Sababu za matokeo ya kidato cha nne 2012 kuwa mabaya

Makomangilo

Member
Joined
Oct 14, 2011
Posts
20
Reaction score
3
SABABU ZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUWA MABAYA NI HIZI HAPA:
  1. Shule za sekondari kuhamishiwa TAMISEMI. Watendaji wa Tamisemi badala ya kusimamia taaluma mashuleni, wanasumbua na kuharibu taaluma kwa (a) kuingilia utawala wa shule katika kuendesha shule; (b) kusumbua na kusambalatisha walimu kila wakati ambapo wanawakatisha tamaa na kuwaondolea utashi 'Morale' wa kufundisha (c) kukata au kuwanyima mafao yao kwa makusudi.
  2. Wanafunzi kutotimiza majukumu yao ya kujifunza. Jamii na wazazi waelewa kuwaacha tu watoto wao kuendelea na uzembe.
  3. Wanafunzi kutokuwa na nidhamu mashuleni na jamii kuwakingia kifua wanapokosa wasipewe adhabu. Kitu hiki huhamisha fikra za mwanafunzi kuwa mtii katika kusoma na kuwa kichaa na mwenye kibuli.
  4. Watoto kuachiwa kutumia simu mashuleni na maeneo mengine ambapo muda mwingi husikiliza muziki, au huchati na rafiki zake au hupiga simu za kutongozana na wapenzi wao. Muda huu ambao ni wa manufaa kielimu hutumika isivyo. kwa mwanafunzi kuacha kusoma na kufikiria kusoma hawezi kufaulu mtihani. Mwanafunzi ameweza kuandika wimbo wa muziki kwenye mtihani ambayo ni kazi ngumu ya kutumia akiri nyingi; kumbe akiri hiyo hiyo ageihamishia kwenye somo la kiswahili angeweza kufaulu hata kama hakuna mwalimu. wimbo wa muziki ameandika bila kufundishwa, hata kiswahili angeweza kujifunza bila mwalimu kwa kutumia vitabu na muhitasari.
  5. Walimu kutolipwa mishahara inayoshotosha mahitaji yao kama wafanyakazi wengine wenye elimu sawa na wao, mfano TRA, AFYA N.K. Hii ingewafanya walimu watulie, wafanye kazi ya ualimu vizuri na kuwaza namna ya kuwaelimisha wanafunzi kwa matokeo ya kufaulu.
  6. Walimu kutotambuliwa na kuheshimiwa na jamii. Jamii inawanyanyasa sana walimu kwa sababu ya msalahi yao duni. Inafikia mahala baadhi ya walimu akiulizwa na mtu ambaye hamufahamu kuwa anafanya kazi gani, huficha kazi zao na kutaja kazi zingine zenye masilahi makubwa ili kulinda heshima ya utu wake au ili apatiwe huduma nzuri. Kitendo cha mwalimu kutotambuliwa na jamii naye anaondoa wito wake wa kufundisha wanafunzi. Anabakiza tu kuingia darasani kama muhubiri ambapo wasikizaji wake hana shinda ya kuwapima kama wamemwelewa na yale aliyosema wameyashika au la. Dawa ni kuwalipa walimu malipo yanayowatosha kuishi vizuri. Mtu fukara katika jamii hana thamani kwa watu kiushirika (social life).
  7. Ukosefu wa walimu wa hisabati, sayansi, maabara na vifaa vya kutosha vya maabara katika shule nyingi za serikali. Watoto wawapo shuleni, wanatakiwa wajifunze mafunzo yaliyopangwa kujifunza wakati ule ule uliopangwa kujifunza. kwa sasa watoto hawajifunzi wakati ule ule ulipangwa na wengi hawajifunzi kabisa. Mwanafunzi anapofanya mtihani wa somo ambalo hakufundishwa ipasavyo au hakufundiwa kabisa, hawazi kufaulu bali hufeli.

Yapo mambo mengi LAKINI MAKUBWA NI SHULE ZA SEKONDARI KUHAMISHIWA TAMISEMI NA MASILAHI DUNI YA WALIMU.
 

dah! Kweli
hilo nalo neno
 
Mdau umesahau moja,ambayo kwa kiswahili mi siijui ila kwa Kiingereza inajulikana kama:lack of clear and consistent curriculum which is used to teach in secondary schools. Kila shule inatumia mtaala wake likini mtihani unatungwa kwa kujzingatia mtaala mmoja tu hivo kujwafanyha wale wanafunzi walotumia mtaala ambao haukutumika katika kutunga mtihani wakibaki kujfeli na kupata zero.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…