Sababu za kwanini Chato haina hadhi ya kuwa Mkoa

Sababu za kwanini Chato haina hadhi ya kuwa Mkoa

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Zimeibuka agenda ati Chato inatakiwa ipandishwe hadhi kuwa Mkoa ili kuridhisha mizimu na kujitakasa kisiasa Kwa watu wa Kanda ya Ziwa

Me natokea Kanda ziwa ila siungi mkono hii hoja ya Chato kuwa Mkoa

1. Utitiri wa Mikoa
Chato itapana na Mikoa ya Geita, Shinyanga na Kagera, ambayo ina ukaribu sana kiumbali
Mfano kutoka Geita Manispaa hadi Chato ni km 70 yaani Kwa gari dakika 30 unakuwa ushafika au masaa 3 kutembea Kwa miguu
Hii inakosesha Radha

2 Shughuli za kiuchumi ziko chini
Kimapato Chato Bado ipo Chini, japo Magufuli alijaribu kujenga Uwanja wa ndege, VETA, Hospital ambavyo kimsingi Kwa Sasa vimejifia
Na Chato inanuka umasikini, wakazi wa Chato wanamtegemea uvuvi mdogo na bandari ya Nyamirembe

3 Chato ipo Pembezoni mno

4. Chato hamna miundo mbinu, ya kuifanya uwe mkoa
Hizo Taa za barabarani zipo center tu
Ila ukienda Kibehe, Bilele, Nyamirembe ila njia ya kuingia biharamlo ni pori hasa

5 Idadi ndogo ya watu na Makazi duni
Mkoa wa Chato, utakuwa na idadi ndogo ya watu, wengi ni wazawa maana mtu hawezi kuhamia Chato akafanyeje hasa
Kigezo cha kuwa Mkoa ni watu wengi

6 Utakuwa upendeleo.
Yaani Ishindwe kuugawa mkoa mkubwa kama Morogoro, Ruvuma, Tabora, Lindi uje uigawe Geita ambayo ni ndogo na ilimegwa hivi majuzi kutoka Mkoa wa Mwanza sio haki

7. Migogoro ya rasimali
Kuigawa Chato na kuipa hadhi ya mkoa itakuza huu mgogoro
Mwanza Jiwe alitudhulumu mbuga yetu watu wa Kagera na kuipeleka Chato kinguvu na kuipa jina la Burugi Chato ambapo asilimia 100 hii hifadhi ipo mkoa wa Kagera
Itakuwa ngumu kutenga mipaka ya ziwa Victoria baina ya mkoa wa Chato, Geita na Kagera

8 Italeta ukabila
Mkoa Huwa una kabila mbili au Tatu
Sasa mkoa wa Chato utakuwa na Makabila sio Chinia ya 10
Mfano
Chato- wazinza
Katoro- wasukuma
Muleba - wahaya
Biharamlo -wasubi
Ngara - wahangaza na washubi
Runzewe- wanyantuzu

Sisi watu Ngara, Biharamlo, Muleba, Runzewe,Bukombe, na Katoro hatupo tayari kutupeleka kwenye hilo li mkoa lenu la Chato, sisi hatulitaki, tunataka mikoa yetu ya asili
 
Umesaha kabila la waha,kuanzia buseresere,butengo,bwanga,iparamasa,buziku,bwera,runazi,waha ni wengi sana
 
Back
Top Bottom