John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Sababu za Kutoa Sadaka
Sadaka ni Nini
Moja ya nguzo muhimu sana katika imani ya Kikristo ni sadaka, Sadaka ni nguzo muhimu sana, kwa sababu hata Kristo mwenyewe alifanyika sadaka kwa ajili yetu ili sisi tuokolewe. Kama Kristo asingejitoa nafsi yake kwa ajili yetu sisi, tusingekuwa popote, tungekuwa ni wana wa Jehanamu wote, hakuna hata mmoja ambaye angepona.
Sadaka siyo mchango. Mchango ni kitu unachotoa kuchangia jambo fulani liendelee mbele lakini sadaka, ni kitu kinachohusisha wewe kupungukiwa ili mwingine aongezewe, au wewe kupoteza ili mwingine apate. Hiyo ndiyo maana ya sadaka. Hata hivyo, Biblia inasema utoaji wa kweli ni kujitoa nafsi yako kwanza kwa Mungu kama dhabihu mtakatifu ya kumpemdeza Mungu.
Sadaka ni ibada kamili kati yako wewe na Mungu aliyekuumba. Unamtolea Mungu ili sadaka yako inene kama ya Abeli (Mwanzo 4:4-5). Na ili sadaka yako inene mbele za Mungu, kwanza mtu asijue umetoa kiasi gani. Mathayo 6: 2-4 inaelezea, usishauriwe na mtu, hata mtumishi, utoe kiasi gani.
Matendo 20:35 inasema ''Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea'. Ukitoa, utasababisha aliyepokea amshukuru Mungu na jambo hilo kukuongezea kitu wewe mtoaji maana wewe ndiye chanzo cha shukrani hiyo. Utoaji wako utakupa sifa na heshima.
Jambo muhimu ni kuwa Mungu hataki matoleo ya ubatili. Matoleo ya ubatili ni sadaka isiyo sahihi. Kwa mfano, huwezi kuiba fedha halafu ukasema ''ngoja niipeleke kanisani ili Mungu anibariki zaidi''. Hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe, na huo ni ubatili mkubwa. Matoleo ya ubatili ni pamoja na kupeleka sadaka isiyo sahihi. Kwa mfano, una shilingi laki moja mfukoni, lakini unamtolea Mungu shilingi mia tano. Hiyo siyo haki, na kumbuka kuwa hata hiyo laki moja uliyo nayo ni Mungu amekupa. Hapa Mungu anaangalia utii wetu, siyo kwamba ana shida na fedha.
Faida za Kutoa Matoleo Sahihi kwa Mungu
Ukitoa utakuwa unaweka hazina mbinguni ambapo hakuna atakayeiondoa
Hazina ni ni mali au vitu vya thamani vinavyohifadhiwa eneo zuri kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Mathayo 6:19-21 inasema ''Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako''.Kutoa matoleo sahihi ni kuweka hazina mbinguni.
Kiroho, tunaweza kusema kuwa hazina ya wateule wa Mungu ni mahali mbinguni ambapo matokeo ya utoaji wa mteule huonekana na kufanyiwa kazi yenye manufaa sasa kwa mteule huyo na baadaye kwenye uzima wa milele. Wako Malaika wa Mungu walio katika kitengo cha uhazini mbinguni, kiasi kwamba hakuna hazina ya mteule inayoweza kupotea, wala kuibiwa wala kuondolewa.
Kitendo cha wewe kutoa maana yake unamjaribu Mungu ili akukuze zaidi
Malaki 3:10-12 inasema ''Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi''.
Kuna watu, shetani huwapangia magonjwa mara kwa mara, lakini hawaumwi kwa sababu Mungu anamkemea mharibifu wa afya zao kwa sababu tu ya utoaji wao sahihi na kwa uaminifu na upendo wa fungu la kumi na sadaka. Mungu anataka tumjaribu kwa matoleo.
Mungu ameahidi madirisha ya mbinguni kufunguka. Madirisha ya mbinguni yakifunguka kwako kwa sababu ya utoaji wako sahihi na wa kudumu, hakika huko mbinguni zitatoka baraka nyingi na upendeleo katika kazi, uchumba, ndoa na chochote kinachokuhusu. Mungu anaposema atakubariki kwa sababu ya uaminifu wako siyo kwamba atakubariki fedha tu, bali ni mambo mengi ya kukubariki.
Ukweli ni kwamba hakuna aliye mwaminifu hata mmoja, ambaye akimtolea Mungu habarikiwi, bali wote hubarikiwa katika maeneo mbalimbali katika maisha yao.
Utoaji wako utakuwa sababisho la wewe kupata kitu fulani kutoka kwa Mungu
Mwanzo 8:16-22 inasema “Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe. Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi. Basi Nuhu akafanya kama alivyoagizwa, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya''.
Mungu, baada tu ya kuikubali sadaka ya Nuhu, alitoa baraka. Mungu alisema Hatailaani nchi wala kuipiga kwa gharika dunia yote, Hiyo ni baraka ya Mungu inayodumu hata leo kwa sababu ya sadaka za Nuhu. Hata iweje leo, haiwezekani dunia nzima kuzama kwenye maji kama ilivyotokea wakati wa Nuhu, hiyo ni baraka kwa Nuhu na uzao wake wote, ambao ni mimi na wewe.
Mungu akiikubali sadaka yako, hakika tarajia muujiza wa Mungu maishani mwako.
Kuna njia nyingi za Mungu kukubariki kama utazingatia utoaji wa sadaka safi na zaka sahihi. Sadaka inaweza ikafufua yale yaliyokufa maishani mwako. Hata leo, yako mambo yaliyokufa maishani mwako, lakini sadaka yako inaweza kuyafufua. Utoaji wako unaweza kuzifufua baraka zako zilizokuwa zimekufa.
Sadaka yako itakuwa ukumbusho mbele za Mungu
Matendo 10:1-8 inasema ''Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtawa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, kuna nini, Bwana? Akamwambia, sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu. Sasa basi, peleka watu Yafa, ukamwite Simoni, aitwaye Petro. Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda. Na yule malaika aliyesema naye akiisha kuondoka, Kornelio akawaita wawili katika watumishi wake wa nyumbani, na askari mmoja, mtu mtawa katika wale waliomhudumia daima; na alipokwisha kuwaeleza mambo yote akawatuma kwenda Yafa''.
Kuwa ukumbusho siyo jambo dogo, Malaika alishuka kwa Kornelio kwa sababu ya utoaji wake sahihi wa matoleo kwa Mungu.
Ni neema ya Mungu malaika aje kwako ametumwa na Mungu. Sadaka sahihi inaweza kumfanya Mungu amtume malaika. Malaika wa Mungu akishuka kwako ni kwa kusudi la Mungu. Sadaka kuwa ukumbusho kwa Mungu ni jambo la muhimu sana.
Hebu mtolee Mungu sadaka sahihi. Atakubariki katika maisha yako.