Sababu za kwanini MaT.O (Tanzania one) hawafanikiwi kimaisha!?

Mkuu HUMBLE umeongea jambo la msingi sana. Kuna genius mmoja aliwahi kusolve a complex equation akaahidiwa kulipwa dola milioni moja lakini akazikataa. Hawa jamaa wanakuwa na matatizo sana kwa kweli.
 
Yap, kuna entrepreneurs na working class na minimum wage labourers, level za society hizo, so very bright mind zikiwa entrepreneurs ndo unakutana na akina gates na zuckerberg na buffet, ila zikiwa white-collar working class unakutana na akina majority ya hiyo population, ila hamna minimum-wage working class ya bright minds, haijawah kutokea
Education wanavyosema ni key to success ni kweli, maana kuna watu niliosoma nao walikua na mentality ya "kusoma bongoo, mchawi pesa, mbona kuna watu hawajasoma wana pesa" sahv nakutana nao kitaa tu wengine mateja.
 
HKL tafadhari msaada tutan....!!!!!
 
Nakumbuka wakati tukisoma sekondari kuna jamaa zangu walikuwa hawajiwezi kabisa lakini sasa wao ndio wanamiliki maghorofa mjini huku sisi tukiendelea kusaga lami. Ama kweli kufaulu shule sio kufaulu maisha.

Ukitaka kuamini hili tazama maisha wanayoishi maprofesa ukilinganisha na wanafunzi wao, tena waliodisco. Ndipo utagundua ni bora kuwa kilaza kuliko kuwa genius.
 
Kama unaamini kufanikiwa kimaisha ni kuwa na magari hela na nyumba hapo umefel na ndio wanaokufa kwa depression wenye izo mindset "I think everybody should get rich and famous and do everything they ever dreamed of so they can see that it's not the answer" jim carrey
 
Mi naona mtaan kwenu mambo yapo tofauti na mtaan kwetu, maana huku waliofeli ndo wezi, mateja wa road, wengine nishawazika kwa wizi, sasa labda wangeishi mtaan kwenu wangetoboa maisha
 
Ila kwanini ma prof wa bongo wana maisha ya kawaida sana ingali wanalipwa almost 6+ million per month...
 
Ila kwanini ma prof wa bongo wana maisha ya kawaida sana ingali wanalipwa almost 6+ million per month...
Wapo bize kuandika thesis, research, na other academic responsibilities, ukiwa professor una wajibu kwa board yako na profession yako, hawanaga muda wa kula bata, maana akili zao hazina matamanio ya materialism km normal person km mimi
 
Yaani huu uzi umeniumiza maneno mnayoanza kutumia,kwaherini naona hapa si mahali kwangu tena,ulikuwa kwa ajili ya utani naona sasa matusi yanatawala.
Sasa kuna neno gani la ajabu kwny huu uzi,ma..pu..mbu au?
 
Mi naona mtaan kwenu mambo yapo tofauti na mtaan kwetu, maana huku waliofeli ndo wezi, mateja wa road, wengine nishawazika kwa wizi, sasa labda wangeishi mtaan kwenu wangetoboa maisha
Mkuu sio mtaani kwetu tu. Huu ukweli una-apply mahali popote pale.
 
Hawana lolote hawa walikuwa wanatubania tuu nafasi ya kwanza na kujifanya kukokotoa hesabu ngumu, lakini wakishamaliza vyuo kwenye maisha wanakuwa wa kawaida tuu, hawana contribution yoyote itakayowaonyesha kuwa sio wa kawaida
 
Napingana na point yako. Ukikrem ni rahis sana kusahau kuliko ukielewa. Wakati niko chuo, kuelewa kitu kuliniokoa sana maana nikielewa kusahau ni ngumu kuliko kukremu.

Nikikrem lazima nisahau tu haina namna


Inaonekana hujaelewa hoja yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…