web link. That is fine. BUT....do majority of Tanzanians have access to the internet? While the opposition concentrates on mainstream voters CCM concentrates where the majority of people are....VIJIJINI & WATU WA HALI YA CHINI who make up a huge chunk of the electorate.

2.Since yo gave me a link to Chadema & not any other party I'm assuming you are wowed by Chadema. If so kwa nini "mwenye shida asimfuate mganga?" Is this the mentality of our opposition? That people will follow them where they are & not the other way around?
 
Hivi ukiondoa Dr. Slaa jamani semeni ukweli nani mwingine mnamsikia japo akikohoa?

na ukitaka upime performance , basi Mtikila kawapita wote!

usitegemee wapinzani wote watakuwa kama dr slaa au mtikila au Rashid Muhamad.Katika jimbo bora tuchague avarage opposition MP kuliko the so called Best perfoming CCM MP. kuwa CCM kunawa-neutralise hawa wanaoonekana kuwa ni wabunge bora kuliko wale waupinzani.

Kuongeza idadi ya wapinzani hata wanaolala bungeni ita add value kuelekea mabailiko ya kweli.

Kuanza kuwatafuta wapinzani kwa kuwalinganisha na Dr slaa, au M, Rashid sio sahihi.
 

I agree with you mkuu. Hata mimi hapa kuna watu walisha anza kuruka na kusema mimi ni "mpenda mafisadi". The whole point of debate ni exchange of ideas. Wote tungekua na mawazo sawa basi kusingekua na JF.

Umepoint out kitu na hicho ni kwamba upinzani hamna wa kumchagua. Well sadly vyama huongozwa na watu pamoja na serikali yenyewe. Sasa kama upinzani haina watu electable hilo tayari ni tatizo kubwa. Upinzani unabidi uattarct watu wenyewe uwezo na njia ya pekee ya kufanya hivyo ni kuwaoyesha kuwa they have a fighting chance. Hamna mtu mwenye akili timamu ata poteza muda kwenye lost course. Upinzani unabidi ujiangalie upya. Unatia huruma. Hatuna wapinzani bali wasindikizaji.
 

Tusiuhukumu upinzani kabla hatujaupa madaraka!
 
unachosema ni ukkweli kwa sababu unaagalia shilingi kwa upande 1ja.Mbona wapinzani wamejitahidi kuonyesha kwa nn uwachague.Kashfa BOT, EPA,RADAR wamekuwa wazi kuzikemea bungeni. try too look the other side of the coin[/B]

Siangalii shilingi kwa upande mmoja bali natoa hoja ya upande mmoja na mwenzangu kama wewe akitoa upande mwingine wote hunufaika na kuelimika. Sikusema maneno yangu ni sheria ndiyo maana nikasema ni maoni yangu. Kuhusu BOT,EPA, RADAR my friend hizo zime fumuliwa zote na chama kimoja i.e. Chadema na nyingi ni za mtu mmoja aitwae Dr. Slaa. Sijaona much evdence kwamba hizo kashafa zilikua juhudi za chama bado naona ni juhudi za mtu mmoja. Mtu mmoja bado hanipi sababu za kukichagua chama kizima.




Ok.....CCM ni reactive kwa nani? Maana mimi nimesema upinzani ni reactive to CCM je CCM ni reactive to who? Huja explain bado.



Yes kuna mfumo huo. Kulikuwa na mfumo unaopendelea chama tawala Kenya mpaka juzi kati tu ila wenzetu waliweza kuovercome. Kama tatizo lia julikana upinzani unafanya nini kupambana na hili? Kama Kenya waliweza sisi tushindwe nini? CCM ni tajiri maybe because muda mrefu wao walikua chama pekee, lakini ni sisi tuliotaka upinzani tukijua yote haya. Tuta lia lia mpaka lini? What are we doing about it?







Mzee kwa kusema baadhi haya maneno hata CCM wamo wa aina hii. Zaidi CCM wamezoea wizi kiasi cha kwamba wanakwapua mchana kweupe. Huoni kuwa wapinzani hata wakiwa mafisadi wataiba kwa aibu.CCM hawana aibu ya kuiba

BTW mkuu mimi siyo hata mzee. Usi shangae kukuta mimi ni mdogo sana kwako. Ni kijana tu mwenye muamko wa kisiasa. Mkuu mwizi ni mwizi tu. Ina maana una endorse "mwizi" ampokee "mwizi" mwingine? Na mwizi huiba kutokana na kilichopo karibu yake. Uta nihakikishiaje mpinzani mwizi akiingia given the chance nae hata iba kama wezi wa CCM wa sasa? Na je mimi niamini vipi mtu ambae ana weza kuiba kidogo hata iba kingi akipata nafasi?




Sijasema ni chama bora bali ndiyo chama nafuu kati ya tulivyo navyo. Na kama Chadema ikishindwa kumuadhibu mtu hicho ndicho unadhani kinafaa kuongoza serikali? Ukubwa wa umri si sababu. Kumbuka utu uzima siyo umri bali upeo na busara.

NB
kuliko kumchagua mbunge mbovu wa CCM bora uchague mbunnge mbovu wa upinzani . Ata Add value,efectiveness na Efficency ya bunge

Mbunge mbovu ni mbunge mbovu haijalishi anatoka CCM au upinzani. Mbunge mbovu haongezi value yoyote wala efficiency bali nae ni strain katika economy kama mbnge mbovu wa CCM.

Nashukuru mkuu kwa maoni yako na walau wewe ume jaribu kutoa hoja kliko wengine walio kuwa wakipinga tu bila msingi wowote. Natumai huu mbadilishano wa mawazo utaendelea.
 
Una maanisha chama mbadala kwenye uchaguzi?
what is your point, najaribu kuelewa lakini bado sijakupata/
 

I agree. Kama jimboni the best candidate ni mpizani tumpe. Tuangalie merit. But let's look at the larger picture....the ultimate goal of every political party. Je kuna chama cha upinzani kinacho faa kuiongoza serikali? Na ni kwa mantik ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…