Sababu za kwanini MaT.O (Tanzania one) hawafanikiwi kimaisha!?

Hahahahhaha kuna kaka mmoja tumesoma wote alivyofanya mtihani wa form six amekuwa kichaaa mpaka leo na matokeo yalitoka safiii PCM
 
Hii ni hatar zaid ya hatar, wakifika kitaa wanakuta mambo co kabsa, vyuma vinakutu mzee baba kila kona
 
Nelson Mwombeki upo sahihi binafsi wote waliokuwa vipanga ninaowafahamu wapo vizuri tu na tunajuana huyu yuko wapi huyu yuko wapi ,kama mtu hajawa sawa jua kuna mtihani umemkumba karudi nyuma ila nae anajipanga akinyanyuka hapo atakuwa sawa tu,mwenye akili ana akili tu.Naamini kabisa injinia yuko safi humu anatuchora tu.
 
Mbassa jr hapa utacheka simu ikilia naikimbilia labda muamala umethibitishwa,halafu wakala wa mtaa anawahi kufunga,ngoja niendelee kusubiri nitaleta update tu najua injinia hawezi kutuangusha vipanga wenzake
 
Mkuu sio mtaani kwetu tu. Huu ukweli una-apply mahali popote pale.
Kwetu hiyo theory imegoma ndomana nasema hivyo, na wote niliosoma nao wale tuliokuwa tunapiga doji class wapo mtaani hawana hili wala lile, ndo hali halisi ya upande wetu kwenu iko tofauti ila kwetu ndo iko hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…