Bwana Mpanzi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2019
- 200
- 195
Cocoa hustawi katika maeneo yenye hali ya hewa ya joto kiasi na mvua nyingi au unyevu kutokana na uwepo wa chanzo kikubwa cha maji iwe mto mkubwa au ziwa au Bahari. Maeneo yanayofaa zaidi ni:
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Ruvuma, Njombe na Songwe): Maeneo haya yana udongo wenye rutuba na mvua za kutosha. Pili uwepo wa ziwa Nyasa unasaidia sana unyevu katika majira tofauti ya mwaka.
Pwani (Tanga, Dar es salaam, Morogoro, Lindi, na Mtwara): Maeneo haya yana hali ya hewa ya unyevunyevu inayofaa kwa cocoa. Hii inatokana uwepo wa vyanzo vya maji kama mito Wami, Ruvu, Rufiji, Ruvuma, Kilombero, Mbwemkuru na Bahari ya hindi.
Kanda ya ziwa (Kagera, Geita, Mwanza, Mara): Hali ya hewa ya joto na mvua ya kutosha inachangia ustawi mzuri wa hi-fi. Na uwepo wa maziwa madogo na mito kama Mara na Kagera na ziwa Victoria.
Magharibi (Kigoma chini,Katavi na Mpanda): Hali ya hewa ya joto na unyevu na uwepo wa mvua. Chanzo cha maji ni mto Malagarasi na maziwa ya Rukwa na Tanganyika
Kanda ya kati (Dodoma) hasa maeneo yenye vyanzo vya kudumu kama ukanda wa Mtera.
2. Uhakika wa Soko la Cocoa ni 100%
Soko la Ndani: Cocoa inaweza kusindikwa kuwa bidhaa kama vile siagi ya cocoa, poda ya cocoa, na bidhaa za chokoleti. Hii inakidhi mahitaji ya viwanda vya ndani vya vyakula na vipodozi. Kwa sasa tuna mdau mmoja Tanzania anayeprocess, tuna nafasi ya kuwekeza hata huku pia, mahitaji ni mengi.
Soko la Nje:
Mahitaji ya kimataifa ya cocoa yameongezeka, hasa Ulaya, Marekani, na Asia. Nchi kama Ivory Coast na Ghana zinaongoza ulimwenguni lakini kutokana na mporomoko uliotokea katikati unaweza kuipa Tanzania nafasi ya kuinuka na kuongoza safari hivyo kuna nafasi kubwa ya Tanzania kuingia kwenye soko hili ikiwa na bidhaa zenye ubora maana tuna Cocoa bora sana.
Ushirikiano kupitia mikataba kama AGOA na EU inaweza kusaidia kufikia masoko ya nje.
3. Fursa za Kilimo cha Cocoa
Mahitaji Makubwa: Cocoa hutumiwa katika tasnia ya vyakula, vipodozi, na dawa, hivyo kuleta uhakika wa soko.
Mahitaji yake ni makubwa kuliko tunachokizalisha, yaani kutoa wastani wa 5000 mTonnes kwa soko la nje bado hatukidhi mahitaji pamoja na mahitaji ya viwanda vya ndani.
Ubora wa Mazingira ya Kilimo Tanzania: Maeneo mengi yana hali nzuri ya kilimo bila gharama kubwa ya umwagiliaji.
Fursa za Kuweka Thamani: Kusindika cocoa nchini kunaweza kuongeza thamani na kukuza ajira.
Ufadhili: Benki kama TADB hutoa mikopo kwa wakulima wa mazao ya biashara na hili bila ushahidi hata benki zingine zitakuwa zimeshaweka macho kutokana na historia ya miaka kadhaa ya ununuzi wa hili zao nchini.
Ushirikiano: Mkulima anaweza kushirikiana na Taasisi kama SAGCOT na taasisi nyingine za kiserikali pamoja na binafsi kama sisi.
Imeandaliwa na kuandikwa na;
Agronomist Mtangi
0714600575 || 0789048661
Info@shambainitiatives.co.tz
Kwa ushauri, miongozo na miche bora ya Cocoa.